EMT
Platinum Member
- Jan 13, 2010
- 14,477
- 15,325
Bei ya heroin na cocaine imeogezeka baada vita dhidi ya biashara ya madawa ya kulevya kusababisha upungufu wa madawa hayo. Kwa mujibu wa msaidizi mkuu wa kitengo cha polisi cha kupambana na madawa ya kulevya Godfrey Nzowa, uchunguzi uliowahusisha watumiaji wa madawa hayo umebainisha kuwepo kwa upungufu mkubwa wa heroin na cocaine.
Kilo moja ya cocaine kwa bei ya mtaani imepanda kutoka Sh. milioni 50 hadi milioni 55. Pia bei ya heroin imepanda kutoka Sh. milioni 45 had milioni 50 kwa kilo. Kamanda Nzowa amedai kuwa polisi wako makini zaidi sasa. Hata hivyo, amekiri kuwa kadri vita ya madawa ya kulevya inavyoongezeka, drug dealers nao wanagundua njia mpya za kuendelea kufanya biashara hiyo.
Kamanda Nzowa amesema drug dealers wanatumia makonteina yenye lebo kama "Original Coffee" na "Sugar" na wakati mwingine hata chupa zilizoandikwa pure water. Amesema kwa sasa madawa mengi ya heroin na cocaine yanasafirishwa kwa njia ya maji, na kudai polisi watageuza kila jiwe. Aidha kamanda Nzowa amesema kuwa kuanzia Januari 2013 jumla ya kilo 32 za heroin zimekamatwa, huku watu 44 wakihusishwa na biashara ya madawa hayo. Pia polisi ilifanikiwa kukamata kilo 4 za cocaine na kumatata jumla ya watuhumiwa 18.
Kamanda Nzowa ameongeza kuwa polisi imemwita na kuhoji mbunge wa Kinondoni Mh. Idd Azan kuhusiana tuhuma zinazoendelea kuwa amekuwa akijihusisha na biashara ya madawa ya kulevya. Amesema uchunguzi wa tuhuma hizo bado unaendelea.
Ziara ya ghafla ya Dkt. Mwakyembe
Wakati huo huo, Waziri wa uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe jana alifanya ziara ya ghafla katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kunako mida ya saa kumi za alfajiri. Katika ziara hiyo, alitembelea vitengo mbalimbali kikiwemo cha ukaguzi wa mizigo na abiria na kitengo cha kamera, ambako hivi karibuni kulipitia dawa za kulevya za mabilioni na kukamatwa Afrika ya Kusini.
Dkt Mwakyembe aliona hali ya ukaguzi katika eneo hilo ilivyokuwa na kubaini kuwa dawa hizo zilionekana katika mzigo lakini kulikuwa na uzembe au njama zilizotokana na maafisa waliokuwa wakikagua. Dkt Mwakyembe alipita katika eneo hilo, ambalo lilikuwa na afisa wa polisi, ambapo alielezwa kuwa siku hiyo mbwa wanaotumika kubaini dawa hizo, walicheleweshwa kufika. Kwa mujibu wa IGP Said Mwema, polisi inamshikilia mtuhumiwa mmoja kuhusiana upitishwaji wa madawa hayo.
Awali wiki hii akitoa ahadi ya kukabilina na biashara ya madawa ya kulevya, Dkt. Mwakyembe amesema kuwa atapambamba kufa na kupona dhidi ya uingizaji wa madawa hayo kupitia kiwanja hapo. "Najitoa mhanga dhidi ya biashara hivyo na siogopi vitisho vya watu, maana nilishakufa siku nyingi, hatuwezi kudhalilisha nchi yetu kiasi hicho," alisema Dkt Mwakyembe.
"Dawa za kulevya sasa zinasafirishwa kupitia kiwanja cha ndege, ambacho kimepewa jina la mtu muhimu katika nchi yetu, Mwalimu Nyerere, ni aibu kwa nchi yetu na Taifa letu, kuona uwanja huo unatumika kwa biashara hiyo, nipeni muda, mimi ndiye Waziri wa Uchukuzi, hatutakubali hali hii," alisema na kuongeza: "Pale uwanjani kuna ofisi nne, Polisi, Uhamiaji, Usalama wa Taifa na watu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, wote nimewaagiza wanipe taarifa, walikuwa wanafanya nini hadi dawa hizo zinapita uwanjani hapo?"
Wakati huo huo na kufuatia ziara ya ghafla ya Dtk. Mwakyembe kiwanjani hapo, Mkurugenzi wa kiwanja hicho, Ndugu Moses Mlaki amesema kuwa kumekuwa na ushirikiano kati ya waendeshaji wa mashine za uwanjani hapo na baadhi ya maafisa wa usalama wa taifa na hivyo kuwezesha madawa ya kulevya kupitishwa kwa urahisi kiwanjani hapo.
Habari kwa mujibu wa Daily News na Habari Leo.