Highest government debt as share of GDP, 2020

Zaidi ya nusu ya nchi ulizozitaja hapo nazo zinatukopesha.

Sasa sisi tunadaiwa na nani? na wao wanadaiwa na nani?.

Maana ishu hapa sio tumekopa ngapi na kina nani wamekopa zaidi, ishu ni Je,Mkopaji akitaka pesa zake tuna kifua hichohicho alichonacho France na Japan?.
 
Sawa boss
 
Sawa boss
Ndio boss, yani ni kheri wahoji viongozi wengine na wanachi ila sio Ndugai maana yeye ndio alikuwa anawazuia kina Zitto kuhoji/kuongelea ongezeko la deni la taifa ndani ya Bunge lake alafu leo hii ndo anajitokeza kulalamika, hajawahi kuwa na uchungu na Tanzania yule mchumia Tumbo
 
Chief kama nadhani umeshawahi kudaiwa kwenye maisha yako, je wakati unadaiwa ulikuwa husaidii wengine? Kwamba ilikuwa kila watu wakikuomba msaada wewe unasema unadaiwa? Ok then tajiri haruhusiwi kukopa? Unadhani WB or IMF wapo kwa ajili ya kuokoa jahazi la nchi maskini pekee? Hawakopeshi nchi tajiri? Kwa hizo percentage hapo juu sisi tunakifua kikubwa kulipa deni letu kuliko hao France na Japan, kwa sababu relatively (and ukilinganisha na GDP yetu) deni letu ni dogo na linalipika kuliko wao
 
Baba wa taifa mwl JK Nyerere aliwahi kusema kuwa upinzani wa kweli wa kuiondoa ccm madarakani utatoka ndani ya ccm.

Kwa hali ilivyo kwa sasa ni dhahiri ccm inaweza ikawa na mimba ya kuzaa chama kipya cha upinzani.
 
Wacha ukichaa asubuhi yote hii.
Yaani unajilinganisha na Japan?
 
Baba wa taifa mwl JK Nyerere aliwahi kusema kuwa upinzani wa kweli wa kuiondoa ccm madarakani utatoka ndani ya ccm.

Kwa hali ilivyo kwa sasa ni dhahiri ccm inaweza ikawa na mimba ya kuzaa chama kipya cha upinzani.
Obvious iko hivo mkuu, ila miongoni mwa hao watakaofanya hiyo U-turn bila shaka Ndugai hawezi kuwa miongoni mwao, huyu mzee always anajali maslahi yake tu, hadi kufika hatua ya kuanza kuongea hivi basi trust me brother kuna ulaji uliokuwepo kwake na haupo tena
 
Tumuombee ule ugonjwa wake uliosababisha akatumia 26billion pale kwa ponjoro usimrudie maana ataozea hapa hapa
 
hizo data za uongo
 
Pale Maskini anapojifariji na Bakuli lake mkononi
 
Ukilinganisha miaka mitano ya Magufuli na miaka mitano ya mwisho ya Kikwete , Miaka mitano ya mwisho ya Kikwete alikopa zaidi kuliko Magufuli.
 
Hapo Kuna uwezekano mkubwa wa hao wanaodaiwa kutupiga cha juu
 
Na Hapa ndio fikra zetu zilipoishia ?

Tumeshindwa kutumia vyanzo vyetu (na vyanzo simaanishi wananchi na kukamuliwa kodi) bali resources tulizonazo, madini, gesi, utalii n.k....

Hio baada ya miaka 20 kulipa tatukuwa tunazalisha nini cha kuweza kulipa kwa urahisi iwapo miaka 60 sasa hata wale maadui wetu watatu bado wapo (kwanza ndio wameongezeka nguvu)
 
Haters wa JPM baada ya kuona mama ametetea kukopa sasa wamepiga uturn kuwa tatizo JPM amekopa sana kwenye commercial bank! Purely tabia za kichawi yaani!
 
Kukopa huku unamiliki zizi la ng'ombe ni matumizi mabaya ya akili
 
Ukilinganisha miaka mitano ya Magufuli na miaka mitano ya mwisho ya Kikwete , Miaka mitano ya mwisho ya Kikwete alikopa zaidi kuliko Magufuli.
Inawezekana uko sahihi Mkuu bahati mbaya me sina figure za muhula wa mwisho wa jakaya, ila tutalinganisha vipi miaka 5 ya jakaya ambayo yeye aliitumikia na miaka 5 ya mwisho ya Hayati Magufuri ilhali ye hajaimaliza miaka ya mwisho

huwezi jua labda Hayati angekopa kuliko jakaya, na kwa kawaida muhula wa mwisho lazima wakope zaidi maana waga kuna miradi mingi ambayo inakuwa ndani ya budget na haijakamilika, hivo wanakopa at least kuacha imefika mbali au kumalizia kabisa

kwa muhula wa kwanza wa Hayati Magufuri hadi Dec 2020 alikuwa kakopa jumla ya trillion 18,kama hutojali unaweza nijuza katika muhula wa mwisho wa Jakaya yeye alikopa kiasi gani cha pesa ili tujaribu kufanya comparison katika hoja yako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…