TANZIA Helikopta yaanguka, aliyekuwa Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe na wengine wapoteza maisha!

TANZIA Helikopta yaanguka, aliyekuwa Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe na wengine wapoteza maisha!

(UPDATED 13:30 - October 16, 2015)

Kwa mujibu wa Jerry Silaa (aliyekuwa Meya wa Ilala):

=========
KUHUSU MAREHEMU FILIKUNJOMBE:

- Deo Filikunjombe alimaliza shahada yake ya Mass Communication Makerere University Uganda

- Alikuwa Ripota wa Radio One na ITV kwa muda mrefu akitumia jina la " Deo Haule" akiripoti toka Kampala

- Alijiunga na Jeshi la Polisi na kufanya kazi kwa mwaka mmoja kisha akaacha kazi sababu alipangiwa kitengo cha Habari makao makuu ya Polisi na kufanya kazi chini ya Mohamed Mhina ambaye alikuwa chini yake kielimu.

- Alipotoka Polisi, alijiunga na World Vision kama Communication/ Information Officer na kufanya kazi kwa miaka kama minne hivi akiwa Makao makuu Arusha na baadae akahamishiwa tawi la dar es salaam

- Alipotoka World Vision akajiunga na MKURABITA ambapo alifanya kazi kwa muda usiozidi miaka miwili akaacha.

- Baada ya kuacha MKURABITA, akafungua duka lake la electronics lipo Benjamin Mkapa Tower, opposite na Posta Mpya ghorofa ya kwanza, akafungua vituo vyake vya kuuzia mafuta Ludewa na ndipo akaanza harakati za kuingia kwenye siasa na kuchaguliwa kuwa mbunge mwaka 2010.

=========
Previously:


Heshima kwenu Wakuu,

Kuna habari zinasambaa kwamba kuna Chopa ilikua imebeba Makada wa CCM imepotea ikiwa inaelekea Njombe.

Taarifa zinasema, wakati inaondoka ilishindwa kupaa lakini mwisho wa siku ikawa imepaa.

Hadi sasa sijajua kipi ni kipi. Hivo nimeileta hii habari kama tetesi ili mwenye taarifa za mwanzo atujuze.

Asanteni sana.

========
UPDATES:

- JamiiForums imejaribu kumtafuta Filikunjombe kupitia simu yake ya mkononi bila ufanisi
- Taarifa zinabainisha kuwa kweli kuna ajali ya helikopta imetokea lakini mpaka sasa hali za waliokuwa kwenye chombo hicho hazijajulikana
- Baadhi ya abiria wanaodaiwa kuwa ndani ya chombo hicho ambacho kinasemekana kilikuwa kikirushwa na Kapteni Silaa ambaye ni baba Mzazi wa Jerry Slaa, ni Haule (ndugu yake Filikunjombe), Deo Filikunjombe, Mtumishi mmoja wa Halmashauri mojawapo ya Mkoa wa Njombe...
- Jitihada za kufika eneo la ajali zimekuwa ngumu kwakuwa ni eneo ambalo si rahisi kufikika nyakati za usiku; juhudi zinaendelea
- Helikopta iliruka saa tisa ilitakiwa itue saa 11 Iringa. Status ni MISSING. Casualties sio CONFIRMED kwa kuwa ni porini mpaka kesho gari likifika eneo la tukio sababu kuna mto na watu wa camp na rangers hawawezi kuvuka usiku huu.

=> Katika Kituo cha Luninga cha ITV taarifa ya habari saa tano usiku wamethibitisha kutokea kwa ajali ya helkopta ambayo Deo Filikunjombe alikuwa anasafiria lakini wanadai yuko salama

================

- Ndege inayodaiwa kuanguka leo katika Hifadhi za Selou...

View attachment 299341View attachment 299342View attachment 299343View attachment 299344
Ninamupmba Mwenyzi Mungu azipumzishe roho pahali pema roho za marehemu wote na awape moyo wa subira wafiwa na Watanzania wote - Amin!
 
Helcopta anayotumia deo hajakodiwa na chama... Ni yeye kama yeye.ndo maana makamba alisema helcopta zilizokodiwa na chama zipo salama zote

Ulichokua unabisha ni nini we Gamba. Huyo si February wenu.
 

Attachments

  • 1445009661999.jpg
    1445009661999.jpg
    15.5 KB · Views: 985
  • 1445009681604.jpg
    1445009681604.jpg
    16.3 KB · Views: 894
  • 1445009718666.jpg
    1445009718666.jpg
    13.7 KB · Views: 889
  • 1445009749819.jpg
    1445009749819.jpg
    12.6 KB · Views: 908
Wkt mwingine ajari ikitokea huwa naombea wangekuwemo ccm
 
Msiba wa Deo umetikisa taifa ....wanasiasa hili ni somo kubwa sana ....wananchi wanaona kazi zenu ....watawaenzi kwa namna mnayostahili ....Taifa limekuwa moja kupitia msiba huu ....
 
Wewe hukai njombe mimi nimesomea njombe
Deo ni mbunge mnafki anayetengeneza picha na video aonekane mchapakazi
Ila kiukweli ni boya sana na ni mmoja kati ya wabunge wa ndiooooo!!tunahtaji wabunge kama kina lembeli ambao wanatengwa na ccm baada ya kuzungumza ukweli

ndugu uwe mkweli, Tanzania na Watanzania tunamjua Deo kama mbunge mahiri kupata tokea. Kama humpendi basi usimzushie uongo. Buriani Deo
 
Kuna taarifa zinazagaa kuhusu janga jingine ...kutokana na sheria hii mpya ngoja tusikilizie .... Matola ameshadokeza ....
 
Last edited by a moderator:
Kuna taarifa zinatoka Kalenga hivi zinaukweli gani? kama kuna mtu ana source ndani ya Kalenga hebu apige simu.
Na mimi nimepata hizi habari kwenye whatsapp group,sasa sijui kama ni kweli,Ukweli utajulikana tu
 
Kazi ya mungu haina makosa umeodoka mpendwa wetu bado tunakuhitaji kushinda kipindi chochote lakin mungu kakupenda zaid (Mzalendo wa kweli mpenda nchi umenitoa machozi )
 
Hii helcopta "pengine" sio ya CCM ....lakini hili tukio linaweza kuiabisha Chama tawala ....
 
God have mercy on us.
R.i.p our friends, the pain is unbearable.
 
RIP Deo Filikunjombe. . . . . . .you did the job. . .We shall always remember you bro. .
 
Back
Top Bottom