Hidden cancer cures

Hidden cancer cures

mkuu Deception naomba unipe ufafanuzi juu ya matumizi ya hiyo black seed oil(mafuta ya habbat sauda) kama tiba ya saratani
Nilikuwa namaanisha niitumie vipi ili iwe tiba?

Nilitaja baadhi tu ya vyakula/vitu vinavyotibu cancer,lakini ili ujue utatibu vipi cancer inabidi kwanza ujue cancer ni nini na mambo gani yanayoweza kumsababishia mtu cancer mwilini na kwa vipi.

Nisingependa kukujibu moja kwa moja kwa kuwa masuala ya afya si ya kuchukulia kirahisi rahisi,inatakiwa nikupe jibu la uhakika kwa kuwa wanaosoma maelezo haya ni wengi na wengi hudiriki hata kuyatumia moja kwa moja ili kutibu maradhi yao.

Ninakushauri ufuatilie uzi wote huu kwa makini sana na utakapomaliza najua lazima utakuwa umeshajua cancer ni nini na mtu anapataje cancer na inatibika vipi.Utapata tiba nyingi zaidi ya hiyo unayouliza.Tiba hizi si za kufikirika,zimefanyiwa utafiti na zimeshatibu watu wengi na zinaendelea kufanya hivyo.Cha msingi ni wewe kusoma na kudadisi tu,elimu hii ni ya bure kabisa utalipia muda wako tu wa kusoma.Ni vigumu sana kupata watu kama sisi tunaotoa elimu kama hizi bure.Watu wengi wanafanya elimu hizi kama mitaji.

Kazi kwako sasa.Niko tayari kukujibu endapo utakuwa na maswali pale ambapo hujaelewa.

Karibu.
 
mkuu Deception uzi nimeufuatilia vizuri kuanza mwanzo mpaka hapa na nimeuelewa sana niliuliza hivyo kwa sababu ili kama utaikosa hiyo vitamin B17 na hayo mafuta ya bangi kipi utumie mbadala wake kwa sababu hizo ampricot sio kote zinapatikana,na katika ile thread nimeona black seed oil ndomana nikauliza
Ahsante mkuu
 
Last edited by a moderator:
mkuu Deception kama nitakuwa nimekosea utanirekebisha
Saratani ni hali ambapo kunakuwa na ukuaji usio wa kawaida wa seli ambazo sio za kawaida katika mwili mwa binadamu,na ukuaji wa hizo seli huanza kushambulia baadhi ya tishu kama vile ini,damu,figo na nyenginezo.Sababu kuu ya kansa katika mwili ni upungufu p wa kinga pamoja na external toxic zinazoingia mwilini,mwili ukiwa na kiwango kikubwa cha asidi na sumu husababisha seli kufa na baadhi kubadilika(mutate) na kuwa seli za kansa,hivyo ili kuponya kansa ni lazima uweke sawa alkaline katika damu na uondoe sumu zote,
baada ya kufanya hayo mambo kinachofuata ni kula vyakula ambavyo ni anti cancerous cells kama amygdalin(vitamin b17),hemp oil-ili kuuwa kansa cells huwezi kuponya kansa kama damu yako ni chafu kwa maana ina asidi na sumu nyingi.hivyo ni vyema ukaondoa sumu kwanza huku ukiendelea kuchukua hzo anti cancerous cells kupunguza ukuaji wa hzo seli za kansa na hatimaye kuziuwa kabisa
Mkuu Deception mpka hapo nipo sawa na wewe au umeniacha njia panda?
 
Last edited by a moderator:
mkuu Deception kama nitakuwa nimekosea utanirekebisha
Saratani ni hali ambapo kunakuwa na ukuaji usio wa kawaida wa seli ambazo sio za kawaida katika mwili mwa binadamu,na ukuaji wa hizo seli huanza kushambulia baadhi ya tishu kama vile ini,damu,figo na nyenginezo.Sababu kuu ya kansa katika mwili ni upungufu p wa kinga pamoja na external toxic zinazoingia mwilini,mwili ukiwa na kiwango kikubwa cha asidi na sumu husababisha seli kufa na baadhi kubadilika(mutate) na kuwa seli za kansa,hivyo ili kuponya kansa ni lazima uweke sawa alkaline katika damu na uondoe sumu zote,
baada ya kufanya hayo mambo kinachofuata ni kula vyakula ambavyo ni anti cancerous cells kama amygdalin(vitamin b17),hemp oil-ili kuuwa kansa cells huwezi kuponya kansa kama damu yako ni chafu kwa maana ina asidi na sumu nyingi.hivyo ni vyema ukaondoa sumu kwanza huku ukiendelea kuchukua hzo anti cancerous cells kupunguza ukuaji wa hzo seli za kansa na hatimaye kuziuwa kabisa
Mkuu Deception mpka hapo nipo sawa na wewe au umeniacha njia panda?

