HESLB itaanza kutoa hela baada ya sikukuu ya EID EL FITR

HESLB itaanza kutoa hela baada ya sikukuu ya EID EL FITR

Udsm mambo bwerere, main oyeee, hii inatia faraja kwa wengine ambao hamjapata. Mwaweza kupata ndani ya wiki hii
 
Kuna mtu amewahi kuuliwa pale Rev-square? Au ni namna mpya ya kuhamasisha wanafunzi wauane pale rev square?

Me nachojua rev square wanasimama watu wa fikra tofauti na kama usipokidhi haja ya wengi unazomewa na kushushwa.

Sina haja ya
kubishana kama nimesoma UDSM ama la! Haina tija. La msingi tu Ni kuwa
nilichokiandika si uchochezi na Ni kikubwa kinakuzidi umri. Kwa taarifa
yako Bodi ya mikopo iliwahi kusema haina hela na tuliposhinikiza Enzi za
uongozi wa Nimrod Mkono tulipewa pesa kesho yake.

Kwa nature ya Fikra kama zako za kukaa kimya ndiyo Sababu mambo ya
msingi hayaendi Hata maofisini lakini POSHO za vikao hazikosi. Fanya
kukaa chini na kutathmini maandiko yangu. Nikionacho yaweza kuwa u
miongoni mwa viongozi wa serikali ya DARUSO mfu. Mnastahili kuhukumiwa
na wanafunzi Kwa kukaa kimya wakati hawana pesa na mkuu wako kwenda
KOREA wakati wananchi wake hajui Hatma Yao. Ni sawa na baba kualikwa
harusini ukaenda kula ukashiba alhali nyumbani wanao hawana uhakika wa
kula. Si kila mkutano huwa wanaenda wote, la hasha. Mnaendekeza tabia za
ki VASCO DA GAMA tu.

Kwa kuwa HESLB wameona hakuna uongozi thabiti wameamua kuwapa fedha
wanafunzi Kwa mafungu na kujisikia katika schools, faculties na
departments tofauti ili kuua spirit ya solidarity ambayo wewe inaonekana
si mnufaika wake na hauko tayari Kuiacha kauli mbiu hii ya DARUSO Kwa
kizazi Kijacho. Poor poor Poor and incompetent DARUSO leadership. Hebu
mtafuteni Hata Mtatiro atakusaidieni nini mfanye maana inaonekana
umekuja kumtetea boss wako na kuonesha ulivyo mgeni na mweupe wa
mikakati ya solidarity hapo DARUSO. Usije ukasimama level square na
maneno yako haya, watakuua kama wewe Ni mwanafunzi ama Kiongozi wa
serikali ya wanafunzi.

Mwambie boss wako ama Kiongozi wako unayemtetea Kwa kutokujali maisha ya
wapiga kura wake chuki dhidi yake miongoni mwa wanafunzi Ni kubwa mno
Kwa sasa.
 
Kuna mtu amewahi kuuliwa pale Rev-square? Au ni namna mpya ya kuhamasisha wanafunzi wauane pale rev square?

Me nachojua rev square wanasimama watu wa fikra tofauti na kama usipokidhi haja ya wengi unazomewa na kushushwa.

Pale huwa hapana chezea, lazima ufuate matakwa ya wanafunzi ukiwa kinyume unaweza zonewa
 
Back
Top Bottom