TANZIA Helikopta yaanguka, aliyekuwa Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe na wengine wapoteza maisha!

TANZIA Helikopta yaanguka, aliyekuwa Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe na wengine wapoteza maisha!

makamba ndiye dalali wa hizo chopa?
kwa nini aichukulie ccm chopa mbovu/
Ccm washazoea kununua vitu vibovu washazoea 10% sasa hata kitu kama chopa wanaleta masihara na upigaji, ona sasa mpaka mpiganaji deo katutoka.
 
Jamani Deo,katika wabunge wa ccm nokiokuwa nawakubali ni wewe deo,RIP Deo tulikupenda mungu kakupenda zaidi..Deo you are promotedto glory.
 
Kuhusu taarifa ya Makamba: Makamba alipotoa hiyo taarifa kuhusu Chopa za CCM alikuwa sahihi kabisa. CCM ilikodi Chpa tatu tu, zote zipo salama hadi hivi sasa na zinatumiwa kwenye kampeni. Chopa aliyokuwa nayo marehemu Deo Filikunjombe aliikodi yeye binafsi..haikukodiwa na chama na wala chama hakikuwa na taarifa yoyote kuwa Filikuchombe (RIP) amekodi Chopa.

Hivyo basi,Makamba alitoa taarifa yake ile ili kuwatoa wana CCM na WaTanzania wote kwa ujumla wasiwasi ulioenezwa kuwa Chopa ya CCM imepata ajali na baadhi ya waliokuwamo ni katibu mkuu wa chama taifa, ndugu Kinana, taarifa ambayo haikuwa ya kweli.

Hivi mnataka kumdanganya Nani?? Hivi Filikunjombe ana pesa gani ya kukodi chopa na kuirusha mwezi mzima bila msaada wa Chama??
 
Kuna kitu nahisi hakiko Sawa mahali, Mtikila, Makaidi, mgombea ubunge wa Chadema Lushoto, mgombea ubunge Act Arusha, Emanuel Makaidi wote hao ndani ya mda usiozid mwezi mmoja, najaribu kutafakar nn kinaendelea lakini sipati majibu sahihi. Mungu azilaze roho za marehemu wote sehem salama. .
 
Kanone kauli yako ya Mungu hajakutendea haki kumchukua Deo Filikunjombe umekosea. Biblia ina sema hapo mwanzo kulikuwa na Neno, nae Neno alikuwpo kwa Mungu, naye Mungu alikuwa ndio hilo Neno. Sehemu nyingine inasema Mungu akaweka umri wa Mtu kuishi duniani, akasema itakuwa miaka 80, ila akizidi hapo atakuwa anamuiba Mungu. Sasa kufa kabla ya hapo ni shetani sio Mungu tena. Uombe toba kwa Mungu.
 
Huyo makamba anajifanya mjuaji sana! Atakuwa kaenda kukodisha helikopta hizo bila kwenda na wataalam, Anakodisha helikopta hizo utafikiri Anakodisha chup za mke wke.
January ndy wa kulaaumiwa

Alafu ukitaka kuona alivyo msanii tangia jana mpaka leo anakanusha hiyo chopa yeye haimuhusu.. Kuna kitu hapa
 
wasipojenga mahekalu mwaka huu basi hawajengi tena ,yule ivorian kampiga mzee Mapadlock na hili sakata bilion 1.7 kamakamba nako kanataka kujinasua na hili sakata, makamba amekesha usiku kucha akiomba jamaa wasife ili lawama iwe kwa chopa tu na sio uhai ,ona sasa umewaacha watu wajane na mayatima kwa ufisadi na kuiga vitu usivyokuwa na uwezo navyo ,Bwana alitoa chopa imetwaa Makamba na CCM walaumiwe

Nawaambiaga watu siku zote hakuna kitu kibaya km kuiga kila kitu kwanza waliwaponda CDM kutumia CHOPA kumbe ilikuwa Wivu mwisho wa siku wameenda kukodisha maKABURI yanayoruka Angani badala ya Chopa ona sasa walisababisha majonzi kwa Familia...
 
January anahusika vipi?
nani ni wataalam wa kutoa go ahead iwapo helicopter hiyo ni nzima na inafaa?
mamlaka husika zilishiriki?

Always I appreciate your comments!

