Zekoddo
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 1,859
- 4,539
Hiki ndicho kinachotokea Vyuo tofautitofauti hapa nchini hususani Chuo Kikuu Cha Kilimo SOKOINE.
Ikumbuke kuwa Takribani wiki tatu zimepita tangu wanafunzi wamemaliza semista ya kwanza ndani ya mwaka wa masomo 2022/2023 na wanafunzi wamerudi likizo fupi toka Ijumaa ya tarehe 03 March 2023, Ila cha kushangaza hadi leo hii wanafunzi hawajapokea meseji za pesa zao na hata hawajasaini pesa hizo.
Ikumbuke pia wanafunzi wengi kuanzia mwaka wa pili hadi wa 3 wanahitajika kwenda Field Practical Training toka tar 06 March katika Mikoa tofautitofauti hapa Tanzania, Ila mpaka muda huu ninavyotype hapa wanafunzi kutoka chuo hicho(SUA) hawajaondoka kwenye vituo vyao vya field na wiki inakatika namna hii.
Kwa mujibu wa Mwanafunzi wa mwaka wa tatu kutoka chuo hicho jina kapuni alisema kuwa "Baada ya kumaliza mitihani yetu ya semista tuliambiwa tusiondoke ili tusubiri pesa za kijikimu(boom) ambazo zitatumwa kabla ya tar 06 March 2023 Kisha tuondoke tuende vituoni Ila Cha kushangaza hatuchapata pesa hadi leo hii na tarehe za field zishafika/zishaanza".
Ni ajabu sana na inasikitisha, sijui kwanini bodi ya mikopo wanafanya mambo meusi kama haya hali ya kuwa Almanac(Ratiba) zote za kila chuo wanazo. Field ni sehemu ya masomo/mafunzo ya mwanafunzi Ila kutokana na kisuasua kwao kunawafanya wanafunzi wakeshe mitaani wakizurura na pesa za kijikimu hamna.
HESLB Mnachokifanya ni Hujuma kubw kwa Rais wetu wa JMT ambaye aliongeza pesa nyingi kwa mwaka Husika wa masomo ili ziwasaidie wanafunzi katika harakati za masomo yao, kwanini nyie mnatoa pesa kwa magendo na pasipo kuendana na wakati au muda..?
Wahusika mliangalie hili huko vyuoni Hali ni mbaya sana, Fanyeni hima mupeleke pesa za wanafunzi vyuoni, hizo ni Haki yao.