Hesabu Za LUKU Zinapigwaje

Hesabu Za LUKU Zinapigwaje

Umeme kabla ya kodi 292.83@1 unit pia baada ya kodi 356.35@1 unit kwa matumizi ya kati/kawaida yaani Tariff 1 T1
 
Habari Wadau! Hapo chini ni kipande cha maelezo ya umeme nilionunua kwenye simu.

Nimejaribu kupiga hesabu hizo asilimia hapo chini za VAT, REA na EWURA zote zinaonekana zimepigiwa hesabu kutoka kwenye shilingi 4098. Kwa gharama ya shilingi 5000, unaweza ona karibu shilingi 902 haipo hapo.

Sasa naomba mwenye kuelewa hizi hesabu zinapigwa vipi anisaidie. Yaani mchakato mzima hapo. Ahsante.

14.0KWH

0592 7638 3409 4517 9226

Cost 4,098.37
VAT 18% 737.70
EWURA 1% 40.98
REA 3% 122.95

TOTAL 5,000.00

Updates:

737.70% +40.98% +122.95% =Tsh. 901.63.
Tsh901.63+ Tsh4098.37 =Tsh.5,000/=

hivyo umeme wako UNIT 14 umetoka kwenye Tsh.4098.37. jumla ya makato yako ya ewura,REA na VAT ni Tsh 901.63.
 
Katika mfumo wa LUKU, hesabu zinafanyika kinyume. Wanaanza na jumla (TZS 5,000) na kisha kuhesabu kodi kana kwamba zimetokana na bei halisi ya umeme. Hii ndiyo sababu unaona tofauti kidogo kwenye hesabu.
Ni kweli. Nimeweka updates kwenye Uzi. Post namba 1 kabisa pale juu.
 
Wamemaanisha gharama ya unit 14 nje na kodi ni 4098.37.

Na 901.63 ndio jumla ya kodi zote.

Gharama ya unit 1 bila kodi inakuwa 292.7
 
Habari Wadau! Hapo chini ni kipande cha maelezo ya umeme nilionunua kwenye simu.

Nimejaribu kupiga hesabu hizo asilimia hapo chini za VAT, REA na EWURA zote zinaonekana zimepigiwa hesabu kutoka kwenye shilingi 4098. Kwa gharama ya shilingi 5000, unaweza ona karibu shilingi 902 haipo hapo.

Sasa naomba mwenye kuelewa hizi hesabu zinapigwa vipi anisaidie. Yaani mchakato mzima hapo. Ahsante.

14.0KWH

0592 7638 3409 4517 9226

Cost 4,098.37
VAT 18% 737.70
EWURA 1% 40.98
REA 3% 122.95

TOTAL 5,000.00

Updates:
Mgawanyo wa Gharama
Kwa kawaida, katika ununuzi wa umeme (Luku), kuna gharama za msingi inayojumuisha,
- Gharama halisi ya umeme
- VAT (Kodi ya Ongezeko la Thamani) - asilimia 18%
- EWURA levy - asilimia 1%
- REA (Rural Energy Agency) levy - asilimia 3%

Ukokotoaji
Umenunua luku ya shilingi 5,000.00, lakini gharama ya umeme pekee ni 4,098.37.
Gharama hii imechanganywa na asilimia za tozo na kodi zifuatazo.
- VAT (18%) ya 4,098.37
- 4,098.37 x 0.18 = 737.70

- EWURA levy (1%) ya 4,098.37
- 4,098.37 x 0.01 = 40.98

- REA levy (3%) ya 4,098.37
- 4,098.37 x 0.03 = 122.95

Ukijumlisha gharama zote pamoja, unapata jumla ya gharama za umeme na tozo zake, ambazo zinafikia 5,000.00.
4,098.37 + 737.70 + 40.98 + 122.95 = 5,000.00

Sehemu ya shilingi 902 ambayo unasema 'haipo' ni jumla ya VAT, EWURA levy, na REA levy.
737.70 + 40.98 + 122.95 = 901.63

Kwa hiyo, kiasi hiki kinaelekea kwenye kodi na tozo mbali na gharama halisi ya ununuzi wa umeme (yaani, 4,098.37).

Kwa Ujumla:
  • 4098.37 - Gharama ya halisi ya umeme
  • 737.70 - Kodi ya VAT (18%)
  • 40.98 - EWURA levy (1%)
  • 122.95 - REA levy (3%)
Matokeo yote haya yanapofikia, ndiyo yanayojumuisha jumla ya 5,000.00 uliyonunua.

Ova
 
Mfano wa kawaida:

Bei ya soda: TZS 1,000
VAT (18%): TZS 180 (18/100 x 1,000)
Jumla ya kulipia: TZS 1,180 (1,000 + 180)

Tunaanza na bei ya soda, tunahesabu VAT, na kisha tunapata jumla kwa kuongeza VAT kwenye bei ya soda.