Mungu Baba wa rehema uliyeumba vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana, baba tunaomba rehema juu ya nchi yetu, tunaomba toba juu ya taifa letu, yamkini hatujasimama ktk zamu zetu basi Mungu tusamehe pale tulipokwenda kinyume na mapenzi yako.
Baba wa mbinguni tunatubu kwa ajili ya nchi yetu, tunatubu juu ya viongozi wetu, Baba mambo yanayotokea katika nchi yetu ni mazito na magumu kwetu, kwa ajili zetu za kibinadamu hatuwezi, Mungu simama na ujidhihirishe ktk taifa letu hasa kipindi hiki kigumu tulichonacho
Mungu tunaomba utuvushe salama ktk uchaguzi huu, tunaomba amani yako itawale ktk uchaguzi, nchi iendelee kuwa na amani ili tuendelee kupata nafasi ya kukuabudu mfalme wa amani.
Mungu wa rehema tunaumizwa mno na vifo vinavyoendelea kutokea ktk nchi yetu kwa watu tunaowafahamu na tusiowafamamu pia, Mungu tunakemea pepo la mauti ktk jina la Yesu, tunaliseta kuzimu, basi Mungu tunaomba ukapate kuonekana na kujidhihirisha, tunaamini utakwenda kututendea sana sawa na mapenzi yako.
Yote haya tunayaomba kupitia jina Yesu mwana wako aliye hai, Amen....!
 
Tatizo ni kutumika mkuu. Angepunguza risk kwa kuamua kubaki jimboni tu.

Inasemekana kwamba kwavile alikuwa n uhakika wakushinda pale Ludewa na karibu watu wengi wanamkubali so alipewa Chopa kwaajili yakupiga KAMBI mikoa ya nyanda za juu kusini kunadi CCM
 
Kuna kitu nahisi hakiko Sawa mahali, Mtikila, Makaidi, mgombea ubunge wa Chadema Lushoto, mgombea ubunge Act Arusha, Emanuel Makaidi wote hao ndani ya mda usiozid mwezi mmoja, najaribu kutafakar nn kinaendelea lakini sipati majibu sahihi. Mungu azilaze roho za marehemu wote sehem salama. .
Hapo tunapowa alarm,kuna kubwa zaidi ya hili linakuja kama hujampa YESU MAISHA YAKO,HUNA BUDI KUJIKABIDHI KWA YESU
 
Ccm hawajawahi kusema ukweli toja dunia imeumbwa, usiamini neno lolote linalotoka kwenye kinywa cha mwana ccm.

Jana walisema mkuu wa majeshi anarudi hadi leo hajaonekana, wamesema ndege zote nzima huku zinaua watu.

Ccm sio ww kuwaamini hata siku moja, heri umkabidhi fisi mwenye njaa bucha na umuamini atalinda nyama kuliko kuamini mwana ccm.

Tulisha ambiwa CCM ni ile ile
 
Ccm walisema kwa mbwembwe wameingiza chopa nne kumnadi Magufuli, eti leo January anasema walikodi chopa tatu! Anaogopa nini kusema ukweli tu kuwa ni miongoni mwa chopa walizokodi!!!
 
Ovyo kabisa huyu mfiwa.. Sijui ndio panic ya msiba au vipi. Ila sioni mantiki ya kumshukuru JK na kumwacha huyu aliyehangaika kutuma watu usiku kucha. Na huyo Magufuli ndiye hapaswi kabisa kuwepo kwenye shukrani..

Usishangae mkuu JERRY anapiga PASI ndefu au naweza kusema kajitangulizia mpira ili akumbukwe sasa mtu km MAGUFULI anashukuriwa kwa lipi hasa
 
Kila kitu bungeni ni, ndiyooooo! Ndiyo nyingine zinawamaliza hata wao wenyewe bila kujua. Hakuna uwajibikaji mtu anasubiri eti akatibiwe India huku raia wakifia barabarani kwa kukosa huduma muhimu. Tuwajibike. Tuache utani. Ipo siku hata hiyo Mhimbili hutaiona pamoja na kwamba umelinda maslahi ya chama na sii ya wananchi waliokutuma. Huu ni mfano tosha. Watanzania wanamlilia Mungu sana sana. Poleni sana wafiwa. Mungu awe nanyi kipindi hiki kigumu cha kumpoteza mpendwa wenu. Apumzike kwa amani.
 
Wanaomtetea Makambako hiyo ni tàarifa ya ccm
 

Attachments

  • 1445009602871.jpg
    1445009602871.jpg
    92.7 KB · Views: 994
  • 1445009700580.jpg
    1445009700580.jpg
    58.6 KB · Views: 877
  • 1445009732439.jpg
    1445009732439.jpg
    32.1 KB · Views: 882
  • 1445009754108.jpg
    1445009754108.jpg
    28.5 KB · Views: 874
Pole nyingi sana kwa wafiwa na naamini ni watanzania wote bila kujali itikadi zetu za kisiasa tumefiwa! Tuzidi kumuomba mwenyezi Mungu atuepushe na ajali hizi za mfululizo katika kipindi hiki cha kuelekea tarehe 25 Oktoba.

Poleni sana ndugu, jamaa, marafiki na wana ccm wote!
 
kila nafsi itayaonja mauti! pumziko la amani wapendwa.
 
Back
Top Bottom