Naomba nikujibu kuwa uko sawa in a way but si vitamin B17 pekee unayo hitaji! Kuna matumizi ya warm lemon water and a lot of other things kama blackstrap molases, wheat grass juice na kadhalika ili kutibu cancer but so far uko sawa kiasi
 
Last edited by a moderator:
Naomba nikujibu kuwa uko sawa in a way but si vitamin B17 pekee unayo hitaji! Kuna matumizi ya warm lemon water and a lot of other things kama blackstrap molases, wheat grass juice na kadhalika ili kutibu cancer but so far uko sawa kiasi

mkuu napoteza nashukuru kwa kujibu swali.
 
Last edited by a moderator:
Mambo ya msingi yanayoweza kusababisha cancer mwilini:

Kwanza kabisa inabidi watu wafahamu kwamba,kila mtu mwili wake unajiponya cancer kila siku katika maisha yake,yaani namaanisha kwamba kila mtu hupata cancer kila siku lakini mwili wake hujiponya kila siku.Hii inatokana na uimara wa kinga ya mtu.

Hivyo basi,ukiona mtu amepata cancer inabidi ufahamu kwanza kabisa kwamba kinga ya mtu huyo ina matatizo,halafu pili ndio unatakiwa kuanza kudadisi mambo yaliyoingia ndani ya mwili wake ambayo kinga yake imeshindwa kuyazuia na hatimaye kumsababishia cancer.

Hivyo basi,mpaka hapo tunaweza kutenga sababu zinazosababisha cancer kwenye makundi mawili ili kurahisisha kuelewa vizuri.Kwanza ni kinga ya ndani ya mwili,na pili ni sababu zitokazo nje ya mwili ambazo huingia ndani ya mwili na kushindwa kuzuiwa na kinga ya mwili na hatimaye kusababisha cancer.

1.Kinga ya mwili:
Mwili unapopata cancer hujiponya wenyewe kwa kutumia kimengenyo cha protini kinachotolewa na kongosho/pancreas kiitwacho trypsin kikishirikiana na chembe nyeupe za damu kufanya kazi hiyo.Chembe nyeupe za damu hazina uwezo zenyewe kushambulia chembe za cancer kwa kuwa zenyewe ni chaji hasi(-ve) pia chembe za cancer ni chaji hasi(-ve) hivyo hukwepana,sasa basi, kazi ya kimeng'enyo cha trypsin ni kumeng'enya ukuta wa nje wa chembe za cancer ambao ni wa protini na una chaji hasi(-ve) na baada ya chembe za cancer kumengenywa huwa zinaachwa uchi na kushambuliwa kwa urahisi na chembe nyeupe za damu.Hivi ndivyo mwili unavyojiponya cancer kila siku.

Kwa watu ambao kongosho zao hazifanyi kazi sawasawa na wanaishi maisha hatarishi huweza kupata cancer kwa urahisi sana.

2.Sababu zitokazo nje ya mwili:
Pamoja na kinga ya mwili kufanya kazi kama nilivyoeleza hapo juu,lakini pia si njia pekee ya kuzuia cancer,hii ni kwa sababu kuna mambo mengi mwilini ambayo yanatakiwa yawe kwenye mlinganyo unaotakiwa kiasilia ili mwili wote uweze kufanya kazi kwa kutegemeana.

Mambo haya ni kama vile;
i/. Kiwango cha tindikali/nyongo(alkali) kwenye damu(blood alkalinity level) ambayo inatakiwa iwe 7.365,
ii/. Mwili unatakiwa uwe na kiwango thabiti cha methly group/HCL tumboni,yaani kiwango kizuri cha tindikali ya HCL kwenye tumbo.Methyl groups husaidia kushikilia maji kwenye utumbo nk,inabidi watu wafahamu kwamba zaidi ya 90% ya afya ya mwili huanzia kwenye utumbo,
iii/. Mwili unatakiwa uwe na vitamini zote muhimu,
iv/. Mwili unatakiwa uwe na madini yote muhimu,
na mambo mengine machache.

