Hesabu ndogo sana; Kwanini Serikali iliwaamuru Polisi wasimtaje mmiliki wa jengo lililoporomoka Kariakoo hadi uchaguzi wa serikali za mitaa uishe

Hesabu ndogo sana; Kwanini Serikali iliwaamuru Polisi wasimtaje mmiliki wa jengo lililoporomoka Kariakoo hadi uchaguzi wa serikali za mitaa uishe

Tueleze wewe kama "ni dhambi" kwa hiyo CCM na serikali yake kumtaja huyo mtu ni dhambi.
Wao ndio wenye wajibu na jukumu hilo.
Na kama huwezi kueleza hilo, eleza kwa nini ifanywe kuwa siri.
Siri gani? Imeshaelezwa uchunguzi ukikamilika taarifa itatolewa, mbona kichwa chako kigumu kuelewa!
Btw wahusika si hawa hapa, ama shida yako ni nini hasa??
 
Attachments

  • IMG_3547.jpeg
    IMG_3547.jpeg
    1.1 MB · Views: 2
Siri gani? Imeshaelezwa uchunguzi ukikamilika taarifa itatolewa, mbona kichwa chako kigumu kuelewa!
Btw wahusika si hawa hapa, ama shida yako ni nini hasa??
Nani kakwambia hao ndio wahusika. Unajuwa historia nzima ya jengo hilo?
Wewe unazijuwa siri zote?
 
Nani kakwambia hao ndio wahusika. Unajuwa historia nzima ya jengo hilo?
Wewe unazijuwa siri zote?
Siijui historia, wala hizo siri!!!
Wewe unayeijua hiyo historia na siri zake zianike hapa basi!!!
Na kama hao si wamiliki hebu waseme wamiliki ni akina nani basi!!!
 
Ndivyo watawala wa chama tawala wanavyoendesha nchi hii. Makosa yanayofanywa na watu wao huwa kila jitihada itafanywa kuyafunika. Na hawaoni aibu juu ya hili, huwa wanasema waziwazi ukiwa mtu wao watakulinda. Kwa maneno mengine kuwa mtu wao kunakufanya uwe juu ya sheria.

Na kibaya zaidi, Polisi wanajua hilo, kwamba wakitaka kazi zao ziwe salama, basi waelewe kwamba watu wa chama tawala wako juu ya sheria. Hata wakiua, wakibaka, wakisafirisha wageni haramu, wakikutwa na madawa ya kulevya au nyara za serikali, wakifanya maandamano bila kibali, wakifanya lolote lile, hawapaswi kubugudhiwa.

Na Polisi wameambiwa tukio la kihalifu linapofanywa na mtu wa chama tawala basi watalitolea maelezo ambayo hayatakichafua chama tawala, hata kama inabidi waseme uongo. Kifo cha risasi au kupigwa kitabadilika kuwa kifo cha shinikizo la damu, nk.

Ndio maana basi, japo maneno makali kuhusu mmiliki wa jengo la Kariakoo yaliyotolewa na waziri mkuu, polisi walipowaambia watawala mmiliki wa jengo ni mmoja wenu katika chama, waliamriwa wakae kimya hadi uchaguzi wa serikali za mitaa upite. Jitihada hata zilifanyika kujaribu kubadilisha jina la mmiliki, na huenda zimefanikiwa tayari.

Hii ndio Tanzania yetu. Au Tanzania yao?
Ccm wahuni
 
Huna chochote unachojua kuhusu mmililik wa hilo jengo, zaidi ni habari za mtaani huko hata kama kweli mmiliki ni mwanachama wa chama tawala kwani ni dhambi?
Kiufupi umeandika nadharia eti umiliki unabadilishwa! Ungekuwa unajua mmiliki halali ambaye anafanya hizo jotihada za kubadili umiliki ungemtaja humu jamvini!!! Ungekuwa unajua taarifa za uhakika ungezianika hapa, huna lolote unalojua!!! Hili ni jukwaa huru ambalo uozo wowote unaweza kuuanika wazi!!!!
Otherwise acha jeshi la polisi na vyombo vinavyofanya uchunguzi vifanye kazi yao!!!!
Imenilazimu nirudi nyuma kutazama uliko anzia hadi hapa ulipo fikia sasa.
Sasa unacholalamikia ni nini??
Polisi si bado wanaendelea na uchunguzi wamemaliza kwani? Na kama unajua polisi wanamjua na hawataki kumtaja kwa nini wewe usimtaje basi humu..?? Btw kwani kama ni kumjua unadhani inashindikana? Wapo wapangaji walikuwa pale na wanafahamika, mafundi waliokuwa wanafanya kazi pale wanafahamika, majirani n.k wote hao unataka kusema hawamjui mmiliki..? Hayo mambo ya sijui polisi wanamjua hawataki kumtaja hizo ni stori za vijiweni tu!! Kumjua mmiliki haihitaji polisi wautangazie umma, wewe sema hapa mmililiki ni nani huyo unayesema eti polisi wanamficha unless, unachosema ni umbeya tu!!!!
Kuna sehemu unazungumzia "wapangaji, mafundi" kumjua mmiliki. Hii ni wazi inaonyesha hujui kitu kuhusu maswala ya umiliki wa majengo.

