Hesabu za matipper ya Mchanga

Hesabu za matipper ya Mchanga

Hivi na vile vigari vidogo Suzuki Carry hesabu yake kwa siku ni Tshs ngapi!?
 
kuna thread humu wamesema 120,000-130,000 kwa wiki wanasema kwa Suzuki carry
 
Mkuu 1.3m sehemu yoyote Dar, hiyo bei inajumuisha manunuzi, vibali transport etc.
 
Wakuu hii niliuliza week mbili zilizopita. Mimi nataka kufuata mwenyewe machine nchini UK. Jee mnadhani ushuru wake upoje? nataka tani 32 scania au DAF

Hiyo DAF umepeleleza uwepo wa spare parts Bongo?
 
Eeeh kumbuka, wewe ndio tajiri ukiamua gari yako ifanye kazi usiku na mchana utapata double ya hizo pesa.

NB: usiku na mchana ni kwa 32 Tones only.

Kunachoangusha ni wakala wa Barabara (tanroads) kila siku lazima waje na fine zao kama nilivyokueleza. Kwa hiyo michakato mingi inakuwa huku kwa huku tu.

Lakini si mbaya kwa Investment ya 120mil kukupa return ya 7.2mil a month. Kama ukibahatika kupata gari nzuri. In a year unaweza pata 86mil. Na hapo ni tu kama gari unafanya kazi day time. Kama itakuwa inakesha means unapata pesa twice japokuwa gari inachoka haraka.
najua kuna faini ya kupitisha vifuzi, michanga na mawe bila kufunika ili kuzuia kuchafua barabra
lkn pia mizani huwa inalipiwa kama mzigo umezidi
kama gari haina kibali ndo mtihani ambapo wengi hufanya kazi usiku mfano kwa kibaha wengi hasa tani 32 na 16 hupiga mzigo usiku ili kukwepa hizi shuruba za tanzroads
 
I think hiyo investment ya 120m ndio inaua nguvu kwa scania , labda kama unaimport hilo tipper labda hiyo starting capital naona itakuwa chini kidogo , ila so far nimeipenda hii Biz
 
Bora niwe dalali kwenye hayo maroli yenu kuliko kufanya biashara hii
 
I think hiyo investment ya 120m ndio inaua nguvu kwa scania , labda kama unaimport hilo tipper labda hiyo starting capital naona itakuwa chini kidogo , ila so far nimeipenda hii Biz

Hii 120M labda kama unataka kulinunua Dar. Nusu ya hiyo bei unapata UK 32 tons scania 8X4 towel.
 
nna shida ya kukodisha mende (8x4). kama unayo au unajua nnaweza kupata wapi, naomba uniambie. nagitaji mende 5 hadi 10. tayari nimeshapata moja.
 
Inategemea na Maeneo ambayo gari itafanyia kazi.

Kwa Dar maeneo ya kazi ni Mbagala, Gongolamboto, kigamboni na Bunju.

Kwa Bunju ton 4 ni 60,000/70,000. Tone 16 ni 120,000/150,000 na Tone 32 ni 250,000 hadi 300,000.

Tone saba kwa huku zimepotea kabisa. Zimebaki Iveco Cargo chache ambazo zinashindwa kuhumili mikikimikiki ya kazi za mjini.

Usisahau kuna watu wa Tanroads wanapima mizani barabarani. Ukikamatwa fine zao minimum 2mil maxmum 6mil.

Ni Pm kwa zaidi.

Mkuu maelezo yako mazuri sn yana encourage tafadhali ningependa kujua km unifanya hii biashara, pia kama ndio kazi yako naomba nikutembelee kwa uwelewa zaidi please
 
nna shida ya kukodisha mende (8x4). kama unayo au unajua nnaweza kupata wapi, naomba uniambie. nagitaji mende 5 hadi 10. tayari nimeshapata moja.

Kaka jee unakodi kwa ngapi kwa siku? Nataka tuu kupata muongozo nione kama hii biashara ipo solid.
 
Kaka jee unakodi kwa ngapi kwa siku? Nataka tuu kupata muongozo nione kama hii biashara ipo solid.

nakodisha kwa trip laki mbili na nusu, kwa siku gari inaweza fanya trip mbili, mafuta na dereva juu yangu, hatakama gari haitafanya kazi dereva atapata allowance yake, kazi Itafanyikia Tanga.
 
Thread imenivutia kuchangia ili kupanuana mawazo maana ukiangalia namba zinavutia lakini ukweli wa hii biashara nisingemshauri mtu ambae atalitegemea hilo lori limfanye ajikimu kwa maisha na aendelee kuwekeza.
Kufuatia uzoefu nilionao kuna changamoto nyingi sana kuliko hata mapato.

Kwanza lori huwa linatumia hela kila siku hata kama ni bovu kama huna parking lazima ulilipie usiku na mchana.

Kingine kwa sababu hufanya kazi kwenye mazingira magumu yaani hupita kusiko na barabara basi matengenezo ni mengi sana.

Kwenye matengenezo ndio kuna utata. Itabidi umuamini mtu akutafutie spea. Sasa ukifika huko Tabata ndio pasua kichwa. Wale watu hamna mkweli wengi ni mradi wapate hela yako.

