PreGE2025 Hemed: Watoa Rushwa, watiaji Gari Vioo Vyeusi (Tinted), wanaokwepa ibada Misikitini, wasichaguliwe mara hii!

PreGE2025 Hemed: Watoa Rushwa, watiaji Gari Vioo Vyeusi (Tinted), wanaokwepa ibada Misikitini, wasichaguliwe mara hii!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla,

"Tafadhalini sana, tusitumike vibaya, sisi viongozi ukiingia kwenye Chama cha Mapinduzi (CCM) tunatakiwa kuwa waadilifu, ukiingia kwenye Chama cha Mapinduzi unakula kiapo"

"Thamani ya Elfu 10 kwa miaka mitano unai-calculate vipi? ebu i-calculate Elfu 10 au Laki 1 kwa miaka Mitano! Alafu unakuja kulalamika, atakusikiliza vipi wakati alishakununua?"

"Chama hivi si cha Viongozi, Chama ni cha Wanachama, nyie ndio mnakuja kulalamika, unamchagua mtu alafu akipata ukupiga simu hapokei tena! Gari yake kama ilikuwa na Vioo vyeupe anaweka 'Tinted' humuoni tena akipita, Msikitini alipokuwa anakuja haji tena Msikitini anasali ndani, pakifiwa simu yake haipatikani, si ndio alikuhonga Elfu 10 huyo! Wasichaguliwe mara hii"



Video: ZANZIBAR YETU (YouTube)
 
Yeye mwenyewe anajua yupo hapo kwa sababu ya chama chake kugawa khanga, kofia na T-shirt na pilau kwa wapiga kura, kikisaidiwa na tume ya uchaguzi na vyombo vya usalama. Bila hivyo huo umakamu angeishi kuusikia kwenye redio.
 
Back
Top Bottom