Naomba msaada kwa wataalaamu wa Kiswahili,
Ni kwamba hawa jamaa wa ndege zenye kutoza nauli ya mabasi (sina uhakika sijathibitisha hilo) yaani Fast jet wana mabango yao yanayosomeka "Hembu tupae....." Kama nilimuelewa vizuri mwalimu wangu wa Kiswahili, katika lugha sanifu haya maneno yalipaswa kusoma "Embu tupae....." Nawaombeni msaada kipi ni sahihi ili kama hawa jamaa wamechemka warekebishe kwani inakera sana kuwa na bango kubwa kama ghorofa halafu lugha imekosewa hasa kama unalazimika kuliona hilo bango angalau mara mbili kwa siku kama mimi.
Ahsanteni sana wadau!