Something must be extremely wrong with CCM.Why all these deaths.CCM take care.
(UPDATED 13:30 - October 16, 2015)
Kwa mujibu wa Jerry Silaa (aliyekuwa Meya wa Ilala):
Heshima kwenu Wakuu,
Kuna habari zinasambaa kwamba kuna Chopa ilikua imebeba Makada wa CCM imepotea ikiwa inaelekea Njombe.
Taarifa zinasema, wakati inaondoka ilishindwa kupaa lakini mwisho wa siku ikawa imepaa.
Hadi sasa sijajua kipi ni kipi. Hivo nimeileta hii habari kama tetesi ili mwenye taarifa za mwanzo atujuze.
Asanteni sana.
========
UPDATES:
- JamiiForums imejaribu kumtafuta Filikunjombe kupitia simu yake ya mkononi bila ufanisi
- Taarifa zinabainisha kuwa kweli kuna ajali ya helikopta imetokea lakini mpaka sasa hali za waliokuwa kwenye chombo hicho hazijajulikana
- Baadhi ya abiria wanaodaiwa kuwa ndani ya chombo hicho ambacho kinasemekana kilikuwa kikirushwa na Kapteni Silaa ambaye ni baba Mzazi wa Jerry Slaa, ni Haule (ndugu yake Filikunjombe), Deo Filikunjombe, Mtumishi mmoja wa Halmashauri mojawapo ya Mkoa wa Njombe...
- Jitihada za kufika eneo la ajali zimekuwa ngumu kwakuwa ni eneo ambalo si rahisi kufikika nyakati za usiku; juhudi zinaendelea
- Helikopta iliruka saa tisa ilitakiwa itue saa 11 Iringa. Status ni MISSING. Casualties sio CONFIRMED kwa kuwa ni porini mpaka kesho gari likifika eneo la tukio sababu kuna mto na watu wa camp na rangers hawawezi kuvuka usiku huu.
=> Katika Kituo cha Luninga cha ITV taarifa ya habari saa tano usiku wamethibitisha kutokea kwa ajali ya helkopta ambayo Deo Filikunjombe alikuwa anasafiria lakini wanadai yuko salama
================
- Ndege inayodaiwa kuanguka leo katika Hifadhi za Selou...
View attachment 299341View attachment 299342View attachment 299343View attachment 299344