Hutakiwi kuogopa kwa kuona kwamba unatakiwa ufanye mambo mengi sana,la hasha,bali mambo yote hayo unaweza kuyakamilisha kwa kufanya vitu vichache sana.

Sasa basi mwili unaweza kuwa na mapungufu katika mambo hayo i-iv kutokana na utaratibu mbovu wa maisha na hasa ule wa kula vitu visivyofaa.Ukila vyakula BORA vya ASILI kwenye mlinganyo unaotakiwa,mwili wako utaondokana na mapungufu ya vitu hivyo nilivyovitaja.

Ulaji wa vyakula vya viwandani/processed foods/enriched foods kama vile white sugar,white flour/sembe,white rice,white salt/chumvi ile ya unga,cornfalkes,KFC foods,vinywaji kama vile soda na juisi zilizosindikwa.Pia ulaji wa mara kwa mara wa vyakula kama vile nyama nyekundu,vyakula visivyooshwa vizuri kutoa sumu za mashambani(pesticides) na pombe kali/zisizo na viwango mara kwa mara,madawa ya hospitali mara kwa mara na mambo mengine kama hayo yanayokiuka asili ya mwanadamu yanaweza kutoa mchango mkubwa sana kusababisha cancer.

Ulaji wa vitu hivyo unaweza kukufanya uwe na tindikali nyingi kwenye damu kitu ambacho ni hatari sana.Uwiano mzuri wa tindikali/nyongo kwenye damu ndio kitu cha msingi sana kukiangalia,wagonjwa wote wa cancer ukiwapima damu zao utaona kwamba damu zao zina tindikali nyingi kuliko kiwango cha kawaida.Hivyo basi,ukiwa na tindikali nyigi kuliko kawaida kwenye damu utapoteza madini mengi muhimu kama vile calcium,magnesium na madini mengine muhimu madogo madogo ambayo yote hayo yana umuhimu mkubwa wa kupigana na cancer,pia ini haliwezi kufanya kazi yake vizuri katika hali ya tindikali nyingi,hali hii pia huweza kuathiri kongosho kushindwa kufanya kazi yake ipasavyo.Hivyo ulaji huu mbovu utakufanya uangukie kwenye matatizo namba i hadi namba iv hapo juu.
Hivyo basi,kama una cancer,huwezi kupona daima kama damu yako ina tindikali.Ili upone kwanza rekebisha kiwango cha tindikali/nyongo(alkali) kwenye damu halafu ndio uendelee na mambo mengine muhimu.

Sasa basi,ili uwe na afya njema na upone cancer kama unayo,inabidi mwili wako uupe virutubisho vyote muhimu ili kuipa nguvu kinga ifanye kazi kwa urahisi.Virutubisho hivi utavipata kwa kula vyakula vya asili vya aina mbalimbali ambavyo vina kazi tofauti mwilini;

1.Ule vyakula vyenye uwezo wa kufanya damu yako iwe na kiwango kizuri cha alkali;
Baadhi ya vyakula hivyo ni juisi ya mboga mbichi za majani kama vile spinach,celery,matembele,broccoli,juisi ya maji ya limao/ndimu nk.

2.Ule vyakula vyenye uwezo wa kuondoa sumu mwilini;
Baadhi ya vyakula hivyo ni tumeric/bizari mbichi,tangawizi,parachichi na mbegu yake,juisi ya maji ya limao/ndimu,juisi ya ubuyu/ukwaju,black seed oil/mafuta ya habbat sauda,kitunguu saumu,juisi ya apple/tufaa,aloevera/shubiri nk.

3.Ule vyakula vyenye uwezo wa kutibu tatizo husika,ambapo kwa maana hii tunazungumzia cancer;
Baadhi ya vyakula hivyo ni mbegu za apricot,mbegu za peach,mbegu za almond,mtama,ulezi,mbegu za maboga,ufuta,juisi/mafuta ya jani kibichi ya bangi,backing soda,juisi ya karoti,juisi ya stafeli nk.

MUHIMU:

1.Huwezi kupona cancer kama damu yako ni acidic,yaani ina tindikali.Inabidi damu iwe alkaline/nyongo kwa kiwango kinachotakiwa ndio uweze kupona.

2.Huwezi kupona cancer kama mwili/damu yako ina sumu.Inabidi uondoe sumu ndio uweze kupona.

