Kwanza kwa maelezo yako sidhani kama unaijua hiyo gari. Hiyo tunaiita kwa lugha za mtaani Tandam yani ni double diff nyuma na ndio fuso yenye uwezo wa tani 18. Na hakuna fuso ya tani kumi bila modification . Japo hoja yako ya msingi inaeleweka. Kama unamruhusu dereva kwenda anapotaka ila atoe tu taarifa akupe either milion mbili na nusu au tatu kwa mwez kulingana na uimara wa gari. Niliwahi kukodi ya mtu nilikuwa nalipa laki sita kwa week ila ilikuwa single mzigo hauzidi tani kumi tena uwe umepanga vizur.