Buyaka
JF-Expert Member
- Jul 29, 2010
- 1,705
- 1,953
Kachukue show room kwa 35M mkuu
Acha hasira kwenye biashara.
Ukisema gari yako nafuu vinginevyo "kanunue show room" inabidi gari yako nayo iwe iko show room au ina hadhi ya show room, imeshuka nchini majuzi.
Gari yako imepigika hapa Bongo tayari, gari za showroom japo sio mpya lakini angalau zimetoka Kumamoto moja kwa moja ambako abiria hawapandi daladala na virumbesa vya viazi, mikaa, mbuzi, mbolea, mitumba, shisha, pembe za ndovu, maiti!
Tena njia ya Gongo la Mboto! Mbovu ajabu... na hapo hatujui ni kifaa gani kilikushinda ukaweka feki cha Mchina uuze gari uachane na stress.
Kwa hiyo acha hasira, nadi bidhaa yako kwa upole, professionally.