jamaikatz
JF-Expert Member
- Jul 11, 2023
- 400
- 1,429
Rais wa Klabu ya Yanga, Injinia Hersi Said, amejiunga na zaidi ya wanachama 20 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliochukua fomu kuwania uteuzi wa kugombea ubunge wa Jimbo la Kongwa, mkoani Dodoma.
Mchakato wa kutafuta mgombea mpya umetangazwa kurudiwa baada ya kifo cha aliyekuwa Mbunge na mshindi wa kura za maoni za awali, Marehemu Job Ndugai, kilichotokea Agosti 6, 2025.
Hersi, ambaye awali aliwania Jimbo la Kigamboni jijini Dar es Salaam lakini jina lake halikurudishwa, amesema safari hii ameona ni vyema kujaribu tena kupitia Jimbo la Kongwa. Kwa sasa, anasubiri hatua zinazofuata za chama, ikiwemo kura za maoni ambazo zinatarajiwa kufanyika muda mfupi ujao