TANZIA Helikopta yaanguka, aliyekuwa Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe na wengine wapoteza maisha!

TANZIA Helikopta yaanguka, aliyekuwa Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe na wengine wapoteza maisha!

Kipindi hiki kigumu sana, Poleni wafiwa na Poleni watanzania wenzangu.
kwa kipindi kifupi tumepiteza wapendwa wetu kama
1. Deo Filikunjombe (ccm)
2. Emanuel Makaidi (NLD)
3. DR Abdallah Kigoda (ccm)
4. mgombea ubunge (act) arusha
5. Christopher Mtikila (DP)
6. Selina Kombani (ccm)
7.Mtoi (CHADEMA).
Na wengine ambao sijawataja. kwa pamoja Mungu azipumzishe roho za marehemu hawa katika pumziko la Milele. Amina.
 
kama kweli makamba aliagiza chopa mbovu ili apige dili na huku vijana wanaangamia namwomba Mungu machozi ya familia za wafiwa pamoja na wana ludewa yakawe laana juu ya uzao wake na familia yake kwa ujumla na kila mwenye pumzi aseme ameen
 
Hii chopa ilikuwa imepambwa kwa picha ya Deo na Magufuli, si Magufuli na Suluhu. Hii inaonesha kuwa, Deo ndiye aliyekuwa amekodi chopa hiyo na si CCM kama ambavyo Makamba anataka tuamini.Tafsiri yangu ni kwamba ama Deo, kama ilivyo kwa wenzake, alishaukwaa ukwasi.Au alikuwa karibu sana na wenye nazo, na sijui alikuwa anawalipa nini.Watu wa Ludewa wanaweza kuwa na majibu.
 
Wewe jamaa ni mtu wa ajabu sana...Aisee yani mmmm...
Punde kidogo nimekusoma hapo nyuma ukisema kuwa Deo yuko ok, mara ukasema shughuli za uokoaji zinaendelea fresh tu ila shida ni kwamba watanzania hawasimami kwenye position zao! ndio maana hata magari ya zima moto yanakuwaga hayana maji kwa hiyo sio kosa la serikali, mara ukasema kikwete shida yake ni kwa vile ni mpole tu, mara ukasema wabunge wachaguliwe wa upinzani ila raisi awe magufuli...

Wewe jamaa ni mtu mwenye mambo vijiweni sana, ndo maana muda mwingi uko busy hapa kuwatoa watu nje ya mada, watu hapa wanatoa condolences wewe unaongelea ruzuku za chadema khaaa...sasa naona uko busy kushabikia na ku-boost ushirikina...dah!!!
Huyo .. Tony anthony akili zake kama february
 
Last edited by a moderator:
DeoFilikunjombe alikuwa mbunge wa sasa kutoka CCM ninayemkubali.#RIPDeo
 
Najiuliza hivi Makamba January baada ya kusema ndege zote za CCM za kampeni ziko salama kumbe sio kweli atatuambiaje sasa

ITV/RADIO ONE kututhibitishia kuwa Deo na wenzio wako salama salimini kumbe sio kweli tuwaeleweje??

Kuhusu taarifa ya Makamba: Makamba alipotoa hiyo taarifa kuhusu Chopa za CCM alikuwa sahihi kabisa. CCM ilikodi Chpa tatu tu, zote zipo salama hadi hivi sasa na zinatumiwa kwenye kampeni. Chopa aliyokuwa nayo marehemu Deo Filikunjombe aliikodi yeye binafsi..haikukodiwa na chama na wala chama hakikuwa na taarifa yoyote kuwa Filikuchombe (RIP) amekodi Chopa.

Hivyo basi,Makamba alitoa taarifa yake ile ili kuwatoa wana CCM na WaTanzania wote kwa ujumla wasiwasi ulioenezwa kuwa Chopa ya CCM imepata ajali na baadhi ya waliokuwamo ni katibu mkuu wa chama taifa, ndugu Kinana, taarifa ambayo haikuwa ya kweli.
 
Akili mgando kama hizi hapa duniani zinapatikana ccm tu.

Jamii tuache utani na mungu kwa sababu si mjomba wako akuna wa kumchagulia mtu wa kumchukua kwa namna yoyote anavyo yeye inafaa

Kama ulimpenda sanaaa nakushauri siku anazikwa uzikwe pamoja naye uudhihirishie umma upendo wako kwake.

