SankaraBoukaka
JF-Expert Member
- Jul 2, 2019
- 3,577
- 5,664
Katika hali ya kushangaza na ya kusikitisha, imekuwa kawaida sasa kwa timu mbalimbali kushiriki mashindano makubwa bila kujulishwa wazi zawadi au motisha wanazotarajiwa kupewa iwapo zitashinda. Hii siyo tu inakatisha tamaa, bali pia ni aibu kwa taifa kama Tanganyika, lenye historia ndefu ya mapambano na mshikamano wa wananchi wake. Inashangaza kuona juhudi za vijana, jasho lao, na muda wao vikidharauliwa kwa kutoweka wazi taarifa muhimu kama zawadi za mshindi.
Timu nyingi hushiriki kwa moyo wote, zikiamini kuwa kuna heshima na zawadi stahiki zikiibuka washindi, lakini mwisho wake huwa ni porojo, vyeti vya karatasi, au ahadi zisizotekelezwa. Hili linafanyika mbele ya vyombo vya habari na viongozi wa serikali bila haya. Kwanini timu zishindane bila hata kujua ni kiasi gani mshindi atapata? Hii ni dharau ya wazi kwa wanamichezo wetu.
Kwa mfano, TFF (Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania) wamepokea zaidi ya shilingi bilioni 3, lakini hadi leo watanganyika hatujui mchanganuo wa matumizi ya hizi hela. Timu shiriki hazijui hata bingwa wa mashindano makubwa atapata kiasi gani. Kichekesho hiki kimevuka mipaka ya busara , ni ujinga na fedheha kabisa. Mbona wako haraka kutoa makaripio, faini, na adhabu kwa timu au wachezaji, lakini hawako tayari kabisa kueleza matumizi ya hizo hela?
Kama wanaona sisi wananchi hatuhitaji kujua, basi kwanini wawe wanajitokeza mbele ya umma kutoa ahadi za uwazi na uwajibikaji? Kwanini wawe wanatutangazia udhamini wanaoupata?
Ni wakati sasa kwa wanamichezo, mashabiki, na jamii kwa ujumla kudai uwazi na heshima. Michezo ni sehemu ya maendeleo ya taifa, na kama tunataka kujenga mfumo wa haki na uendelevu, basi TFF na vyombo vingine vya michezo lazima viwajibike kwa umma.
Tanganyika haiwezi kuendelea kuwa nchi ya ajabu inayowachezea vijana wake kisaikolojia na kiuchumi kwa sababu ya ukimya, uzembe na tamaa ya wachache.