3.Ukifanya namba 1 na namba 2 hapo juu ndio hatua namba 3 itafanikiwa kwa urahisi sana.Hapa kwenye hatua hii ni kula vyakula vyenye uwezo wa kuua moja kwa moja chembe hai za cancer.Chembe hizi zikifa hazirudi tena kwa kuwa tayari damu iko safi na mwili/damu haina sumu tena hivyo madini muhimu hayawezi kupotea mwilini.

Hii ndio sayansi ya cancer kwa lugha ya ki laymen/rahisi kabisa.

Baadaye nitaenda specific kwenye tiba mojawapo niliyoizoea na kuwapa specifications zake jinsi ya kumtibu mgonjwa ambaye tayari ana cancer na mmepoteza matumaini kabisa.
Deception kwa huu Uzi
Nimekuelewa zaidi ya ulivyo tarajia.
 
Sasa tuzungumzie tiba maalum ya cancer:
Kama nilivyoeleza mwanzoni kwamba kuna tiba nyingi za cancer ambazo zimetuzunguka bila sisi wenyewe kujua kutokana na kutokuwa na maarifa na kudanganywa na sekta rasmi ya tiba za magharibi.Tiba hizo zinakuwa na nguvu zaidi kama zitatumika kwa kushirikiana na tiba nyingine.

Kwa sasa nitazungumzia kimelea cha asili kiitwacho amygdalin,jina la kawaida inaitwa laetrile,kimelea hiki kimepewa jina ambalo sio rasmi na kuitwa vitamin B17.Kimelea hiki kinapatikana kwenye vyakula vya asili kama vile; mbegu za apricot/peach/almond,mbegu za maboga,mbegu za ufuta,mtama,ulezi,mbegu za alizeti,mihogo mibichi,uyoga.

Lakini kimelea hiki kinapatikana kwa kiwango kikubwa zaidi kwenye mbegu za apricot/almond.Kwa mtu ambaye haumwi cancer anashauriwa awe anakula tu vyakula vya aina hii na kamwe hatopata cancer.Lakini kwa mtu ambaye tayari ana cancer anashauriwa apate kimelea hiki kikiwa katika concetrated form.Concentrated form ya kimelea hiki inapatikana baada ya kufanya solvent extraction kutokana kwenye vyakula vinavyobeba kimelea hiki kwa kiwango kikubwa kama vile mbegu za apricot.

Baada ya kupatikana kwa kimelea hiki kwenye concentrated form,mgonjwa anaweza kutumia kama food supplement kama chakula katika dozi maalum itakayopendekezwa au kwa njia ya IV injection.Kumbuka kwamba kabla ya kutumia hiki kimelea hakikisha umepitia au unafanya kwa pamoja na hatua ile ya kwanza na ya pili,yaani unafanya therapy ya kuiweka pH ya damu yako iwe alkaline(pH=7.365) halafu unafanya therapy ya kuondoa sumu mwilini kwa pamoja.Mambo haya yakienda pamoja ndio tiba inakuwa imekamilika.

Kazi ya vitamin B17 ni kuua chembe za cancer,chembe hizi zinapouawa cancer inatoweka na haiwezi kurudi kwa kuwa mazingira yanayofanya cancer kuwepo yanakuwa yameshaondolewa,yaani mwili unakuwa hauna sumu na pH ya damu iko sawa,hivyo ukipona umepona,yaani cancer ndio imekwenda zake,haiwezi kurudi.Kwa wale mliofanikiwa kupitia ile documentary nadhani mtakuwa mnaelewa ni kwa jinsi gani/kwa vipi vitamin B17 inaua chembe za cancer,nisingependa nielezee hapa kwa kuwa nataka kuokoa muda na nafasi.

Sasa basi,kama una mgonjwa wa cancer,kwanza kabisa hakikisha anapitia hatua ya kwanza na ya pili huku wakati huohuo ukimpatia vitamin B17 ili kuzuia cancer isiendelee zaidi.Mara nyingi kwa cancer zilizokaa muda mrefu huweza kupona kuanzia miezi 3.Haijalishi ni cancer gani,vitamin B17 inatibu au inaua cancer yoyote ile mwilini.Kwa wale wagonjwa waliopitia tiba za hospitalini kama vile chemotherapy na mionzi huweza kuchukua muda mrefu zaidi kupona kutokana na uharibifu uliofanywa na chemo na mionzi.Wagonjwa hawa ni vizuri kuwapa madini ya zinc ili kurahisisha usafirishwaji na unyonywaji wa vitamin B17 mwilini.

