PostGE2025 Hichi kipindi ni fursa adhimu ya vuguvugu jipya la vyama vya siasa nchini

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Naantombe Mushi

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2015
Posts
6,253
Reaction score
15,748
Kwa sisi watafiti, nguzo yetu kubwa ni kugundua chanzo cha tatizo na kulichambua vema, ili kuja na suluhisho.

Kwa kilichotokea Octoba 29, japo chanzo chake, kwa nje, inaonekana ni "ujeuri na ubabe wa Chama cha Mapinduzi (CCM)," ila ki uhalisia kabisa, chanzo kikuu, mimi naweza kusema, ni kukosekana kwa mrengo imara wa vyama vya siasa vya upinzani; na sio vyama vya upinzani vilivyotengenezwa na vinavyoongozwa na dola, kwa mlango wa nyuma.

Kuelekea Octoba 29, ndo watanzania wengi tumegundua ya kwamba, kuna makosa yalifanyika mwaka 1992: wananchi wazalendo walijisahau, na kuwaachia CCM na dola, kuhodhi vuguvugu la vyama vya upinzani vyenye magamba ya ki-CCM.

Na ikumbukwe: mchakato wowote wa kisiasa kama; kupata katiba mpya, tume huru ya uchaguzi, na kutunga sheria sheria mbali mbali, na hayo yote ni michakato ambayo inahusisha ushiriki wa vyama vya kisiasa vya upinzani; CCM wamejikuta wakati wote, wakiwa kwenye hali ya kunufaika, kwa kuweza kujihakikishia uungwaji mkono kwenye kila mchakato wowote wa kisiasa, uchaguzi ukiwemo.

Hivyo, kwakuwa nadharia ya ukaribu wa anguko la CCM bado inaishi; wananchi wazalendo watanzania, wanawajibika moja kwa moja, kuja na mirengo mipya na imara ya vyama vya kisiasa, vya kisasa, na vinavyoendana na utamaduni wa mtanzania.

Mchakato huu ni muhimu kufanyika, na wakati wake ni sasa, ikiwa kweli tunataka, kama nchi, kujiokoa na hali ya nchi kuingia machafukoni au jeshi kuchukua nchi kwa mapinduzi, pale CCM itapofikia tamati.

Uwepo wa vyama imara vya kizalendo utazuia machafuko, au nchi kutawaliwa na jeshi, kwa sababu, CCM itapofika tamati, basi hakutakuwa na ombwe la uongozi, kwa sababu, chama imara cha kizalendo kitashika dola.

Wakati ni sasa; hakutakuwa tena na kipindi kizuri cha harakati mpya za kisiasa, zaidi ya hichi kipindi ambacho, CCM wapo kwenye taharuki.

Wenu,
N.Mushi
 
Vyama vya siasa vinasajliwa kwa msajili. Msajili mwenyewe mtu wa dola. Kabla hawajakipa chama usajili wanafanya sana scanning kuona kama kitakua ni shida kwa chama dola au kitaingia ktk mnfumo. Na hap ndio mara nyingi kupandikizwa mapandikizi ktk uongozi wa chama. Vinginevyo vihunzi ivyo vikirukwa mawazo yako ni mazuri. Kudos.
 
Y

Yote hayo muarobaini wake ni katiba mpya.
 
Vyama vya siasa vilivyoinyume na ccm haviwezi pata usajiri nchi hii na hata vikipatav vitajaziwa mapandikizi ya ccm,ikishindwa itapambana nacho kwa nguvu ya dola kwa kukiweke vikwazo vyote ikibidi kutrka na kuua na kesi za hovyo.
Shida ya nchi hii ni ccm ya wahuni.
 