Ukiipata hiyo spea amini hili mafundi wetu makanjanja, wote wababaishaji tu yaani hamna anayejua asilimia 100 nini anafanya. Akikufungia spea wakati mnatest inakata kingine halafu anasema kiurahisi tu aaah kulikuwa na hiki nilisahau ndio maana. Tafuta spea hii nitakufungia bure wee sikweli ni kazi ingine utamlipa tu. Kumbuka hapo unalipia daily na dereva na tingo wake wana familia nazo ziishi.

Biashara yenyewe nayo majanga. Kuanzia ukweli wa dereva, stika huyo kwenye machimbo, trafiki na hao madalali wanaojua tenda ziko wapi?

Kwa kifupi lori SI BIASHARA YA KUWEKEZA kwa mtu mwenye hela ya 120m kwani lori likileta 800,000 linachukua 8m matengenezo.

Nachangia ili mtu asitumbukie kwenye hizi changamoto ila kama una gereji yako LABDA utakuwa na afadhali.
 
Changamoto zipo kwenye magari yote. Ninalo liona mimi ni kwamba wengi wanaingia kwenye biashara ya magari bila kujua. Kwanza sishauri hata siku moja kununua lori kutoka kwa Mtu ambae ameshatumia NDANI YA TANZANIA. Kama umetezama kwa ukaribu sana kwa Mazingira ya Tanzania lazima lori uliendeshe kwa miaka 2 kisha uliuze sababu repair and maintenance cost itakuhamisha mji.

Kama hili gari linakupa 250,000 kwa trip na likakupa 4 trip on average kwa siku. Na kama gross margin yako ni 40% basi kama unaendesha siku 6 kwa week, basi kwa mwezi unaweza kuleta 9.6M. Na kama upo makini ina maana gross Margin a year ni karibu na Million 100. Hili lori umelinunua Uingereza, nashauri ukanunue mwenyewe. Anataka kuagiza ani inbox nakuletea bila hata kukucharge shillingi moja, unanilipia nauli ya ndege nalifuata mwenyewe UK. Bei ya Scania ya 2005 ni kama 25,000 USD mpaka ifike Dar na custom na kila kitu gharama itakuwa 36,000 USD sawa na 64Million.

Kama kwa mwaka Gross Margin ni 100M, ina maana ndani ya miezi kumi ume break-even baada ya kutoa direct related cost. Sasa uki run kwa mwaka mmoja zaidi unakuwa umekusanya return yako kwenye asset, na baada ya mwaka wa pili unauza at fair value ambayo piga uwa haiwezi kuwa chini ya 20% below bei uliyonunulia.

Tatizo kubwa nilionala mimi watu wanashindwa kuelewa kuna tofauti kubwa sana kati ya MSHAHARA NA MAUZO, revenue na salary ni vitu viwili tofauti. Sasa kama wewe unatengeneza 400,000 kwa siku alafu unasimama bar unakula 50,000 ujue umetafuna revenue ambayo mazala yake ni 10 times ya pesa uliyokula. Kabla ujadumbukia kwenye biashara tafadhali jifunze heshima ya pesa.
 
Itabidi umuamini mtu akutafutie spea. Sasa ukifika huko Tabata ndio pasua kichwa.
Either that au uwe mtu wa kushinda kwenye ma gereji uswahilini na maduka ya wauza spea used ambazo hata huelewi unauziwa kitu gani. Huko Tabata kwanza gari yako ndogo uliyoenda nayo inaweza kubaki huko huko na yenyewe, kuna hii njia ya kuingilia Tabata kwenye ma spea kutokea Kigogo nilishanusurika kupinduka na SUV, it is so effed up utadhani unaenda maficho ya ISIS. And then mafundi wanadanganya initial estimates za matengenezo, au hajui undani wa tatizo mpaka akishafungua machuma ndio ndio anakwambia kuna hiki na kile na hiki na kile, inabidi u come up na hela ambayo hukuijua toka mwanzo. Kwa kweli biashara za kusimamia mafundi gereji hazina mpango aisee.... kwa hiyo watu wana resort kwenye kuamini watu, kama ulivyosema, which I don't believe in anymore, utafanyaje biashara kwa hesabu za kupewa facts and figures na mtu baki/mwajiriwa? Kuna dereva ashanambia gari imepasuka engine block njiani Mkata, how? The angels know. Na kwamba amefanya kila awezalo akisaidiana na madereva wenzake kuivuta gari kurudi karibu na mji bila ku incur costs za kupeleka spea/mafundi wa kushusha engine maporini huko au kulivuta at a fee, sasa hujui umshukuru ama umfukuze, sina muda kwa kweli wa kwenda Mkata kuhakikisha engine block limepasuka au amefanya change quarter. No way, not again na hizi biashara za kuaminiana.
 
Nashukuru wadau kwa kuweka changamoto wazi , mkuu hamna kitu kirahisi kwenye biashara , gari ni chombo kinachopungua value kila siku, kila mwaka. Pia hata kama unapata laki 8kwa siku kama alivyosema mdau lazima ujue haya ni mauzo sio hela unayochukua lazima uweke pembeni hela ya matengenezo , changamoto ni kupata garage , Fundi na Dereva ambao watafanikisha biashara , spare na gari unaweza agiza mwenyewe nje , kama ni kweli mpaka linafika kwa 60-70 aisee sio mbaya kwa hiyo return
 
Back
Top Bottom