Roboti Wa Nape
JF-Expert Member
- Nov 20, 2023
- 1,174
- 2,876
Leo nimeenda kumtembelea jamaa yangu mmoja anaishi sehemu moja inaitwa Kilolo Mkoa wa Iringa.
Huyu ni mate wangu, nilisoma naye chuo kikuu anafanya kazi huku ni Afisa fulani.
Wazee hii baridi sio mchezo. Kesho nitaikimbia na kurudi kwangu Dar. Sijui wanaishije hawa watu. Yaani nimeingia jioni hii hapa kwake, kesho saa 7 naondoka niwaachie na taabu yao.
Ona hiyo Temperature inavyosoma.
Hapa wameniwashia moto niote na shem ananiambia nikaoge. Hahaha hata kama maji ya moto, leo siogi.
Wenyewe wanasema sasa ndio kipindi cha joto kwani wanakaribia msimu wa kuanza kwa mvua. 😀😀😀😀
Kipindi cha baridi ni kuanzia mwezi 2 hadi mwezi Septemba na peak huwa mwezi Juni hadi Agosti.😀😀😀
Kumbe ndio maana tunasikia watu wamefia ndani kwa kukosa hewa kwani wanapaswa mikoa na carbon monoxide inawaua.