Herufi R na L ni tatizo kwa Rais wetu, tumsaidie

Lini Magufuli akawa msukuma? Ebu niambie ukoo wa wazila nkende kwa Kisukuma wanapatikana wapi?
Tusidanganyane apa..inaeleweka vizuri watu wenye tatizo la R na L ni Wahaya.
 
Kwani Magu ni msukuma!?
 
Tatizo la kitaifa mbona.
yaani hilo ndio jibu sahihi kabisa, unaweza kumsamehe mtu akokosea kutamka kwa ajili ya lugha zetu na sehemu uliyotoka lakini asilimia kubwa sana wanakosea katika kuandika tu sehemu ya L inawekwa R au kinyume ni tatizo la kitaifa kama ulivyosema. ukikosea kuandika tatizo kubwa zaidi inaonesha ndio uelewa wako huo kutamka unaweza ukapotezea kidogo.
 
Hili tatizo kwa kiasi kikubwa linaendelea kukua kwa kasi
Nimegundua kwa baadhi ya wazungumzaji wa kiswahili kama Zanzibar hili tatizo hakuna kabisa, baadhi ya Wachaga, Waarusha, Wameru na Warangi hili tatizo hakuna. Katika kadhia hii tunaweza sema tatizo ni lahaja na lugha zinazotuzunguka na matamshi yake

Tatizo kubwa lingine linachangiwa na aina ya Walimu ambao tunao ktk shule zetu za msingi kwa maana wao wenyewe ni wahanga wa tatizo hilo na tunajua matamshi yanahatamishwa vijana wakiwa bado wadogo
Lakini tena katika darasa la wanafunzi 200 badala ya 30 ambao Mwalimu alitakiwa awafundishe ni muda gani anaweza kuupata Mwalimu kuchunguza matamshi ya kila mtoto kuangalia kama yanalingana na kile anachoandika. Ukichunguza sana utaona wakiwa wanaandika, huandika sawasawa tatizo lipo kwenye matamshi. Lakini tatizo linazidi sana mpaka hivi sasa tunaanza kuona hata kwenye kuandika vijana wanaanza kuharibu. Tunaanza kushuhudia
Latiba = Ratiba
Kamali = Kamari
Tayali = Tayari

Tatizo hili ni aghlabu kulikuta kwa vijana wanaosoma Madrassa kwa maana ya Quran/Kiarabu kwa maana kwenye darsa zao kuna msistizo mkubwa wa kutofautisha herufi hizo
 
kuna katoto fulani kale kalikotaka kumfunga babayake kwa kuuza shamba la familia.. kalihojiwa na AYO kalitamka kuwa '' najjuwaa raisi wa Tanzania ni Magufuli... alakiniii... ni MURUNDIIII'' sasa sijui kamejuawaje.. ile lafudhi wanajuana mana haka katoto na kenyewe ni karundi kalikozaliwa tanzania
 
Wasukuma hawana R wanatumia L kwenye maneno yao mengi
mimi ni msukuma mbona naweza kutamka R au L je nimekosea hapo? tuambiane tu ukweli MAGU alikotokea ni wapi nani anajua hospitali aliyozaliwa hapa TANZANIA atutajie. alizaliwa lini mji upi.
 
Unapoongelea watu hasa public figures, waangalie kwa taaluma yao na upana wa mambo wanayoyafanya;
Mh Rais siyo Linguist, ni scientist
Mh Rais anaangalia maendeleo ya watu milioani 50+ ni dhahiri hawezi kuangalia matumizi ya R na L
 
wacha akutukane. Unaandikaje tena MZALAMO badala ya "MZARAMO". Unaonekana kama hujasoma vile! Unajilemaza makusudi bila kujua...
Sawa mkuu, nimekusoma , lakin nilichokiandika si umekifahamu ?? Hata Kama nimekosea
 
Praise team watakuja kumtetea. Wao kila jambo wanamtetea hata kama la kijinga.
Hili unalolalamikia wewe unaona ni la msingi kweli na akili zako mbwa wewe r au l inakupunguzia nini ktk maisha yako?
 
Kwa hili namtetea. Wasukuma R na L ni janga. Kwa hili Rais mnamuonea.
 
pia english yake ni very poor ukimsikiliza alipokua malawi alitema broken english inayoaibisha mpaka unajiuliza phd aliandika namna gani na akafaulu?nadhani kwa kumpoteza ben saanane haikua suluhisho
 
Sasa mtu mzima tena msomi wa PhD watu tuhangaike kumfundisha kutamka maneno kweli? Kama inalipa asaidiwe na wale walinzi wake wenye silaha nzito nzito za kivita, pmbavu😅
 
Ni ujuha wa kiwango cha Phd ya magamba ya korosho kuchanganya matumizi ya "L" na "R"!
 
Tukiwa wakosoaji inabidi tuangalie kama sisi tuko sahihi katika matumizi ya herufi sehemu yoyote iwe kutamka au katika uandishi. Tena ukikosea kuandika ndio balaa kuliko ukitamka.

Sitaki kukukosoa ila nahitaji ufafanuzi kidogo kuhusu baadhi ya herufi ulizotumia kumkosoa namba moja. Hivi kipi ni sahihi angepaswa kutamka kati ya "rite truck" au right truck. Kwa kumbukumbu ya nilichofundishwa na mwalimu wangu wa St. Kayumba ni kwamba hapo ilitakiwa iwe "Right truck" na si "Rite truck" kama ulivyoandika. Yawezekana mwalimu wangu alikosea lakini kama hakukosea basi tumsikosoe Rais wakati sisi wenyewe tuna makosa yetu ya kisarufi. Kwa mfano mimi hata unifundishe vipi huwezi kunifundisha kutamka fa badala ya va, bha badala ya ba, gha badala ya ga na mengine mengi. Huwezi kutubadili wanyakyusa kwenye matatizo hayo ya kisarufi hata tuwe na maphd kiasi gani lazima kuna sehemu tutakosea tu.
 
Nadhani ujuaji pia unahusika mkuu!mtz huwa hajifunzi kitu[emoji16]utamsikia tu "ukizaliwa mjini form 6"...hapo ndo ashajua yote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…