Hemed awaangukia mashabiki lakini.......

Hemed awaangukia mashabiki lakini.......

issenye

JF-Expert Member
Joined
Feb 2, 2011
Posts
3,788
Reaction score
5,217
ALiyekuwa mshiriki wa shindano la Tusker Project Fame, lililomalizika mwishoni mwa wiki iliyopita lilopewa jina la All Stars, Hemed Selemani amewaomba msamaha mashabiki wote waliokerwa kwa kitendo chake cha kumsemea maneno mabaya jaji Ian Mbugua.

Alisema hakutegemea kufanya kitu kile ingawa hajutii kwa kuwa ilikuwa lazima afanye vile ili kujiridhisha baada ya kuona kama amemkashifu.

Hemed alifanya kituko hicho cha mwaka kwenye usiku wa fainali za shindano hilo zilizofanyika Nairobi Nchini Kenya baada ya jaji mkali kwenye mashindano Ian kumwambia anajisumbua hawezi kuimba bora akatafute kazi nyingine afanye.

"Kitendo kile kilinikera sana na ndio maana nikaamua kumwambia ukweli,anajiona matawi wakati ni mshamba tu kwanza hana hata singo bora mimi ni Super Star wa muvi lakini mashabiki wangu wasinielewe vibaya na kwa wale walikerwa na kitendo kile nawaomba msamaha"alisema Hemed.

Alifafanua kuwa ilikuwa karibu wapigane baada ya kumalizika fainali hizo lakini watu waliwaamua na jaji Ian alikuwa anasafiri hivyo akawahishwa uwanja wa ndege.

Hii ni mara ya pili kwa washiriki wa Tanzania kufanya matukio ya namna hiyo, kabla ya Hemed kumtukana jaji Ian, mshiriki katika shindano la Big Brother Amplified, Lotus Kyamba alitolewa kwenye shindano hilo baada ya kumpiga kibao mshiriki mwenzake, Luclay kutoka Nchini Afrika ya Kusini.

Huyu dogo ni mjinga kiasi kwamba hata hajui maana ya kuomba msamaha. Sasa hawa mashabiki anwaomba msamaha gani kama hajuitii kitendo alichofanya?

Pia anatangaza kwamba alikuwa karibu apigane na Ian? Basi huyu jamaa no hovyo sana hafai kuwafanya mambo yoyote yanayomweka mbele ya public. Ningefurahi sana kama angejaribu kurusha ngumi, kwani angeweza kupata stahili yake...Kwa sasa lazima angekuwa anacheza na mitondoo huko Shimo la Tewa!!

huwa sifagilii wabana pua kwani ndo zao hii kitu na tupa kule..

ati bora yeye ni super staa wa movie kibao...
izo pia ni movie?
POLE KIJANA PUNGUZA USHARO

dogo mpuuzi sana kuna siku km sikosei ilikuwa january mwk huu au december mwk jana alikuwa akiongea na radio clouds alipata dili ka kucheza picha na wa nigeria wakampa masharti apungue uzito na wakampa miezi mitatu dogo alivyo mbwida akachomoa eti yuko bize hana muda wa kufanya mazoezi, nilibaki mdomo wazi kucheza haya maigizo ndo kameshajiona kako biize

Hemedi alichofanya sawasawa. Huyo Jaji aelewe kuwa Watanzania hatustahamili upumbavu. Mtu kafika fainali unamwambia hajui kuimba? Huyo jaji ni mshamba kweli.

Hemedi ulichofanya sawasawa wala huna haja ya kuomba radhi kwa mshamba kama yule. Na asikanyage Tanzania.

Vijana wa Tanzania, msikubali wenzenu kudhalilishwa na haya manyang'au. Angemlamba makofi hapo hapo kwenye mashindano. Kalambwa kofi Ruksa kwa kusema hovyo itakuwa huyo mshamba.

Ya kweli hayo na unamtakia mema huyo dogo?

Fainali gani alifika wakati wote walioingia kwenye shindano walienda hasi mwisho?

Unaweza kutengeneza picha ya Hemedi miaka 10 ijayo??

labda alidhani anabishana na Yusuph Mlela, akataka kurusha konde!...

Ya kweli hayo na unamtakia mema huyo dogo?
Fainali gani alifika wakati wote walioingia kwenye shindano walienda hasi mwisho?
Unaweza kutengeneza picha ya Hemedi miaka 10 ijayo??

Hakuna cha wema hapo. Kadadadeki. Angemlamba makofi tu.

Mimi sina uwezo wa kujuwa la dakika moja ijayo wewe unanambia miaka kumi ijayo? Usinipe kazi ya Mungu. Koma.

Hakuna cha wema hapo. Kadadadeki. Angemlamba makofi tu.

Mimi sina uwezo wa kujuwa la dakika moja ijayo wewe unanambia miaka kumi ijayo? Usinipe kazi ya Mungu. Koma.

Wewe ndiye Hemedi???

Huyo hemed c nackiaga ni shoga,au aliisha acha?

Huyu dogo hamnazo.

Kama utakua umefuatilia matukio yake na mahojiano mbali mbali aliyofanya na vyombo vya habari basi utaelewa nnachosema. Jaji wana mbinu nyingi za kumpima mshiriki...
Subiri hapa bongo mtasikia kaibuka n nyengine super star wetu???

Kwani huyo Hemed nae anajua kuimba sasa zaidi ya kuuza sura tu!! Anachekesha kweli!

Jaji alisitahiri! niliona hicho kipande Jamaa aliponda utafikiri yeye ni shabiki! Jamaa anae aka-apply 3rd Newton's law of motion! Dawa ya moto ni moto!

Sasa hemed mwenyewe anaetaka kupigana ni yupi? Huyu shoga au? Mh! No
c
o
m
e
n
t

Jamani wengine hata hatuijui hiyo hemedi imekaa vipi ijapokuuwa anajisifu ni super staa.

Hebu mwenye picha yake atuwekee tafdhali

Hemedi alichofanya sawasawa. Huyo Jaji aelewe kuwa Watanzania hatustahamili upumbavu. Mtu kafika fainali unamwambia hajui kuimba? Huyo jaji ni mshamba kweli.

Hemedi ulichofanya sawasawa wala huna haja ya kuomba radhi kwa mshamba kama yule. Na asikanyage Tanzania.

Vijana wa Tanzania, msikubali wenzenu kudhalilishwa na haya manyang'au. Angemlamba makofi hapo hapo kwenye mashindano. Kalambwa kofi Ruksa kwa kusema hovyo itakuwa huyo mshamba.

duh! We utakuwa ni wamagwanda bila shaka!!

Back
Top Bottom