Utaratibu wa kutumia vitamin B17/amygdalin/Laetrile:

1.Hakikisha pH ya damu ya mgonjwa iko sawa kwa kula vyakula nilivyovitaja mwanzo.

2.Hakikisha mgonjwa anakula vyakula vinavyoondoa sumu mwilini kama nilivyovitaja.Hapa nitaongezea supplement iitwayo pangamic acid ambayo ina uwezo mkubwa wa kuondoa sumu mwilini.Dozi ya pangamic acid ni 500mg mara mbili kwa siku,yaani asubuhi na jioni.

3.Sasa ili kuua chembe za cancer utatumia vitamin B17,500mg mara mbili kwa siku,asubuhi na jioni.Pia kuna supplement iitwayo zinc citrate(20-50 mg mara mbili kwa siku)ambayo husaidia kusafirishwa na kunyonywa kwa vitamin B17 haraka mwilini.Pia kuna supplement iitwayo bromelain/papain,hizi ni proteolytic enzymes ambazo kazi yake ni kumenya ukuta wa nje wa chembe za cancer ambao kiasilia ni wa protini na kuziacha wazi ili kushambuliwa na kinga ya mwili.Kazi ambayo inafanywa na hizi proteolytic enzymes ni sawa na ile inayofanywa na trypsin itolewayo na pancreas/kongosho.

NB:
Bromelain:Hutokana na extract ya tunda la nanasi/pineapple.
Papain:Hutokana na extract ya tunda la papai/pawpaw.

Hivyo basi,mgonjwa anatakiwa atumie aidha bromelain au papain na si zote mbili kwa pamoja,200mg mara mbili kwa siku.

Vitamin B17 inatakiwa itumiwe pamoja na zinc citrate na pangamic acid.Bromelain au papain zinatakiwa zitumiwe asubuhi kabisa kabla mgonjwa hajakula chochote.

ANGALIZO:
1. Vitamin B17 na pangamic acid zinashusha presha na hivyo basi ni vyema mgonjwa akajua mapema hili.Dozi niliyoitoa hapo juu ni maalum kwa wagonjwa ambao wana presha ya kushuka.Kwa wale wasio na presha kabisa dozi yao inaongezeka na kufikia 1000mg mara mbili kwa siku kila moja.Vitamin B17 na pangamic acid zina faida mara mbili kwa wagonjwa wa cancer wenye presha ya kupanda kwa kuwa zinashusha presha.

2.Zinc citrate inaweza kusababisha mgonjwa kujisikia baridi hasa viganjani, pia homa kama mgonjwa atazidisha dozi.

3.Bromelain au papain huweza kusababisha maumivu ya tumbo kwa baadhi ya wagonjwa lakini si wote.Endapo mgonjwa atapata maumivu ya tumbo anaweza kupunguza dozi au kuiacha kabisa na kuendelea na nyingine zilizobaki kwa kuwa kazi ya hizi ni huharakisha tu kupona.

4.Kama mtu atakosa supplement ya vitamin B17 na pangamic acid anaweza tu kula mbegu zenyewe za apricot,anaweza kuanza na mbegu 7 kwa siku na aendelee kuongeza idadi hadi kufikia 26 kwa siku,kila siku.Nasema hivyo kwasababu supplement ya vitamin B17 na pangamic acid hazipatikani hapa kwetu kirahisi na uingizwaji wake unaweza kuwa na matatizo kutokana na chemical compound iliyomo ndani yake.Chemical compound yake ni sababu tosha ya kupigwa marufuku na TFDA kwa kuwa TFDA wanafanya kazi kwa kufuata protocols na si mantiki.TFDA wakishaona cynide component ndani yake huweza kuipiga marufuku bila hata kujiuliza sayansi ya ufanyaji kazi wake.

Kazi kwenu sasa,someni kwa makini huku mkirudia rudia mpaka huu mtiririko ukae kichwani na muwe madaktari wenu na watu wenu wa karibu.Kama kuna swali hapa mnaweza kuuliza,au kama kuna kitu sijakizungumzia mnaweza kukumbusha.
Sorry nilichelewa ila lazima niseme.
Hii imekaa vizuri sana.
 