USIMRUSHIE MUNGU MADONGO ASIJE AKATULETEA SUNAMI NA MAVOLKANO TUHANGAIKE NAYO.
hawa wanaokosoa kazi ya Mungu wanafikiri kuna binadamu wana haki ya maisha kuliko wengine? Ni ajali imetokea aliyekuwepo amekufa sasa kuanza kumlaumu Mungu ni ukosefu wa akili sababu mtu hawezi kuishi milele na siku yako ikifika hauwezi kwepa hata kama we rais siku hiyo utakufa tu.
 
Mungu Halaumiwi, Ni Kosa Kubwa Kusema Mungu Hajatutendea Haki, Wkt Wapo Watu Muhm Duniani Kuliko Filikunjombe Na Wamekufa.

Mshukuruni Mungu Kwa Kila Jambo.

Hata hivyo ametumia (m) ya herufi ndogo kuandika neno Mungu,sidhani kama anamaanisha Mungu wetu aliye hai.
 
Nimejiuliza sana Deo ni wapi amepata jeuli ya pesa za kukodi chopa wakati jimboni kwake hana upinzani wa kumtisha? uchaguzi wa Ludewa ulikuwa ni kukamilisha ratiba tu lakini mbunge ni Deo je ni kwa nini atumie gharama zote hizi wakati yeye anatoka familia masikini? bado najiuliza sana hili swali.

You are probably partly right. Alikuwa na upinzani mkali. Tangu jaribio lake la "kupita bila kupingwa" kushindwa, alipata upinzani mkali. Nasikia Deo alianza kampeni mwezi huu wa kumi wakati kijana wa Ukawa amesha cover ground ya kutosha.
 
Mungu wa mbinguni angalia taifa letu la tanzania maana tunapatwa na wasiwasi ndugu yangu deo filikunjombe nilikuwa nakupenda sana japo mimi ni team mabadiliko mungu ailaze maala pema peponi roho yako mwana harakati nlyekupenda
 
Wanaukumbi.

Nyeti toka Lumumba zinathibitisha pasi na shaka kuwa January Makamba anataka kukwepa lawama.

Ccm imekodi chopa kadhaa na kukabidhi kwa makada waka akiwemo Filikunjombe (R.I.P) na alikabidhiwa kupambana na nguvu ya Lowassa Iringa,Mbeya na Ruvuma.

Kwa nini alijihami toka jana kuwa iliyopata ajali haipo ktk mahesabu ya chama?

Je anakwepa kutuhumiwa kukodi chopa mbovu?

Aje hapa akanushe apewe ushahidi.

Hivi inaingia akilini Mbunge ambaye tayari ana Uhakika wa kushinda akodi chopa kwa gharama zake apige nayo kampeni?? Hizo pesa yeye katoa wapi??

January is fully responsible hapa ila analeta ujanja ujanja tu
 
Duh jamani..ccm walikuwa na kiongozi mmoja tu bungeni...nae Mungu kamchukua...wanabaki kina mwigulu? Duh sasa basi tena..pumzika kwa amani kaka..tunashukuru kwa kazi nzuri uliotufanyia watz...hakika jina lako halitafutika kwenye miyoyo yetu...kikubwa umewaachia watoto wako kitu cha kujivunia..hawatadharaulika kamwe...Baba yao alikuwa mtu wa tofauti pamoja na kuwa ndani ya nyumba ya wanyang'anyi ccm..
 
Hivi inaingia akilini Mbunge ambaye tayari ana Uhakika wa kushinda akodi chopa kwa gharama zake apige nayo kampeni?? Hizo pesa yeye katoa wapi??

January is fully responsible hapa ila analeta ujanja ujanja tu
Huyo makamba anajifanya mjuaji sana! Atakuwa kaenda kukodisha helikopta hizo bila kwenda na wataalam, Anakodisha helikopta hizo utafikiri Anakodisha chup za mke wke.
January ndy wa kulaaumiwa
 
makamba ndiye dalali wa hizo chopa?
kwa nini aichukulie ccm chopa mbovu/
 
Back
Top Bottom