issenye
JF-Expert Member
- Feb 2, 2011
- 3,788
- 5,217
ALiyekuwa mshiriki wa shindano la Tusker Project Fame, lililomalizika mwishoni mwa wiki iliyopita lilopewa jina la All Stars, Hemed Selemani amewaomba msamaha mashabiki wote waliokerwa kwa kitendo chake cha kumsemea maneno mabaya jaji Ian Mbugua.
Alisema hakutegemea kufanya kitu kile ingawa hajutii kwa kuwa ilikuwa lazima afanye vile ili kujiridhisha baada ya kuona kama amemkashifu.
Hemed alifanya kituko hicho cha mwaka kwenye usiku wa fainali za shindano hilo zilizofanyika Nairobi Nchini Kenya baada ya jaji mkali kwenye mashindano Ian kumwambia anajisumbua hawezi kuimba bora akatafute kazi nyingine afanye.
"Kitendo kile kilinikera sana na ndio maana nikaamua kumwambia ukweli,anajiona matawi wakati ni mshamba tu kwanza hana hata singo bora mimi ni Super Star wa muvi lakini mashabiki wangu wasinielewe vibaya na kwa wale walikerwa na kitendo kile nawaomba msamaha"alisema Hemed.
Alifafanua kuwa ilikuwa karibu wapigane baada ya kumalizika fainali hizo lakini watu waliwaamua na jaji Ian alikuwa anasafiri hivyo akawahishwa uwanja wa ndege.
Hii ni mara ya pili kwa washiriki wa Tanzania kufanya matukio ya namna hiyo, kabla ya Hemed kumtukana jaji Ian, mshiriki katika shindano la Big Brother Amplified, Lotus Kyamba alitolewa kwenye shindano hilo baada ya kumpiga kibao mshiriki mwenzake, Luclay kutoka Nchini Afrika ya Kusini.