Hao jamaa wanatengeneza hizo dawa mbili, Vidatox na Cimavax, hata kabla ya kuwa na uhusianao mzuri na USA, sasa hivi hata USA wenyewe ndiyo wanazinyemelea na baadaye zikiingia mkononi mwao basi itakuwa bei zake hazishikiki, maana wao wanataka kufanya hiyo iwe biashara lakini wenzao wa cuba wanaziuza kwa bei ya chini ili kuwasaidia binaadamu. ONYO! kuna makampuni mengi tu ya eastern europe na china na India wanadai wao wamepewa kibali cha kutengeneza dawa hizo, akili kichwani mwako, hizo zinatoka cuba tu. mkizihitaji ni pm niwape mchongo wa wapi unaweza kuzipata.
 
Ukweli ni kuwa ukishapata mgonjwa wengi wa nategemea afe mf kwenye ukoo wetu upande wa baba cancer imekaa km ni kitu wanarithi maana waliotangulia mbele za haki wote ni cancer imewachukua, sasa baba yangu amekuwa akipima every year na majibu yalikuwa yanakuja kuwa hana cancer until last year ndo cancer ilionekana around mwezi wa nane, mahospitali ya hapa bongo alikuwa akienda ku some wa result wanamwambia bado ni stage ndogo asiogope atapata dawa but he chose kutibiwa nje ya nchi, amefika huko a naambiwa ni stage 4 na siku anasafiri ndo alianza kusikia maumivu, imagine madaktari wa hapa ambao ni marafiki zake ndo wanamwambia asihofu! Alipewa chemo ila bahati nzuri mama aliambiwa kuh blackstrap molases na bicarbonate of soda, warm lemon water, juice za mboga and no water added na in alipo rudi mara ya pili a kaambiwa cancer cells zinapotea haraka, na pia alipo rudi mara ya tatu a kaambiwa hana kabisa cancer cells na mpaka sasa anakula hivo vyakula na amepima tena jana kaambiwa yuko normal jamani cancer inatibika, tunachowish ni kuwa tungejua mapema hata chemo as inge pata, alinyonyoka nywele but zimeota haraka huwezi hata kujua km zilinyonyoka, sasa hivi mama anawafanyia consultation wagonjwa wa cancer on foods maana yy alisomaga nutrition so ameaamua kuagiza hizo blackdtrap na anaziuza maana hapa nchi ni tulitafuta hazikupatikana na pia anawatengenezea wagonjwa vyakula na wheat grass juice pia anapanda majani na zengine kwa wanao afford ku nunua ile imported ya powder form anawauzia! Tumeresort kuwa chakula anachokula mgonjwa ni tiba haswa! So Deception anapaswa kushukuriwa maana mtu akiamua kupatilizq ushauri wake atakuja hapa kusema kuwa hata mgonjwa kaamka kitandani there is cure in foods


Poleni sana Mkuu napoteza. I hope now mzee anaendelea vyema.

-Kaveli-
 
Hao jamaa wanatengeneza hizo dawa mbili, Vidatox na Cimavax, hata kabla ya kuwa na uhusianao mzuri na USA, sasa hivi hata USA wenyewe ndiyo wanazinyemelea na baadaye zikiingia mkononi mwao basi itakuwa bei zake hazishikiki, maana wao wanataka kufanya hiyo iwe biashara lakini wenzao wa cuba wanaziuza kwa bei ya chini ili kuwasaidia binaadamu. ONYO! kuna makampuni mengi tu ya eastern europe na china na India wanadai wao wamepewa kibali cha kutengeneza dawa hizo, akili kichwani mwako, hizo zinatoka cuba tu. mkizihitaji ni pm niwape mchongo wa wapi unaweza kuzipata.
mkuu hizi dawa bado zipo
 
mkuu hizi dawa bado zipo
Hizo dawa zipo mkuu, kwa sasa zipo kama vichupa 2 vya vidatox ambavyo vina xpire mwakani.Ila uelewe kitu kimoja, dawa hizi hazitibu kensa ambayo imechafikia stage ya mwisho, huwa zinasaidia sana wakati maradhi yanaanza na kufanya zisinyae na siziendelee kutapakaa. Sasa sisi huwa tunakosea na tunakuwa desperate pale tunapoambiwa mtu wetu ana maradhi hayo, ambayo kwa kweli ni mabaya, bila ya kujua ni stage gani anayo, nina maana wakati mwingine huwa tunapoteza fedha bila sababu.Ni ushauri wangu huo tu mkuu. Ila dawa hizo zipo.
 
