HESLB itaanza kutoa hela baada ya sikukuu ya EID EL FITR

Poleni sana wadogo zangu mungu ameskia kilio chenu na kwa habari zisizo rasmi ni kuwa ile 60% imeshapatikana kwani mwanzo ilikuwapo 40% ,so mjiandae kupokea haki yenu ila angalizo muwe na nidhamu ya matumiz ya hzo pesa kuanzia mtakapozipata
 
Kati ya kizazi cha wanafunzi wa vyuo vikuu waoga hiki Ni cha kwanza. Na bado eti mna watu wanajipitisha kwenu wanataka kuwa viongozi wa serikali za wanafunzi mnawapigia kura!!! Ngoja mkome na uoga wenu na UCCM wenu. Kiongozi anapanda ndege kwenda KOREA alhali waajiri wake hawana hela, yeye anakula POSHO ya DARUSO na serikali kwenye mkutano wa viongozi wa Vyuo duniani?

Hapo Chuoni (mlimani) kuna mtu anaitwa Bush aka Buhenyenge Steven ofisi ya Afisa mikopo ilianzishwa Kwa ajili yake maana alikuwa Ni Waziri wa mikopo Enzi hizo na kauli mbiu yake ilikuwa kama hela hazitoki nalala na kufia HESLB. Leo hii anawasaidiaje wanafunzi?

acheni UOGA nyie watoto, HESLB watawachezea mpaka mkome. Na assessment lazima mkutwe vituoni hakuna excuse eti sina hela.
 
Mkuu

unajitahidi kuchochea lakini unashindwa kufanikiwa. Kwanza Bush sio
afisa mikopo pale Udsm kwa miaka zaidi ya minne sasa, siku hizi yupo
Silva na Silva anafanya kazi nzuri sana ila kwa round hii pesa haijafika
chuo, sasa unataka Silva aandamane?

Pia si kwamba bodi wanawachezesha kwato wanafunzi, bali bodi nayo
haijapokea hizo fedha,

Pili rais wa DARUSO kwenda nje ya nchi huwa hatumii pesa wala posho za
DARUSO. Sasa kama rais anapata ufadhili wa nje hilo lisikusumbue cha
msingi akiwakilishe chuo vizuri.

Mwisho, CCM ndio chama tawala, na kinafanya kazi yake vizuri, ukienda pale Udsm viongozi wazuri wa daruso wana asili ya CCM, wanaharakati wazuri wana asili ya CCM, kama hulijui hilo wewe hujasoma UDSM. Kaa kimya.

 
Hata mie kura yangu haipo mpaka watakapojifunza kutekeleza majukumu yao kwa wakati pasipokuwahumiza watu wa tabaka flani!
 

People Like You Are the Reason Why We Have
Middle Fingers ...
 

Eid imeisha mbona bado.....
 
kuna jamaa kaniambia hizo pesa mpaka mwezi 10 hizi habari zina ukweli wowote?
 
Sina haja ya kubishana kama nimesoma UDSM ama la! Haina tija. La msingi tu Ni kuwa nilichokiandika si uchochezi na Ni kikubwa kinakuzidi umri. Kwa taarifa yako Bodi ya mikopo iliwahi kusema haina hela na tuliposhinikiza Enzi za uongozi wa Nimrod Mkono tulipewa pesa kesho yake.

Kwa nature ya Fikra kama zako za kukaa kimya ndiyo Sababu mambo ya msingi hayaendi Hata maofisini lakini POSHO za vikao hazikosi. Fanya kukaa chini na kutathmini maandiko yangu. Nikionacho yaweza kuwa u miongoni mwa viongozi wa serikali ya DARUSO mfu. Mnastahili kuhukumiwa na wanafunzi Kwa kukaa kimya wakati hawana pesa na mkuu wako kwenda KOREA wakati wananchi wake hajui Hatma Yao. Ni sawa na baba kualikwa harusini ukaenda kula ukashiba alhali nyumbani wanao hawana uhakika wa kula. Si kila mkutano huwa wanaenda wote, la hasha. Mnaendekeza tabia za ki VASCO DA GAMA tu.

Kwa kuwa HESLB wameona hakuna uongozi thabiti wameamua kuwapa fedha wanafunzi Kwa mafungu na kujisikia katika schools, faculties na departments tofauti ili kuua spirit ya solidarity ambayo wewe inaonekana si mnufaika wake na hauko tayari Kuiacha kauli mbiu hii ya DARUSO Kwa kizazi Kijacho. Poor poor Poor and incompetent DARUSO leadership. Hebu mtafuteni Hata Mtatiro atakusaidieni nini mfanye maana inaonekana umekuja kumtetea boss wako na kuonesha ulivyo mgeni na mweupe wa mikakati ya solidarity hapo DARUSO. Usije ukasimama level square na maneno yako haya, watakuua kama wewe Ni mwanafunzi ama Kiongozi wa serikali ya wanafunzi.

Mwambie boss wako ama Kiongozi wako unayemtetea Kwa kutokujali maisha ya wapiga kura wake chuki dhidi yake miongoni mwa wanafunzi Ni kubwa mno Kwa sasa.
 
Mkuu mimi nilihitimu hapo mlimani 2012.

 
Mkuu mimi nilihitimu hapo mlimani 2012.
Ndiyo Sababu nimesema niliyoandika yanakuzidi umri. Aksante kwa kunifahamisha hili. Basi tambua wana UDSM wenzio pamoja na wengine wa vyuo vingine vikuu na vyuo vishiriki wanateseka Kwa kukosa fedha za mafunzo Kwa vitendo mpaka sasa tunavyoandika humu. Mhitimu wewe saidia kuelimisha jamii yako ione jinsi nchi ilivyopoteza Hata focus kwenye mambo ya msingi Kwa ustawi wa Taifa. Wataalam wa aina gani watazalishwa na mfumo wa elimu usiowawezesha kufanya mafunzo Kwa vitendo ama mazoezi ya kile wanachojifunza?
 

True


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…