Hesabu ya Fuso Ton 10

Hesabu ya Fuso Ton 10

iMind

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2011
Posts
3,039
Reaction score
4,889
Fuso ina ton 10 lakini kutokana na manuva iliyofanyiwa inaweza kubeba hadi ton 18. Nataka nimkabidhi dereva awe ananipa hesabu ya mwezi. Matengenezo na service ndogo ndogo ni juu yake. Je nimwambia anipe shs ngapi kwa mwezi? Maximin na minimum. Kwa anayejua tafadhali
 
Tsh 5,000/= Kutoka Ktk Hesabu Ya Siku Ya Tsh 200,000/= Ambapo Tsh 80,000/= Ni Ya Mafuta Siku Nzima, Tsh 25,000/= Ushuru Wa TANROADS, Tsh 50,000/= Ya Matrafiki Njia Panda Zote Utakazokatisha, Tsh 20,000/= Za Madereva Na Utingo Wake KUHONGA Mademu Huko Kote Wapitapo, Tsh 20,000/= Za Kununua Chakula, Maji Na Fegi Kutwa Nzima Kwa Hao Madereva na Utingo Wake Na Tsh 5,000/= Ndiyo Wanakuletea Wewe Bosi Wao Nyumbani Kama Faida Yako Ya Siku. Nakutakia Biashara Njema Mkuu.
 
Hakuna dereva mzuri gari lako litakaa juu ya mawe yeye anunuwa canter ya kuanzia maisha
 
Kwanza kwa maelezo yako sidhani kama unaijua hiyo gari. Hiyo tunaiita kwa lugha za mtaani Tandam yani ni double diff nyuma na ndio fuso yenye uwezo wa tani 18. Na hakuna fuso ya tani kumi bila modification . Japo hoja yako ya msingi inaeleweka. Kama unamruhusu dereva kwenda anapotaka ila atoe tu taarifa akupe either milion mbili na nusu au tatu kwa mwez kulingana na uimara wa gari. Niliwahi kukodi ya mtu nilikuwa nalipa laki sita kwa week ila ilikuwa single mzigo hauzidi tani kumi tena uwe umepanga vizur.
 
Asante kwa maelezo ya kina.
 
mmmmmh yani gari bila usimamizi wa wako utakuwa umeingiliwa coz usidhani dereva atafanya service ipasavyo
 
Back
Top Bottom