Vyama vya siasa vinasajliwa kwa msajili. Msajili mwenyewe mtu wa dola. Kabla hawajakipa chama usajili wanafanya sana scanning kuona kama kitakua ni shida kwa chama dola au kitaingia ktk mnfumo. Na hap ndio mara nyingi kupandikizwa mapandikizi ktk uongozi wa chama. Vinginevyo vihunzi ivyo vikirukwa mawazo yako ni mazuri. Kudos.
Penye nia pana njia. Hata kama msajili ni dola ila ukiwa na wazalendo wa kweli, uwezekano wa kuwa na vyama imara unakuwa ni mkubwa
 
Vyama vya siasa vilivyoinyume na ccm haviwezi pata usajiri nchi hii na hata vikipatav vitajaziwa mapandikizi ya ccm,ikishindwa itapambana nacho kwa nguvu ya dola kwa kukiweke vikwazo vyote ikibidi kutrka na kuua na kesi za hovyo.
Shida ya nchi hii ni ccm ya wahuni.
Ukiwa na nia na watu thabiti, hizo hila zote ni rahisi kupambana nazo
 
Mleta maada tukupe tu taarifa, Tangu 1992 ni kwa mara ya kwanza CCM wamepata mpimzani 2025.

Hata wao wanajiuliza ilikuaje kuaje tumeruhusu hili kutokea.

Sasa wewe nawe unataka kuongeza CHAMA kingine serious cha 2? Labda ukakisajili UN, na kiwe kinaongozwa club house, ila kama unataka kusajili hapa Bongo haufanikiwi.

Dawa ni kuanza kama CHADEMA tu ya mbowe, Mkishakua na Ngivu ya Wanachi mnawabadirishia gia hewani kama lissu
 
Hao watu unawatoa wapi wewe wakati chama chako ni kipya?

Unlesa otherwise limeguke kundi linalo aminika kutoka CCM liunde CHAMA lkn kama ni wapinzani kweli hawawezi kusajiliwa.

Alizuiliwa Mpina, Asie na impacts yeyote kugombea sembuse wazo lako la chama serious
 
And you think this is just political ?!!!!

Hii ni zaidi ya Siasa na nane aliyepo bali juu; hili ni bomu la watu kuwa mafukara na kuona wazi kabisa kwamba keki ya taifa inaliwa na wachache bila hope yoyote ya kesho yao...

Na kwa taarifa yako hii ni rasharasha mvua yenyewe itakuja hapo Gen Alphas watakapokuwa umri wa watu wazima - kama hakuna mabadiliko basi machafuko itakuwa order of the day....

Does not matter the color of the Cat....; kama hawezi kushika panya basi outcome itakuwa ileile - Hana faida
 
Nchi ya watu milioni 70; haiwezi kuwa shida kupata wanachama watiifu 2000 wa kukipigania chama.

Ni mipango tu, wala sio shida.
 
Mleta maada tukupe tu taarifa, Tangu 1992 ni kwa mara ya kwanza CCM wamepata mpimzani 2025.

Hata wao wanajiuliza ilikuaje kuaje tumeruhusu hili kutokea.

Sasa wewe nawe unataka kuongeza CHAMA kingine serious cha 2? Labda ukakisajili UN, na kiwe kinaongozwa club house, ila kama unataka kusajili hapa Bongo haufanikiwi.

Dawa ni kuanza kama CHADEMA tu ya mbowe, Mkishakua na Ngivu ya Wanachi mnawabadirishia gia hewani kama lissu
Sijakuelewa unavosema, "kwa mara ya kwanza CCM wamepata mpinzani mwaka 2025." Una maana gani haswa? Gen Z kwako ni wapinzani?
 
And you think this is just political ?!!!!

Hii ni zaidi ya Siasa na nane aliyepo bali juu; hili ni bomu la watu kuwa mafukara na kuona wazi kabisa kwamba keki ya taifa inaliwa na wachache bila hope yoyote ya kesho yao...

Na kwa taarifa yako hii ni rasharasha mvua yenyewe itakuja hapo Gen Alphas watakapokuwa umri wa watu wazima - kama hakuna mabadiliko basi machafuko itakuwa order of the day....

Does not matter the color of the Cat....; kama hawezi kushika panya basi outcome itakuwa ileile - Hana faida
Kwahiyo unashauri nini? Hakuna umuhimu wa mrengo mpya wa kisiasa, kupitia kuasisi vyama vipya?
 
Back
Top Bottom