Hembu ya Fast Jet

Hembu ya Fast Jet

Bobby

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2008
Posts
2,182
Reaction score
1,896
Naomba msaada kwa wataalaamu wa Kiswahili,

Ni kwamba hawa jamaa wa ndege zenye kutoza nauli ya mabasi (sina uhakika sijathibitisha hilo) yaani Fast jet wana mabango yao yanayosomeka "Hembu tupae....." Kama nilimuelewa vizuri mwalimu wangu wa Kiswahili, katika lugha sanifu haya maneno yalipaswa kusoma "Embu tupae....." Nawaombeni msaada kipi ni sahihi ili kama hawa jamaa wamechemka warekebishe kwani inakera sana kuwa na bango kubwa kama ghorofa halafu lugha imekosewa hasa kama unalazimika kuliona hilo bango angalau mara mbili kwa siku kama mimi.

Ahsanteni sana wadau!
 
Sio Hembu wala Embu. Ni Ebu.
 
Kinaathiri nini kwenye suala zima la usafiri,binafsi mimi nawapa, Bg Up,mbona matangazo ya TANESCO yote ni mazuri na yanapendeza.

TAFAKARI :confused2:
 
Swahili - English Dictionary | Kamusi ya Kiswahili - Kiingereza - TshwaneDJe
 
Nimerudi wakuu. EBU na hebu haya yoe yapo kwenye kamusi na yana maana mmoja.

EBU na HEBU ni maneno sahihi.:target:

Kwa kuongezea HEBU ndio sahihi ila kimatamshi HEBU hua ni rahic kutamkika kama EBU
 
Lakini pamoja na kutojua kwao lugha ya kiswahili au kujua kwao lugha kulikopitiliza bado usafiri wao wa ndege wanatoza nauli za mabasi,hilo ndio swali la kujiuliza je;wanapata faida?.Hilo ndio swali la msingi.
 
Kinaathiri nini kwenye suala zima la usafiri,binafsi mimi nawapa, Bg Up,mbona matangazo ya TANESCO yote ni mazuri na yanapendeza.

TAFAKARI :confused2:

Nawashukuru wote kwa kunifungua macho kumbe Hebu and Ebu ndio maneno sahihi na huu ndio uzuri wa JF, hata wazo la kuiconsult kamusi ya kiswahili online sikuwa nalo.

Nirudi kwako mika kati, huenda ni kweli kwamba kukosea lugha ya kwenye bango hakuathiri huduma zao lakini kwanini wakosee? Nijuavyo mimi mambo ya matangazo yanafanywa na wataalamu na mara nyingi kampuni nyingi zina outsource hii huduma so makosa madogo madogo kama haya huwa hayatarajiwi kabisa kutokea kwani kuna kuwa na chain ya watu wanahakiki kabla ya kufika mwisho wa kazi. Nimesikia serikali inataka kufungua ofisi za kufundishia kiswahili kwenye balozi zetu. Ni matario yangu kwamba watu kama hawa wa Hembu hawataenda huko kutufundisha wageni kiswahili.
 
Pmwasyoke kama umechemka vile!!? Hicho labda umesema Kinyakyusa, maana hata kwenye Kisukuma hatuna EBU!!!. Jibu sahihi ni "HEBU"

Yote mawili ni sahihi. Rejea kamsi ya kiswahili.
 
Wakati mwingine kukosea spelling hufanywa kwa makusudi kwenye matangazo ili msomaje aweze kulikumbuka tangazo na kuliweka kichwani. Kikubwa zaidi huwa inasaidia hata mtu mmoja akisoma tagazo aweze kulibeba ili akawatangazie wengine kama ambavyo mtoa mada.
Kwa mfano, mimi niko mbali na sijaliona tangazo la fastjet, lakini wewe umeshanitangazai. So, they know the language na wala hawajakosea kama unavyofikiria. Wamefanya hivyo kwa makusudi!
 
Chris yote yanawezekana nikimaanisha kwamba huenda wamekosea kweli au wamefanya deliberately kama ulivyoeleza. Lakini kikubwa ulichonishtua kwenye comment yako ni wewe kuhitimisha kwamba wamefanya makusudi kama unavyosema hapo nilipobold. Unapata wapi ujasiri wa kuyasema hayo as if ulishiriki kwenye kuandaa hilo bango? Umefanya kazi ya mgambo, polisi, hakimu na ukamalizia magereza. Hii ni hatari unless uniambie unafanya kazi fast jet lakini maneno yako pia yanalipinga hilo. Ahsante!
 
Lakini pamoja na kutojua kwao lugha ya kiswahili au kujua kwao lugha kulikopitiliza bado usafiri wao wa ndege wanatoza nauli za mabasi,hilo ndio swali la kujiuliza je;wanapata faida?.Hilo ndio swali la msingi.

kiagata hiyo ni mada nyingine kabisa, kiongelewacho ni msamiati uliotumika..ishu ya faida au hasara alieanzisha mada wala hana mpango nayo..nenda kwenye uchumi post hiyo kitu utachangiwa mawazo
 
Back
Top Bottom