Mfumo wa LUKU:

Fikiria unataka kununua LUKU ya TZS 5,000. Badala ya kuanza na bei ya umeme halisi, mfumo wa LUKU unafanya hivi:

Wanaanza na jumla: TZS 5,000 (hii ndiyo kiasi unachotaka kulipia)

Wanahesabu kodi "kinyume": Wanatumia asilimia za kodi (VAT 18%, EWURA 1%, REA 3%) kuhesabu ni kiasi gani cha kodi kinachopaswa kuwemo ndani ya hiyo TZS 5,000.

Wanapata bei halisi ya umeme: Kwa kutoa jumla ya kodi kutoka kwenye TZS 5,000, wanapata bei halisi ya umeme uliyonunua.

Kwa nini wanafanya hivi?
Kuna sababu kadhaa zinazowezekana:

Wanarahisisha hesabu na kuhakikisha kwamba mteja analipa kiasi sahihi (TZS 5,000) kwa umeme pamoja na kodi.

Mfumo wa LUKU umeundwa kuuza umeme kwa njia ya vocha zenye thamani maalum (mfano TZS 5,000, TZS 10,000, nk). Kwa hiyo, wanalazimika kuanza na jumla ya vocha na kisha kuhesabu kodi "kinyume".

Kama Kuna mwenye maoni tofauti na yangu ruksa kuuliza maswali
Hapo kwenye soda mkuu hauko sahihi:

Mwenye duka atakuuzia soda kwa Tsh. 1,000/=. Kwenye hiyo elfu 1 utakayotoa asilimia 18 (18%) inakatwa kama kodi ambayo ni:
18%x1,000=180. Kwa hiyo Tsh. 180/= ni kodi.

Kinachobaki ni Tsh. 820/= (1,000-180) ndicho kiasi anachopata mwenye duka kama hela yake.

Kwa hiyo jumla ni 820+180=1,000/=

Ni hesabu tu mkuu!
 
Hoja ikiwekwa mezani inatakiwa ipanguliwe kwa hoja, wewe unaleta mambo mengine kabisa! Kwani iyo hela aliyonunulia umeme ulimpa wewe?

Halafu hela inaanzia shilingi ngapi? hivi hujiulizi iyo 901.63 ambayo haionekani hapo mleta mada anataka ufafanuzi ilikoenda wewe unaona ni upuuzi, vipi wakinunua umeme wa elfu tano watu laki moja ukizidisha 901.63 × 100,000 = 90,163,000 bado sio hela?
Mkuu unasumbuka na watu wajinga humu. nimewahi kuuliza swali kama hilo kwenye vocha voda ikibaki hata 40
au 25 ukipigia mtu unaambiwa huna salio je hii 40 ni nini? nikaambiwa tafuta hela dogo anae kuambia hata ukimuomba kazi akuajiri kwenye kampuni yake hana kila kitu anaishi magetoni kama panya.

piga hesabu voda inatumiwa na watu wangapi tz nzima? ebu fanya kwa watu kama m10 tukwa siku
kwa harka tu kuna pesa ya bure m4 hapa daily zidisha kwa mwezi then mwaka? Safari bado mkuu
 
Hapo kwenye soda mkuu hauko sahihi:

Mwenye duka atakuuzia soda kwa Tsh. 1,000/=. Kwenye hiyo elfu 1 utakayotoa asilimia 18 (18%) inakatwa kama kodi ambayo ni:
18%x1,000=180. Kwa hiyo Tsh. 180/= ni kodi.

Kinachobaki ni Tsh. 820/= (1,000-180) ndicho kiasi anachopata mwenye duka kama hela yake.

Kwa hiyo jumla ni 820+180=1,000/=

Ni hesabu tu mkuu!
Nimechanganya kidogo mkuu kuhusu jinsi VAT inavyohesabiwa kwenye bidhaa.

Kama ulivyosema, mwenye duka anauza soda kwa TZS 1,000 ambayo tayari inajumuisha VAT. Kwa hiyo, ili kupata bei halisi ya soda na kiasi cha VAT, hesabu inapaswa kuwa hivi:

Jumla ya bei (ikiwa ni pamoja na VAT): TZS 1,000
Asilimia ya VAT: 18%
Ili kupata kiasi cha VAT, tunatumia formula ifuatayo:

Kiasi cha VAT = (Jumla ya bei X Asilimia ya VAT) / (100 + Asilimia ya VAT)

Kwa hiyo, katika mfano wetu:
Kiasi cha VAT = (1000 * 18) / (100 + 18) = 18000 / 118 = 152.54

Kiasi cha VAT ni TZS 152.54

Ili kupata bei halisi ya soda (bila VAT),

tunatoa kiasi cha VAT kutoka kwenye jumla ya bei:
Bei halisi ya soda = Jumla ya bei - Kiasi cha VAT

Bei halisi ya soda = 1000 - 152.54 = 847.46

Kwa hiyo, bei ya soda ni TZS 847.46 na kiasi cha VAT ni TZS 152.54.

