Hii bei ya mafuta wiki chache zijazo tutaiona ni bei ndogo

Hii bei ya mafuta wiki chache zijazo tutaiona ni bei ndogo

chai ya rangi

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2026
Posts
1,042
Reaction score
3,095
Leo nimepita nimekuta wese linasima 3820, nikashangaa sana nikaamua tu nijaze full tank, kwasababu najua baada ya muda huenda yatafika 5700, kama hali itaendelea kua mbaya baada ya muda tutakutana na 6500 kisha hii bei ya leo itaanza kuonekana ilikua mteremko sana.

chakuomba ni kwamba watu wasianze kuficha mafuta, na wauze bei ya fair bila kutafuta faida kubwa, nawe kama utapenda leo nenda kajaze full tank, lakini na wakati huohuo mafuta yakiwa juu kwa muda mrefu, bidhaa mbalimbali tunategemea zitafuata kupanda bei
 
Sisiem sio wa kuwaamini
IMG_9571.jpeg
 
Nakumbuka mwaka 2020 Lita moja ya Petrol ilikuwa 2,100.

Corona ikatingisha. Ikaanza kupanda kidogo kidogo hadi kufikia Climax ya 3,300...

Na hata baada ya Corona bei haikurudi ile 2,100. Ikakomea 2,700/=.

Je hii vita ikiisha unafikiri itarud 2,700 lowest price tuliyozoea?.au itakomea 3,500+ 😭😭😭😭

Hata kama hujui Uchumi. Utaelewa ni kwa namna gani Sera ,Siasa, Vita za nchi tunazozitegemea zinavyoathiri Maisha yetu.

Na pia tuweke akilini kuwa kuna nchi nying hii Bei ya Mafuta haiwahusu. Wanajitosheleza.

Afrika haiwez kuwa Huru Bila kuwa na Malighafi zake.
 
Uchunguzi ufanyike,iweze ghafla bei ya mafuta itokee tarehe 1/04/2026.

Nchi jirani viongozi wanaosimamia sekta hii wamejiuzulu,baada ya kuwepo tuhuma za kula njama,kupandisha bei kwa kusingizia kuwa mzigo mpya(shehena ya mafuta) umekuja kwa gharama kubwa.

Tanzania,inasemekana shehena ya mafuta iliyokuwepo(Stock) haikupaswa kupandishwa bei.

Yawezekana njama ipo,ndio maana baadhi ya uuzaji walisita kuuza mafuta yao wakisubiri bei mpya.

Suala hili lisipofuatiliwa kwa umakini,Serikali itajikuta imeshondwa kudhibiti mfumuko wa bei kwa kila sekta.

Bahati mbaya mwaka wa fedha ujao 2026/2027,misaada na ufadhili kutoka nchi wahisani inaenda kupungua au kusitishwa.

Serikali icheze karata yake sasa(Kulinda umaarufu wa Serikali kwa wananchi)!!!,

Serikali Ichunguze sababu na idhibiti upandishwa wa bei ya mafuta kwa kiwango ambacho kinaenda kuathiri sekta ya usafirishaji na hatimaye mfumuko wa bei kila Sekta.
 
Back
Top Bottom