Sasa tuzungumzie cannabis/bangi;
Kama kawaida inabidi mkumbuke kwamba ili uwe na uhakika wa kupona cancer lazima upitie hatua zote tatu,yaani,kuweka damu ya mgonjwa iwe alkaline,kuondoa sumu mwilini na ya tatu kuua chembe za cancer.Kwenye hatua zote mbili nina uhakika wote mnazijua vyema.Sasa kwenye hatua hii ya tatu tayari tumeshazungumzia Vitamin B17/Laetrile/Amygdalin,leo nitazungumzia cannabis/bangi.
Hakuna mtu yeyote duniani aliye na uwezo wa kupinga kwamba cannabis inaua chembe za cancer.Cannabis/bangi ilitumika miaka mingi sana kutibu magonjwa mbalimbali ikiwemo cancer,watu wenye nguvu na ubinafsi wamezuia siri hii kwa manufaa yao binafsi.US government yenyewe inajua kwamba cannabis ina uwezo wa kuua chembe za cancer,Ronald Reagan mwenyewe alijua umuhimu wa cannabis/bangi na ndio maana aliwahi kuilima bangi,lakini yeye mwenyewe aliku mstari wa mbele kupinga matumizi ya bangi baada ya kupata shindikizo kutoka kwa wenzake ambao ni wamiliki wa viwanda vya madawa.
Ili cannabis/cannabinoid iwe na nguvu zaidi,inabidi itumiwe kama extract kwa kutumia solvent extraction.Active ingredient/vimelea vinavyohusika kuua chembe za cancer kutoka kwenye bangi ni CANNABIDIOL(CBD) na TETRAHYDROCANNABINOL(THC).Najua kwa watu wengi hiki ni kitu cha kushangaza sana kwa kuwa wanajua na wamesikia kwamba bangi ni haramu.Lakini inabidi mkumbuke kuwa,hata hao wanaosema bangi ni haramu huwa wanasema ni haramu kuvuta tu,sasa kama mwingine anaitumia kukamulia kwenye sikio kuondoa maumivu,je,uharamu wake uko wapi?Wengine wanakula kama mboga,je,ni haramu?wengine wanaitumia kuondoa kichefuchefu,je,ni haramu?Wengine wanatumia mafuta ya mbegu za bangi kulinda ngozi,je,ni haramu?Hata mahospitalini wanatumia dawa kama vile DRONABINOL na NABILONE ambazo zimethibitishwa na FDA ya Marekani ili kuondoa side effects zilizosababishwa na chemotherapy kwa wagonjwa wa cancer,dawa hizi zimetengenezwa kwa kutumia bangi.
Hawa jamaa wanazuia watu kujua matumizi makubwa sana ya bangi likiwemo lile la kutibu cancer na badala yake wanajifanya kukubali kwamba kweli bangi ina faida lakini wanataja faida ndogondogo tu,kubwa hawazitaji na hata wakizitaja watakwambia bado hazijakuwa proved,sasa tangu miaka 130 ya utafiti wa cancer ipite hadi leo hii wanashindwa vipi kutafuta proof?Kitu kingine ambacho hakiingi akilini ni pale wanaporuhusu bangi itumike baadhi ya states zao kama vile California nk na kuzuia states nyingine wasitumie,mshawahi kujiuliza kwa nini waruhusu sehemu moja lakini wazuie sehemu nyingine ilihali bangi ni haramu?Kama kweli bangi ni haramu kwa nini wasizuie sehemu zote tu?Akili kichwani kwako.
Kati ya mambo rahisi sana kujua ukweli wake,bangi ni mojawapo,ukiamua tu kujua ukweli wa bangi wala haipiti wiki moja utakuwa umejua kila kitu.