Ahsante kwa kunisahihisha mkuu
 
Ndiyo mkuu, sahihi kabisa
 
shida sio kujumlisha shida ni kwamba kodi ambayo ni 18.0326%,
Mteja kanunua umeme wa 5000
18.0326% of 5000 = 901.63

Hela ilionunua umeme ni 4098.37
[(18% of 4098.37)+(1% of 4098.37)+(3% of 4098.37)] = 901.6414

Hiyo 901.63 kwa nini ilingane?? wakati hizo ni sehemu za hela tofauti au ni coincidence!
ISIJEKUWA IMELINGANISHWA ILI WATU WAKATWE KODI MARA MBILI
Lazima ilingane kwa sababu kilichofanyika ni kuigawa hicho hicho kiasi cha Tsh. 901.63/= (ambayo ndiyo kodi ya jumla) kati ya VAT, EWURA na REA kwa asilimia (%) kama ilivyoainishwa.

Asilimia hizo (za VAT, EWURA, REA) utazipata kwa kutumia gharama ya kununulia umeme, ambayo ni 4,098.37/= ambazo lazima jumla yake ikuletee Tsh. 901.63/=

Kwa hiyo kwa ujumla ina maana kila unaponunua umeme wa kiasi chochote cha pesa ujue asilimia 18.0326 (18.0326%) ya kiasi hicho cha pesa hukatwa kama kodi na kiasi kinachobaki ndicho huhesabika kama gharama ya kununulia umeme.
 
Na mimi nilikuwa naona kama wewe ila kuelewa hapo ni mpaka ufikirie na upandewa pili wa shilingi.
 
Hapo kwenye soda mkuu hauko sahihi:

Mwenye duka atakuuzia soda kwa Tsh. 1,000/=. Kwenye hiyo elfu 1 utakayotoa asilimia 18 (18%) inakatwa kama kodi ambayo ni:
18%x1,000=180. Kwa hiyo Tsh. 180/= ni kodi.

Kinachobaki ni Tsh. 820/= (1,000-180) ndicho kiasi anachopata mwenye duka kama hela yake.

Kwa hiyo jumla ni 820+180=1,000/=

Ni hesabu tu mkuu!
Ni kweli Mkuu.
 
Kwani hizo VAT, EWURA na REA si ndio Kodi zenyewe hizo, au!? Mimi nataka nielewe TU hizo hesabu niwe na Amani. Isije ikawa Yale mambo ya kuiba mia mia kwa Kila akaunti., unakuta watu wanakula mabilioni kwa ujinga wetu.
Kuna kitu kinaitwa Hidden Tax, niliwahi kusikia nadhani ndio imeanza kuwa implemented
 
Habari Wadau! Hapo chini ni kipande cha maelezo ya umeme nilionunua kwenye simu.

Nimejaribu kupiga hesabu hizo asilimia hapo chini za VAT, REA na EWURA zote zinaonekana zimepigiwa hesabu kutoka kwenye shilingi 4098. Kwa gharama ya shilingi 5000, unaweza ona karibu shilingi 902 haipo hapo.

Sasa naomba mwenye kuelewa hizi hesabu zinapigwa vipi anisaidie. Yaani mchakato mzima hapo. Ahsante.

14.0KWH

0592 7638 3409 4517 9226

Cost 4,098.37
VAT 18% 737.70
EWURA 1% 40.98
REA 3% 122.95

TOTAL 5,000.00

Updates:
Mbona makato yote yameoneshwa wazi na umeme uliopewa ndiyo huo wa 4098.37!
 
wewe ndo huelewi kumbe, iko ivi ukinunua vocha ya 5000 kodi(%) itakatwa kwenye hiyo elfu tano.

ila ukinunua umeme wa 5000 ni tofauti kodi inakatwa kwenye 4098.37 na hao wengine EWURA na REA asilimia zao watakata kwenye 4098.37 sasa swali la msingi 901.63 imeenda wapi maana jumpa ya malipo ni 5000.
Siyo kweli,hata kwenye umeme kodi inakatwa kwenye 5000 na wanaonesha makato yote na hela inayobaki ambayo ni 4098 ndiyo unapewa umeme,labda tulalamikie huo utitiri wa hiyo kodi na tozo za Rea na Ewura.
 
Hivi wewe unajua kutafuta asililia? tafuta asilimia ya hela ya VAT, EWURA na REA uone zinakatwa kwenye 5000 au 4098.37

Hivi unadhani 1% EWURA 40.98 wamekata kwenye 5000?
hili nalo ni suala la kujadili!

1% of 4098.37 = 40.98
1% of 5000 = 50.00

Kufikia hapo nadhani ushajua VAT, EWURA na REA asilimia zao wanakata kwenye 4098.37
 
5000-4098.37=...?

Usilete hesabu za makadirio hapa
 
Back
Top Bottom