Kwa imani yangu, wote ni Watanganyika. Hakuna Mtanganyika Priority na Mtanganyika Non-priority. Taifa hili lina uwezo kabisa wa kutoa Elimu Bure kuanzia Vidudu hadi Elimu ya Vyuo Vikuu bila kubagua Watanganyika katika misingi ya Priority na Non-priority. Shida/tatizo ni ubinafsi. Hebu fuatilia ubishi ukiopo kuhusu Ukaguzi wa Mahesabu ya Ruzuku zinazotolewa na Serikali kwa Mwaka kwa Vyama vya Siasa. Nimeshangaa kusikia Vyama vya Siasa vinapata Ruzuku ya MABILIONI kila Mwaka! Kwa kazi gani? Ni pesa nyingi mpaka zinawashinda hata kuzifanyia Ukaguzi wa Mapato na Matumizi! Vipi, mfano 25% ya hiyo jumla ya Ruzuku ikapelekwa kama Ruzuku kwenye Elimu na Taasisi za Elimu? Si italisaidia Taifa kuliko Wanasiasa wachache ambao wengi wamesoma bure wakati wa Mwalimu? Tatizo ni ubinafsi wa Watunga Sera wetu. Inauma sana!