Cannabis oil/Hemp oil huwa kuna watu wanaifanya kama biashara kwa kuitengeneza wao wenyewe kama Rick Simpson alivyoelekeza.Lakini kwa hapa kwetu hamna watu hao.Wengi wapo Canada,Mexico na Marekani na huwa hawaruhusiwi kuuza nje ya nchi zao(unaona utata huo?),mimi nilishawahi kuulizia kampuni moja Canada ili ninunue lakini walisema hawauzi nje ya nchi kwa kuwa sheria zao haziruhusu,baada ya kuwabana sana wakasema hawatengenezi hemp oil.Mimi nilijua kwamba hawaruhusiwi kuuza nje ya nchi lakini niliuliza kwa makusudi ili kupata uhakika kwa maana nilikuwa katika utafiti tu.Mimi mwenyewe najua jinsi ya kutengeneza.Yaani kama ningekuwa mfanya biashara kwenye tiba kama baadhi ya watu walivyodhani,basi mimi ndio ningekuwa naongoza kwa kuuza dawa zenye uhakika wa kutibu magonjwa yote sugu kuliko watu wote hapa Tanzania.

Sasa kwenye moja ya reply zangu nimeweka link ambayo nimeandika jina la RUN FROM THE CURE/RICK SIMPSON,link hii ni documentary ambayo mwishoni Rick Simpson mwenyewe anaonesha jinsi ya kutengeneza Hemp Oil/Cannabis oil kutoka kwenye bangi/cannabis,ni rahisi sana ukifuatilia na kila mtu anaweza kutengeneza mwenyewe nyumbani.Fuatilia hiyo documentary utaelewa tu.Watu wanaona haya mambo kama miujiza lakini ni kweli kabisa na hii ni kwasababu tumedanganywa kwa muda mrefu ndio maana inakuwa vigumu kwa watu kuamini,wewe fanya mwenyewe kwa kuwa kuona ndio kuamini,usisikilize watu wanaopinga bila sababu za msingi.FANYA MWENYEWE,UTAJUA TU.Kama huoni faida utakuja kuniambia hapahapa na wengine wathibitishe,haya mambo sio blaa blaa,hii ni sayansi.



Yaani mkuu hapa ndio napata homa nikiwaza hili.Hata wale wababe wenyewe waliotushinikiza tufuate sheria hii kwamba bangi ni haramu,wameshaitoa bangi kutoka schedule I drug kwenda schedule II drug ambapo bangi sasa imethibitishwa kuwa na medicinal value.Lakini hii dunia yetu huku kwetu ni dunia ya giza,hao 'miungu' waliotuaminisha kwamba bangi haramu kwa kuiweka kwenye schedule I drug wamebadilika tayari lakini sisi wafuasi bado tuko kulekule,yaani hizi ndio akili mgando ninazozilalamikia kila siku.Bado hata leo hii mtu akikamatwa na bangi ni jela tu bila kujali alitaka kuitumiaje hiyo bangi.Polisi wajinga,wanasheria wajinga,mahakama wajinga na hadi viongozi wa serikali pia ni wajinga,wote ni wajinga,sasa katika nchi kama hiyo unafikiri nani atamwokoa mwenzake?

Hebu chukua mfano mmoja rahisi sana;Panadol ni dawa inayotumika kutuliza maumivu ya kichwa nk,ukimeza panadol kichwa au homa inatulia,hivyo panadol ni muhimu sana kwa matumizi ya binadamu.Lakini ikitokea mtu mmoja kachukua panadol tembe 50 akameza kwa pamoja atakufa tu,sasa je,kufa kwa huyu mtu kwa kumeza panadol tembe 50 inaweza kuwa sababu ya kuifanya panadol iwe haramu na isiruhusiwe kutengenezwa na hata kuuzwa hata madukani?Najua kila mtu atasema hapana,na huo ndio ukweli.Hili liko wazi kwamba uharamu wa kitu uko kwenye matumizi yake.Lakini je,kwa nini mpaka leo hii serikali yetu ni wajinga hivyo kiasi cha kumfunga mtu yeyote atakayekamatwa na bangi bila kujali anataka kuitumia bangi kwenye matumizi gani?
Hapa ndipo utakapoona kwamba ujinga ni kitu kibaya sana na hasa pale ambapo mtu atashindwa kugundua kwamba yeye ni mjinga kwa kuwa kila kitu kipya hakitamwingia akilini hata kama kina mantiki.Ukiwa unajua kujieleza vizuri mahakamani huwezi kufungwa hata kama wamekukamata na bangi tani 20,kwa kuwa sheria zao wenyewe zinawabana.Kwa hiyo mkuu sisi bado tuko gizani na bado sijui tutauona mwanga lini.Wewe kwa sasa nitakachokushauri ni kutumia elimu hii kwa manufaa yako na watu wako wa karibu.
Sasa Mkuu Deception, Bob Marley alikuwa ni mvutaji mkuu wa bangi, mbona alikufa kwa cancer?
ina maana bangi haikuweza kumsaidia?
Haya matunda yanapatikana sana kule Mbeya kwa wingi, kumbe apricot ni hizi, ni jamii ya mapera Mungu ashukuriwe ni vitu ambavyo vipo karibu sema hatujui matumizi yake!
 