Unacho elewa wewe ni kuwa, polisi wakisha sema kitu, basi wamemaliza kwa vile wao ni watu wanao sema kweli tupu wakati wote. Sasa mtu wa aina hiyo tutamfanya nini kumbadili mawazo potofu!

Inawezekana sana ukawa ni mmoja wa hao wapindisha ukweli huko ndani ya CCM na serikalini. Kazi kubwa kwenu ni kupindisha tu na kufanya madudu kila mahali.
Serikali ya Samia imejipambanua kuwa ni serikali yenye kufanya maswala ya waTanzania gizani, kuficha ukweli, kila mahali. Na hii ni kwa sababu za ufisadi mwingi unao fanyika humo humo serikalini.
Sasa utakuja hapa unilazimishe nikupe ushahidi; wakati unajuwa mambo yenu ni ya gizani!
 
Siijui historia, wala hizo siri!!!
Wewe unayeijua hiyo historia na siri zake zianike hapa basi!!!
Na kama hao si wamiliki hebu waseme wamiliki ni akina nani basi!!!
Mkuu 'Freyzem', ni hivi: Ni kazi bure mimi na wewe kubaki humu tukizungushana kuhusu "kujuwa au kutojuwa" mambo mengi yanayo fanyika huko serikalini; ambayo ina lazimu kuwa siri kila jambo.

Ni wajibu wa serikali yoyote ile yenye kuwatumikia wananchi wake kufanya mambo ya wananchi kwa uwazi na kuaminika. Serikali inapo anza kufanya kila kitu kiwe siri, huo ndio mwanzo wa serikali hiyo kutoaminiwa na wananchi wake.
Hakuna sababu ya kufanya maswala ya wananchi kiujanja ujanja, ulaghai, na uongo mwingi. Hakuna. Matokeo yake ndiyo haya, ya kila jambo kuhojiwa.
Serikali ina wajibika kwa wananchi, na uwazi katika utendaji wake ndio unao fanya wananchi wasiwe na sababu ya kuhoji maamuzi mengi yanayo fanywa kwa niaba yao.
Serikali ya Samia inafanya kinyume kabisa na hayo yote. Inataka wananchi ndio wawajibishwe kwa matendo yake yenyewe. Hiyo siyo serikali inayo watumikia wananchi. Na yote haya yanaanzia ndani ya chama CCM. CCM imekuwa ni balaa kwa Tanzania.
 
Imenilazimu nirudi nyuma kutazama uliko anzia hadi hapa ulipo fikia sasa.
Kuna sehemu unazungumzia "wapangaji, mafundi" kumjua mmiliki. Hii ni wazi inaonyesha hujui kitu kuhusu maswala ya umiliki wa majengo.

Unacho elewa wewe ni kuwa, polisi wakisha sema kitu, basi wamemaliza kwa vile wao ni watu wanao sema kweli tupu wakati wote. Sasa mtu wa aina hiyo tutamfanya nini kumbadili mawazo potofu!

Inawezekana sana ukawa ni mmoja wa hao wapindisha ukweli huko ndani ya CCM na serikalini. Kazi kubwa kwenu ni kupindisha tu na kufanya madudu kila mahali.
Serikali ya Samia imejipambanua kuwa ni serikali yenye kufanya maswala ya waTanzania gizani, kuficha ukweli, kila mahali. Na hii ni kwa sababu za ufisadi mwingi unao fanyika humo humo serikalini.
Sasa utakuja hapa unilazimishe nikupe ushahidi; wakati unajuwa mambo yenu ni ya gizani!
Acha ujuha wewe! Tatizo akili yako ni ndogo ndio maaana umeshindwa kuelewa nilichoandika!!
Karudie tena nilichoandika ujitahidi kukielewa!!! Period
 
Acha ujuha wewe! Tatizo akili yako ni ndogo ndio maaana umeshindwa kuelewa nilichoandika!!
Karudie tena nilichoandika ujitahidi kukielewa!!! Period
Mimi nina akili ndogo, kwa mjibu wako, ambaye ni chizi. Ni nani aliye na nafuu hapo!
 
Back
Top Bottom