Hichi kitita kipya cha NHIF kina nini ndani yake? Kwanini kipigiwe debe na kupingwa vikali? Tujadiliane

Hichi kitita kipya cha NHIF kina nini ndani yake? Kwanini kipigiwe debe na kupingwa vikali? Tujadiliane

Shida kubwa ni kutengeneza perspective zenu kuliko kusikiliza kiini cha mzozo from the horse’s mouth (waziri au yule mwenyekiti wa kamati ya tume iliyofanya review).

Dawa
Serikali aijapunguza dawa, kuna orodha ya dawa karibu 750.

Wamefanya price review kwa kuangalia price ya wholesalers 10, na kutumia hizo data kupata average price kama bei ya NHIF kulipia dawa.

Kiasi watakacholipa kwenye dawa pia kinazingatia gharama (hesabu) za unit costs za hospitali.

Baada ya review zao 2/7 ya dawa zote zimeshuka bei, 2/7 ya dawa zote bei yake ni ile ile ya awali na 3/7 ya dawa wamekubali kulipa zaidi (bila ya kuombwa).

Vipimo
Vipimo vinafanywa na machine au laboratory tests.

Machine zinanunuliwa na zina life span. Wamezingatia depreciation rate (uchakavu utokanao na matumizi yake) ili kubaini kiasi gani cha matumizi na tozo kinahitajika kununua machine mpya (recover cost or break even).

Baada ya hapo wakajumlisha na faida ya matumizi (hiyo machine sio charity lazima itengeneze faida), wakajumlisha costs za mishahara ya wahusika wanao operate hizo machine na wataalamu wote. Total ndio kigezo cha gharama watakazolipa kwenye kila kipimo.

Matibabu
Wamepiga hesabu za hospital bed services costing (huo ndio utaratibu wa kupanga bei za huduma ya afya duniani, sio Tanzania tu). Wakaangalia kila huduma inayotelewa na kupanga bei + profit.

Consultation
Hii wametumia average ambayo imekuwepo sokoni na kufanya national standardisation, hapa hakuna malalamiko.

Kiwango cha faida wanachoruhusu
Kwenye kila faida katika dawa, matibabu, na vipimo. Wameset viwango vya ‘cost + percentage (ambazo ni either 10%, 15% or 20%).

10% ni kwa dawa, huduma au vipimo zinatolewa kwa wingi, ndogo kwa sababu wana benefit ya economic of scales.

15% ni kwa dawa, huduma na vipimo ambazo movement zake ni median.

20% ni kwa zile ambazo slow moving medication, vipimo ambavyo sio regular au havina watu wengi na matitabu ambayo ni machache kwa siku kama operations kubwa kubwa.
…………,.

Hao watoa huduma binafsi za afya wameshindwa kujibu justification ya bei za ivyo vitita vya serikali with counter argument pamoja na kupewa muda wamekimbilia kugoma.

Shida yetu watanzania atupendi kusikiliza ndio maana mtu kama Magufuli ambae hakuwa na huu muda wa kupoteza kutoa elimu kila siku. Ambae alikuwa aelewi anachosema ataelewa kwa action za serikali mbeleni.
 
Naona sasa hivi taratibu ukweli unaanza kufahamika, jana NHIF wamerudisha dawa 178 ambazo walizitoa kwenye kitita kipya na bila ya aibu walikuwa wanashupaza shingo kuwa hawajapunguza isipokuwa dawa zote muhimu zipo kwenye kitita.

Huu mfuko unaendeshwa kisanii na siasa sana, yaani bado wana ile principle ya tengeneza matatizo kibao kwa makusudi kwa mikono na akili yako kisha tatua robo tu ya hayo matatizo na anza kujisifu na kuomba pongezi za watu.

Kwa mwendo huu nina hakika yale yote yaliyosemwa kuwa yameletwa na hawa jamaa moja baada ya jingine yatatuadhibu huko mbeleni.

Changamoto kubwa ni kuwa wanataka watengeneze faida kubwa kupitia michango yetu ili watumie wanavyotaka wao na si kugharamia huduma za matibabu za wanachama.
 
Back
Top Bottom