Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
da mbona kiasi ni kidogo sana kiongozi!
Wakuu hii niliuliza week mbili zilizopita. Mimi nataka kufuata mwenyewe machine nchini UK. Jee mnadhani ushuru wake upoje? nataka tani 32 scania au DAF
Hivi na vile vigari vidogo Suzuki Carry hesabu yake kwa siku ni Tshs ngapi!?
najua kuna faini ya kupitisha vifuzi, michanga na mawe bila kufunika ili kuzuia kuchafua barabraEeeh kumbuka, wewe ndio tajiri ukiamua gari yako ifanye kazi usiku na mchana utapata double ya hizo pesa.
NB: usiku na mchana ni kwa 32 Tones only.
Kunachoangusha ni wakala wa Barabara (tanroads) kila siku lazima waje na fine zao kama nilivyokueleza. Kwa hiyo michakato mingi inakuwa huku kwa huku tu.
Lakini si mbaya kwa Investment ya 120mil kukupa return ya 7.2mil a month. Kama ukibahatika kupata gari nzuri. In a year unaweza pata 86mil. Na hapo ni tu kama gari unafanya kazi day time. Kama itakuwa inakesha means unapata pesa twice japokuwa gari inachoka haraka.
I think hiyo investment ya 120m ndio inaua nguvu kwa scania , labda kama unaimport hilo tipper labda hiyo starting capital naona itakuwa chini kidogo , ila so far nimeipenda hii Biz
Inategemea na Maeneo ambayo gari itafanyia kazi.
Kwa Dar maeneo ya kazi ni Mbagala, Gongolamboto, kigamboni na Bunju.
Kwa Bunju ton 4 ni 60,000/70,000. Tone 16 ni 120,000/150,000 na Tone 32 ni 250,000 hadi 300,000.
Tone saba kwa huku zimepotea kabisa. Zimebaki Iveco Cargo chache ambazo zinashindwa kuhumili mikikimikiki ya kazi za mjini.
Usisahau kuna watu wa Tanroads wanapima mizani barabarani. Ukikamatwa fine zao minimum 2mil maxmum 6mil.
Ni Pm kwa zaidi.
nna shida ya kukodisha mende (8x4). kama unayo au unajua nnaweza kupata wapi, naomba uniambie. nagitaji mende 5 hadi 10. tayari nimeshapata moja.
Kaka jee unakodi kwa ngapi kwa siku? Nataka tuu kupata muongozo nione kama hii biashara ipo solid.
Thread imenivutia kuchangia ili kupanuana mawazo maana ukiangalia namba zinavutia lakini ukweli wa hii biashara nisingemshauri mtu ambae atalitegemea hilo lori limfanye ajikimu kwa maisha na aendelee kuwekeza.
Kufuatia uzoefu nilionao kuna changamoto nyingi sana kuliko hata mapato.
Kwanza lori huwa linatumia hela kila siku hata kama ni bovu kama huna parking lazima ulilipie usiku na mchana.
Kingine kwa sababu hufanya kazi kwenye mazingira magumu yaani hupita kusiko na barabara basi matengenezo ni mengi sana.
Kwenye matengenezo ndio kuna utata. Itabidi umuamini mtu akutafutie spea. Sasa ukifika huko Tabata ndio pasua kichwa. Wale watu hamna mkweli wengi ni mradi wapate hela yako.
Ukiipata hiyo spea amini hili mafundi wetu makanjanja, wote wababaishaji tu yaani hamna anayejua asilimia 100 nini anafanya. Akikufungia spea wakati mnatest inakata kingine halafu anasema kiurahisi tu aaah kulikuwa na hiki nilisahau ndio maana. Tafuta spea hii nitakufungia bure wee sikweli ni kazi ingine utamlipa tu. Kumbuka hapo unalipia daily na dereva na tingo wake wana familia nazo ziishi.
Biashara yenyewe nayo majanga. Kuanzia ukweli wa dereva, stika huyo kwenye machimbo, trafiki na hao madalali wanaojua tenda ziko wapi?
Kwa kifupi lori SI BIASHARA YA KUWEKEZA kwa mtu mwenye hela ya 120m kwani lori likileta 800,000 linachukua 8m matengenezo.
Nachangia ili mtu asitumbukie kwenye hizi changamoto ila kama una gereji yako LABDA utakuwa na afadhali.
Either that au uwe mtu wa kushinda kwenye ma gereji uswahilini na maduka ya wauza spea used ambazo hata huelewi unauziwa kitu gani. Huko Tabata kwanza gari yako ndogo uliyoenda nayo inaweza kubaki huko huko na yenyewe, kuna hii njia ya kuingilia Tabata kwenye ma spea kutokea Kigogo nilishanusurika kupinduka na SUV, it is so effed up utadhani unaenda maficho ya ISIS. And then mafundi wanadanganya initial estimates za matengenezo, au hajui undani wa tatizo mpaka akishafungua machuma ndio ndio anakwambia kuna hiki na kile na hiki na kile, inabidi u come up na hela ambayo hukuijua toka mwanzo. Kwa kweli biashara za kusimamia mafundi gereji hazina mpango aisee.... kwa hiyo watu wana resort kwenye kuamini watu, kama ulivyosema, which I don't believe in anymore, utafanyaje biashara kwa hesabu za kupewa facts and figures na mtu baki/mwajiriwa? Kuna dereva ashanambia gari imepasuka engine block njiani Mkata, how? The angels know. Na kwamba amefanya kila awezalo akisaidiana na madereva wenzake kuivuta gari kurudi karibu na mji bila ku incur costs za kupeleka spea/mafundi wa kushusha engine maporini huko au kulivuta at a fee, sasa hujui umshukuru ama umfukuze, sina muda kwa kweli wa kwenda Mkata kuhakikisha engine block limepasuka au amefanya change quarter. No way, not again na hizi biashara za kuaminiana.Itabidi umuamini mtu akutafutie spea. Sasa ukifika huko Tabata ndio pasua kichwa.