Hezbollah imesema hawatasalimu amri kwa vitisho vya Israel

The Zanzibar Echo

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2025
Posts
490
Reaction score
838
Kiongozi mpya wa Hezbollah, Naim Qassem, amesema kundi lake halitoweka chini silaha wala kujisalimisha licha ya vitisho vya Israel. Akihutubia maelfu ya wafuasi wake wakati wa maadhimisho ya Ashura mjini Beirut,
Qassem alisisitiza kuwa, "vitisho hivyo havitatufanya tukubali kusalimu amri.”

Qassem, aliyemrithi Hassan Nasrallah aliyeuawa na Israel Septemba mwaka jana, amesisitiza kuwa Israel lazima ijiondoe kwenye maeneo ya Lebanon na kuachia wafungwa kabla ya kuanza mazungumzo kuhusu usalama wa taifa.

Tamko lake linakuja wakati mjumbe wa Marekani, Tom Barrack, anatarajiwa kuwasili Beirut kuwasilisha wito wa kuitaka Hezbollah ivunje nguvu zake za kijeshi kufikia mwisho wa mwaka huu. Hata hivyo, mashambulizi ya Israel yameendelea licha ya makubaliano ya kusitisha vita yaliyofikiwa Novemba.
 
Wapigane sasa, hao washakosa la kufanya hawana pesa,nguvu,hamasa na hawana tena washabiki wajinga kila mlebanon anawaona wajinga kwa kila tamko la kipashkuna, huku wanachapika kila siku na location wanatoa wanalebanon wenyewe itakuwa
 
Back
Top Bottom