Heshima vs Upendo katika ndoa

Heshima vs Upendo katika ndoa

Sokulu Mkombe

Senior Member
Joined
Oct 31, 2018
Posts
126
Reaction score
167
Habari wakuu, Heshima yenu popote mlipo

Naanza kwa kunukuu

Wakolosai 3:18-19​

"Enyi wake, watiini waume zenu, kwani ndivyo apendavyo Bwana. Nanyi waume, wapendeni wake zenu, na msiwe wakali kwao".

Huwa najiuliza kwa nini Mungu alimuaguza mwanaume kumpenda mkewe huku mke akiagizwa kumheshimu mumewe.

Swali langu niJe?

1. Mwanamke hujifunza kupenda? ( i.e Upendo kwa Mwanamke ni Aquired character? ) au kwa mwanamke upendo upo ndani ya heshima kwa mumuwe? Maana utasikia wanawake wanasema " Kikubwa akupe huduma kumpenda utajifunza"

2. Mwanaume Hana chembe ya upendo ndani yake ndio maana Mungu anamuagiza Kumpenda mkewe? Maana makatazo ya Mungu Hutuepusha na Mengi kama yakifuatwa.

Msaada wenu wakuu kwa wenye uzoefu katika hili

Natanguliza shukrani.
 
Ke ana upendo wa dhati kuliko Me kwa asili ya Binadamu tulivyoumbwa na Me huwa anatamani.

Ke kinachomponza kuonekana hana upendo kwa Me ni udhaifu wake wa kuamini uwongo sana kuliko ukweli, husababisha kuwa kigeugeu na kukosa msimamo kimaamuzi wakati wowote.
 
Asante mkuu
 
Mi naona kama Mungu aligawa majukumu haki bin sawa kila mmoja afanye lile aliloagizwa na Mungu mwanamke kazi yake ni kuheshimu na mwanaume kazi yake ni kupenda ila sasa hvi watu wamevamia kazi zisizowahusu basi imekua ni tafrani
 
Kwanza nivizuri utambua nature ya jinsia hiz mbili. Mwanaume kaumbwa na hali ya kumiliki power & authorities, while mwanamke waongozwa na hisia zaidi.

Kwanini mwanaume ndio anatakiwa ampende mke wake? Jibu ni kuwa kwa sababu mwanamke anaongozwa na hisia bas anaitaji matendo ya kihisia zaid ili kumliki na kumfanya ajihisi yupo sehemu salama na kwa mwanaume pia anaitaji matendo ya heshima zaid ili kumfanya ajihisi bado ana possess power & authorities ndan ya imaya yake.
 
asant sana mkuu nimejifunza kitu
 
Back
Top Bottom