Sasa kwenye tafiti nyingi sana imebainika bangi ina uwezo wa kuua chembe za cancer,hata US government yenyewe wanakubali kwamba bangi ina uwezo huo,sasa kwa nini hawaruhusu bangi itumike kwa wagonjwa wa cancer?Wanazuia isitumike active ingredient yenyewe ya bangi kwa kiwango kinachotakiwa na badala yake wanasema eti bangi ikitumika pamoja na chemotherapy au mionzi inaongeza uwezo wa tiba hizo mbili kutibu cancer,yaani huu ni uongo mtupu,wanachanganya tiba sahihi na sumu zao za chemo na mionzi wakati bangi peke yake ina uwezo wa kipekee.Sasa wewe mwenyewe fikiria,kama chemo na mionzi yenyewe husababisha madhara/cancer mwilini ukiachilia mbali ugonjwa wenyewe wa cancer halafu wanasea ukitumia bangi bado unapata nafuu,je,hamuoni kwamba kama mtu atatumia akili atagundua kwamba kweli kumbe bangi ina uwezo mkubwa sana?Kwa maana kwa kesi hii bangi itakuwa inapambana na madhara ya chemo na mionzi na wakati huohuo inapambana na cancer yenyewe.
Kuna watu walitumia na wanatumia bangi extract na bado hawapitii hatua ya kwanza na ya pili nilizotaja na bado wanapona,hapa ndipo utakapoona kwamba bangi ni suala lingine kabisa.Hawa jamaa kuizuia ili kulinda maslahi yao hawajakosea kabisa.Huko Marekani kuna watu wameshafunguka akili na kujua umuhimu wa bangi na ndio maana maandamano ya kutaka bangi iruhusiwe marekani ni jambo la kawaida sana,lakini kwa nchi zilizo gizani kama zetu hizi huwa wanacheka na kushangaa eti wanaposikia watu wanaandamana kutaka bangi iruhusiwe,ama kweli ujinga ni kitu kibaya sana,wakati tunawacheka wenzetu wakati huohuo wenzetu nao wanatucheka sisi na kweli wao ndio wana haki ya kutucheka.
Ili kujua jinsi ya kupata extract kutoka kwenye bangi na mambo mengine muhimu nitawakea documentary hapo chini kwa kumbukumbuku zenu.Rick Simpson ni mmoja wa watu wanaopigania bangi US Canada,anaelimisha watu bure bila kudai pesa,anafanya hivyo kwa kuwa yeye mwenyewe ndugu zake ni wahanga wa cancer kabla hajajua ukweli huu wa bangi,pia yeye mwenyewe ni shuhuda baada ya kujitibu cancer ya ngozi kwa kutumia bangi.Kama mtu anatoa uelewa huu bure bila kudai fedha,je, watu hawaoni kama kuna ukweli hapo?
Pia wewemwenye unaweza kufuatilia kwenye mitandao mingine kuhusu bangi na cancer,yaani ukweli huu haufichiki,karibu kila site utakayoingia lazima itaonesha kwa namna moja ama nyingine kwamba bangi inaua chembe za cancer.Hata wenyewe wanakubali angalau huwa wanasema kwamba bangi inaua aina fulani ya cancer tu badala ya kusema kwamba inaua chembe za cancer yoyote.Sasa wakati wao wanaendelea kujifanya wanafanya utafiti kuhusu bangi huku wale wanaojua ukweli tayari wanatumia bangi kujitibu.Hawa jamaa hawawezi kumaliza utafiti huu leo wala kesho,miaka 130 sasa imepita bado hawajui.Sasa hata sisi tukijua ukweli huu tutakuwa tunatumia bangi kujitibu cancer wakati wao wanaendelea na utafiti,washenzi sana hawa watu.
Pitia wenyewe kwenye mitandao ujionee,au unaweza kuperuzi hizi baadhi ingawa nazo zimeficha baadhi ya mambo;
Federal Government Finally Admits Cannabis Can Help Kill Cancer Cells
Marijuana can kill cancer cells, says US government-funded research - Americas - World - The Independent
'Major hypocrisy': US govt-funded agency admits marijuana can kill cancer cells ? RT USA
The US Finally Admits Cannabis Kills Cancer Cells | Collective-Evolution
Cannabis kills cancer cells and shrinks brain tumours, report reveals | Daily Mail Online
Cannabis and Cannabinoids - National Cancer Institute
RUN FROM THE CURE/RICK SIMPSON;