Hii biashara inanipa stress wallah!

Anzisha kijiwe cha kuuza juice ya miwa. Tafuta location nzuri piga kazi.
 
Jaribu kuwasiliana na Wizara ya ajira na vijana(Mavunde) /Wizara ya kilimo na mifugo wanaweza kukusaidia kwa kiwango fulani kukulink na masoko hata kama siyo to the fullest.
 
Ingekuwa ni miwa ya kienyeji hakuna tatizo la kuharibika, lakini umefanya kosa ndogo, wakati mwingine unavyoleta bidhaa yako kwa mara ya kwanza kwenye soko jitahidi ulete kiasi kidogo hata tani 3, ungeleta na gari canter wala usingelia lia. Soko unatakiwa ujaribu likisoma positive unaongeza kidogo kidogo.
USHAURI:
  1. Kama unaweza kukamu juice na kutunza kwenye freezer alafu unawauzia wauzaji wa juice kwa bei ya jumla
  2. Jaribu kuhifadhi kwenye sehemu ya baridi ukinyweshea maji lakini hiii inategemea jinsi ulivyokata shambani
  3. Watafute waaminifu uwakopeshe lakini hii ni risk pia
Best wishes!
 

Miwa inayozalishwa na hayo mashamba ya viwanda bado haitoshelezi na ndo mana wanaingiaga mikataba na wakukima wa nje. huu uhaba wa sukari unaotokeaga ni ishara kubwa kwamba miwa inayozalishwa haitoshelezi.
 
[emoji106][emoji106][emoji106]
 
Mkuu pole sana ila ushauri wangu ambao nilishawahi kushuhudia, ni kwamba nunua manual machine ya kukamua miwa 450k uifunge shambani uanze kukamua hiyo miwa kutumia cheap lbr (4) 5000@ kwa siku,

uwanze kuichemsha kwa kutumia hayo magada ya miwa itaganda baada ntakuelekeza chemical( endiony) 50k moja ili isafishe iwenyeupe arafu uisange kuna manual machine vya kusagia inakua sukali nzuri lakini sio high quality

ununue mifiko ya sukali ya kagera suger au mtibwa uchanganye mufuko moja kwenye mifuko 10 ya kwako kisha pakie upeleke sokoni.....unalipwa keshi hela yako hapo hapo inarudi ndoanze paper work ya small scale industry

hiyo ni kazi nzuri ila fitina nyingi kutoka serikalini na wawekezaji kwa kisingizio cha kiwanda bubu, Tbs TRA nk.. ndani ya mwaka unakua mbali sanaaaa
 
miwa inayozalishwa na hayo mashamba ya viwanda bado haitoshelezi na ndo mana wanaingiaga mikataba na wakukima wa nje. huu uhaba wa sukari unaotokeaga ni ishara kubwa kwamba miwa inayozalishwa haitoshelezi.
Ushahidi uliopo sasa hivi wa viwanda kukataa kununua miwa ya wakulima unaonyesha kuwa miwa inayolimwa na viwanda vya sukari huwa inawatosheleza!
 
Ushahidi uliopo sasa hivi wa viwanda kukataa kununua miwa ya wakulima unaonyesha kuwa miwa inayolimwa na viwanda vya sukari huwa inawatosheleza!
viwanda vya sukari vnajitoshelezaje angali kuna malalamiko sukari iliyopo haitoshi? kuna sehemu kuna kauongo.
 
viwanda vya sukari vnajitoshelezaje angali kuna malalamiko sukari iliyopo haitoshi? kuna sehemu kuna kauongo.
Sukari kutokutosha haitokani tu na ishu ya miwa bali kuna sababu nyingine zinazoweza kusababisha tatizo hilo kama vile uwezo wa viwanda kuzalisha sukari,management mbovu,sera mbovu za serekali juu ya usambazaji wa sukari na kadhalika
 
Pole mkuu, juice ya miwa inanyweka sana kufuatana na hali ya hewa, sasa miwa umeitoa kukiwa na hali ya kipupwe, hata biashara zingine za vinywaji kama maji na soda hazitoki sana..

Hope utapata usaidizi...Pole SANA

Everyday is Saturday........................ 😎
 
Pole sana mkuu.
Hiki mi kipindi kibaya sana.
Biashara ya juice ya miwa haitembei kabisa sababu ya baridi.

Hata vijiwe vya juice hiyo vinachelewa kabisa kufunguliwa na mauzo yameshuka.

Kwa sasa hesabu maumivu na ada ya dogo tafuta plan b.

Kuna ushauri hapo umepewa unaweza ifanyia kazi ya kutengeneza sukari.

Komaa hivo hivo kuwa na kakiwanda kako kisirisiri.
 
Sukari kutokutosha haitokani tu na ishu ya miwa bali kuna sababu nyingine zinazoweza kusababisha tatizo hilo kama vile uwezo wa viwanda kuzalisha sukari,management mbovu,sera mbovu za serekali juu ya usambazaji wa sukari na kadhalika
Naona haukosi sababu chief. anyway point yako imeeleweka na point yangu imeeleweka. Amani.
 
Nenda soko la Tandale
 
Yaani boss hapo ilibdi utafute wewe kijishehemu chako Cha kuuzia hii juice Hasa kariakoo pale hata ungepata vimkokoteni vya kusukuma vya kisasa ingekuwa poa sana

Tuwe tunawaza Mambo mbadala aisee sio kuahikira Jambo moja tu

Don't put all your eggs in one bucket .think aloud

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona Dar kubwa sana?,tembelea vijiwe vya hiyo juice,,naamini kwa dar yote wanaweza kuwa na zaidi ya vijiwe 10,wape sample kisha waachie namba na uwape bei ya chini kidogo
 
Sukari kutokutosha haitokani tu na ishu ya miwa bali kuna sababu nyingine zinazoweza kusababisha tatizo hilo kama vile uwezo wa viwanda kuzalisha sukari,management mbovu,sera mbovu za serekali juu ya usambazaji wa sukari na kadhalika
Hata kampuni nayo inaweza kutoa false information kuhusu scarcity ya bidhaa zake ili ipandishe bei makusudi pale wanapotaka wafikie malengo flani financially.
 
Hebu boss njoo utueleze hiyo chemical mbona juu juu tu umeeleza
 
Mkuu DSM kuna wauza juice wengi sana kama umemaliza tani 3 kwa watu hao hizo 7 zinaisha.

Anza kuwafata Kariakoo pale ndio wengi, makumbusho, mwenge, tandika, temeke, mbagala, mbezi mwisho, gongo la mboto na maeneo mengine ya balabala...kwa idadi wako wengi hizo tank zako 7 zinaenda siku moja tu then tuna Push na zile tani 100 za shambani kwanini mzigo uoze Cheaf.

Nenda na Sample akielewa muuzie kwa Affordable price na asiye na pesa mkopeshe mzigo.

Weka mzigo mezani tufunge Deal hilo chapuuu kijana wa Sales nipo hapaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…