Sasa Mkuu Deception, Bob Marley alikuwa ni mvutaji mkuu wa bangi, mbona alikufa kwa cancer?
ina maana bangi haikuweza kumsaidia?

umeshasema alikuwa mvutaji wa bangi,mimi sizungumzii kuvuta bali nazungumzia kula,tena si kula tu kwa jinsi yoyote atakavyo mtu,bali kula/kunywa chlorophyll ya bangi.Chlorophyll ya bangi ikiingia kwenye damu ndio inakuwa dawa,sasa ukivuta bangi haiwezi kuingia kwenye damu yako,na pia moshi sio chlorophyll,simple and clear.

Halafu pia,masuala kama haya ya kuwatumia watu maarufu ku justify kwamba cancer haina tiba ni hoja za baadhi ya watu ambao wengi wao hawana uelewa wa kutosha kuhusu masuala haya.Wewe umemtumia Bob Marley,lakini wapo waliomtumia Steve Jobs,lakini wote hawa wana sababu zinazofahamika kwanini walikufa kwa cancer,lakini watu wengi hawajui kwa undani kuhusu vifo vya watu hawa wawili.

Labda nikupe homework moja kuhusu Bob.Fuatilia utafahamu kwamba kifo cha Bob kilihusishwa na ugomvi wake na CIA...CIA ndio walihusika....sasa fuatilia mwenyewe vizuri.
 
umeshasema alikuwa mvutaji wa bangi,mimi sizungumzii kuvuta bali nazungumzia kula,tena si kula tu kwa jinsi yoyote atakavyo mtu,bali kula/kunywa chlorophyll ya bangi.Chlorophyll ya bangi ikiingia kwenye damu ndio inakuwa dawa,sasa ukivuta bangi haiwezi kuingia kwenye damu yako,na pia moshi sio chlorophyll,simple and clear.

Halafu pia,masuala kama haya ya kuwatumia watu maarufu ku justify kwamba cancer haina tiba ni hoja za baadhi ya watu ambao wengi wao hawana uelewa wa kutosha kuhusu masuala haya.Wewe umemtumia Bob Marley,lakini wapo waliomtumia Steve Jobs,lakini wote hawa wana sababu zinazofahamika kwanini walikufa kwa cancer,lakini watu wengi hawajui kwa undani kuhusu vifo vya watu hawa wawili.

Labda nikupe homework moja kuhusu Bob.Fuatilia utafahamu kwamba kifo cha Bob kilihusishwa na ugomvi wake na CIA...CIA ndio walihusika....sasa fuatilia mwenyewe vizuri.
Nakushukuru mkuu hapo sasa nimekuelewa, kumbe uzuri wa bangi sio kuivuta kama sigara bali ni kuitumia ikiwa natural kama mboga, ahsante umenipa pia homework.
 
Sina uhakika kwa kiswahili linaitwaje,lakini ni tunda linalofanana kabisa na apple/tufaa ukiliangalia kwa nje ila tofauti yake kwa ndani lina mbegu moja kubwa kiasi katikati tofauti na tufaa lenye mbegu kadhaa ndogondogo.Ile mbegu yake ukiimenya na kuila ina ladha chungu sana,sasa ule uchungu ndio kimelea kiitwacho amygdalin ambacho ndio tiba yenyewe inayotumika kuua chembe za cancer.
ukiweza utuwekee hata picha kama unayo
 
Back
Top Bottom