ladyfurahia
JF-Expert Member
- May 10, 2011
- 14,753
- 9,575
Habarini marafiki wote humu mjengoni natumai nitapata marafiki wazuri na wema wa kuwa pamoja nao nafurahi kuwa mmojawapo wenu kwani nilikuwa guest kwa muda mrefu na sasa nimeona nijiunge rasmi kama member wa jf humu ndani. Nilifurahi sana thread zenu ambazo zimenihamasisha kuingia humu na kuwa pamoja nanyi Nilipenda sana kufuatilia post za kaka Mtambuzi , posts za dada ladyfurahia zilikuwa zinanigusa na yale mafundisho yake yalinisaidia sana ila kwa sasa sijaona kama ametoa post zingine za kutia moyo na kushauri sijui kwanini? ila samahani sana dada lady kama utaboreka kwa kukusema hapa. na vilevile nimefurahi kuwaona ndugu zangu akina Passion Lady, Sweetlady, Lady doctor, charminglady, FirstLady, Lady Unbreakable, Lady lady, Lady lulu na wengineo wengi ambao sijawataja hapa ni kutokana na ugeni huu hapa nawapenda na naomba mnioneshe ndugu zangu wengine kama wapo humu mjengoni. Nimefurahi sana kuwa pamoja nanyi. Nawapenda sana
Last edited by a moderator: