SI KWELI PreGE2025 Hii barua ni ya mchakato wa ugombea Urais imetolewa na CCM

SI KWELI PreGE2025 Hii barua ni ya mchakato wa ugombea Urais imetolewa na CCM

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
CCM Urais. July 20, 025.jpg
 
Tunachokijua
Madai

Ipo barua inayosambazwaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii inayodaiwa kutolewa Julai 20, 2025 na Chama cha Mapinduzi (CCM) ikieleza kuwa mchakato wa kumpata mgombea wa Urais kwa tiketi ya chama hicho utarudiwa.

Uhalisia wa Taaarifa hiyo

JamiiCheck imefuatilia taarifa hiyo na kubaini kuwa haijatolewa na Chama cha Mapinduzi (CCM).

Kupitia kurasa zao rasmi za mitandao ya kijamii CCM hawajachapisha taarifa hiyo kwa Umma kama ilivyo utaratibu wao ambapo wamekuwa wakichapisha taarifa zao katika mitandao hiyo ya kijamii.

Ufuatiliaji umebaini kuwa taarifa ama barua hiyo ni ya kughushi kutoka kwenye taarifa iliyotolewa Juni 8, 2025 ambapo CCM walitoa taarifa kuonesha masikitiko yao kutokana na vifu vya watu 28 kilichotokea Juni 7, 2025 huko Iwambi Mbeya (Scan QR Code iliyopo kwenye barua).

Julai 19, 2025 Katibu wa halmashauri kuu ya CCM Taifa, Itikadi Uenezi na Mafunzo Amos Makalla alifanya mkutanona waandishi wa habari na kueleza kusogezwa mbele kwa mchakato wa uteuzi wa ugombea ngazi ya ubunge na udiwani na hakugusia suala lolote kuhusiana na jambo la Urais.

Aidha taarifa hiyo kwa Umma licha ya kughushiwa kutoka kwenye taarifa ya Juni 8, 2025 lakini pia imetumia aina tofauti ya mwandiko (font) na unaotumiwa na chama hicho kwenye taarifa zao.
Sio lazima uwe na akili timamu kuelewa hilo, kila mtu ni kuzusha upumbavu tuu
 
We need to verify this first before being spread to social media
 
Barua ya kuhairisha mkutano haikuwa na QR-code (umeita bar code) kabisa na ilikuwa authentic.
JF ina watu wenye akili jaman tusiwe mazezetq, hiyo barua ina bar code, ukiscan hapo inaonssha barua ya kutoa pole vifo vya ajali
 
Back
Top Bottom