January anahusika vipi?
nani ni wataalam wa kutoa go ahead iwapo helicopter hiyo ni nzima na inafaa?
mamlaka husika zilishiriki?
Always I appreciate your comments!
Mungu Baba wa rehema uliyeumba vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana, baba tunaomba rehema juu ya nchi yetu, tunaomba toba juu ya taifa letu, yamkini hatujasimama ktk zamu zetu basi Mungu tusamehe pale tulipokwenda kinyume na mapenzi yako.
Baba wa mbinguni tunatubu kwa ajili ya nchi yetu, tunatubu juu ya viongozi wetu, Baba mambo yanayotokea katika nchi yetu ni mazito na magumu kwetu, kwa ajili zetu za kibinadamu hatuwezi, Mungu simama na ujidhihirishe ktk taifa letu hasa kipindi hiki kigumu tulichonacho
Mungu tunaomba utuvushe salama ktk uchaguzi huu, tunaomba amani yako itawale ktk uchaguzi, nchi iendelee kuwa na amani ili tuendelee kupata nafasi ya kukuabudu mfalme wa amani.
Mungu wa rehema tunaumizwa mno na vifo vinavyoendelea kutokea ktk nchi yetu kwa watu tunaowafahamu na tusiowafamamu pia, Mungu tunakemea pepo la mauti ktk jina la Yesu, tunaliseta kuzimu, basi Mungu tunaomba ukapate kuonekana na kujidhihirisha, tunaamini utakwenda kututendea sana sawa na mapenzi yako.
Yote haya tunayaomba kupitia jina Yesu mwana wako aliye hai, Amen....!