Tila-lila2
JF-Expert Member
- Oct 20, 2019
- 652
- 1,058
Nimempenda sana Membe. Ukweli nakipenda sana Chama changu cha Mapinduzi yaani CCM. Lakini pia sioni ubaya wa upinzani na zaidi Membe kanibadilisha. Nilikuwa nikimpalilia mno Tundu Lissu lakini kwa sasa ni Benard Membe na Tundu Lisu ndiyo wanashindania kura yangu. Ninajua sana kuwa ni kura moja tu lakini najua ina maana kubwa kwenye Uchaguzi
Ubashiri wangu - mlolongo wa wagombea wa CCM ni lazima utawafikisha kwenye ugomvi na kuna wengine watahama. Ninaomba Act Wazalendo msikatae kuwachukua watakaokosa nafasi CCM wakiamua kuja kwenu. Wapeni nafasi. Hata kama ni mwehu au mwizi akija kwenu ilimradi ana uhakika wa kuongezea kura zenu pls msikatae. Kubalini pls pls. Ninavyoona mwelekeo tayari Act Wazalendo na CHADEMA mnaweza kufikisha idadi ya wabunge kwa asilimia 35 mpaka 50 hivi.
Ukishapata idadi hii ya wabunge basi ujue demokrasia katika nchi hii itakuwa imekuwa kubwa sanaaaaa. Ikitokea hivi kwa kweli Benard Membe atakuwa kailetea sana nchi sifa kuwa kuna demokrasia na yeye atakuwa ni bingwa wa demokrasia. Bila BM kwa kweli upinzani ulikuwa bado unasua sua kwani Tundu Lissu na wengine wanaojulikana ni wapinzani wanajulikana tu kuwa ni wapinzani original na wasingebadili sana matokeo. Ujio wa Bernard Membe kambi ya upinzani una maana kubwa sana sana. Nimekupenda bure Membe!
Kinachotakiwa kufanyika ni kufanya mashambulizi makali sana dhidi ya CCM ambao tayri tamaa yao ya madaraka inaonekana wazi. Mtu alikuwa Mkuu wa Mkoa anataka na ubunge - Puuuuuu! Kule Kigamboni mbona Faustine Ndugulile alikuwa bado anafaa tu sana. Namshauri Ndugulile iwapo CCM wanakukata Kigamboni pls usisite kwenda upinzani. Wewe ni mzuri sana. JIAMINI na Makonda hatakushinda kamwe.
Tena mbaya zaidi kesi dhidi ya Makonda kuhusu vyeti vyake sasa itaiubuka wakati huu itakapotokea kapewa ushindi wa ubunge. Akumbuke kesi ya Kihiyo - linakuja hilo mwaka huu. Makonda anaenda kujiexpose vibaya sana na tena ninafurahia sana nilivyoona kachukua Fomu. Wanasheria wanamsubiria kwa hamu.
Hivyo vivyo hata majimbo mengine wanayoenda kuchukua waliokuwa vigogo wa Serikali kama akina Kabudi, Kitila Mkumbo, Dkt Mpango, Ndalichako, Tulia n.k kuna uwezekano mkubwa sana yatapotelea kwa wapinzani. Kwangu mimi MCCM ninayependa ushindani wa kidemokrasia ambao unaleta maendeleo itakuwa furaha sana sana. Hapo Serikali itakumbuka kupandisha mishahara, kujali uhai wa binadamu, uhuru wa kujieleza na kuacha kuongoza kwa ubabe.
HIMA HIMA WAPINZANI - tupunguzieni makali ya Baba MEKO huyu! Laaahh tumechoka dakeki!