Hii biashara inanipa stress wallah!

Hii biashara inanipa stress wallah!

Mkuu DSM kuna wauza juice wengi sana kama umemaliza tani 3 kwa watu hao hizo 7 zinaisha.

Anza kuwafata Kariakoo pale ndio wengi, makumbusho, mwenge, tandika, temeke, mbagala, mbezi mwisho, gongo la mboto na maeneo mengine ya balabala...kwa idadi wako wengi hizo tank zako 7 zinaenda siku moja tu then tuna Push na zile tani 100 za shambani kwanini mzigo uoze Cheaf.

Nenda na Sample akielewa muuzie kwa Affordable price na asiye na pesa mkopeshe mzigo.

Weka mzigo mezani tufunge Deal hilo chapuuu kijana wa Sales nipo hapaa.
hahahah
naona wengi hatukuona fursa katika hili. hongera sales agent kwa kuwa na akili ya tofauti. ukiishi hivi kila siku utatoboa [emoji1421][emoji1421][emoji1421][emoji1421]
 
Mkuu pole sana!

Ila ungejaribu kuuzia hata wale vijana wanaouza barabara kwenye maguta na baiskel labda ingepunguza mzingo.

Ila tani 10 c mchezo mkuu pambana ziende angalau 3/4 ya mzingo
 
Nimekuwa mkulima wa miwa ya kuzalisha sukari katika Bonde la Kilombero kwa miaka kadhaa sasa ila kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita soko limeyumba kupita kiasi. Tatizo kubwa ni mwekezaji(kiwanda Cha sukari) kushindwa kuhimili wingi wa miwa ya wakulima wa nje (autogrowers).

Kwakuwa ni uwekezaji mkubwa na nguvu nyingi nilielekezea huko ilibidi nitafakari njia mbadala ya kuiuza miwa ile (ukizingatia mimi ni ni mkazi wa Dar, so hata usimamizi wa mauzo kule shamba unakuwa mdogo). Mwanzoni mwa mwezi March nikapata wazo la kuileta Dar kuiuza kwa wanaouza juice ya miwa. Nikaanza kufanya upembuzi wa kutafuta soko kwakuwa miwa ile iko tofauti kidogo kulinganisha na miwa iliyozoeleka kukamua juice hapa mjini.

Ilibidi nilete sample ya bidhaa yangu kwa wateja niliowakusudia, walionyesha kuikubali sababu miwa ile ina sukari zaidi ya hii waliyoizoea. Nikatafuta pia mahali pa kuweka mzigo wangu pindi nitakapoianza hiyo biashara. Baada ya kuona kila kitu kimeenda sawa wakati najiandaa kufuata mzigo ndo balaa la Corona likawa limepamba moto then kukawa na mfungo wa Ramadhan so ikabidi nitulie kidogo.

Baada ya hali kutulia na mfungo kuisha nikafanya safari. Kwa kuanzia nilipanga kuanza na angalau tani10, ili kama biashara itaenda vizuri niongeze ukubwa wa mzigo. Nilifanikiwa kukata na kupakia fuso, Jumapili tarehe 21/6 nikaingiza mzigo Dar.

Balaa lilianza kesho yake Jumatatu nilivyoanza ku-suplly mzigo kwa wateja wangu. Biashara haikuwa kama matarajio niliyokuwa nayo. Hadi leo ninandika thread hii mzigo uko zaid ya tani 7. Mbaya zaidi bidhaa hii baada ya siku 10 haifai tena kwa matumizi kwahiyo nikiangalia uchache wa mzigo ninaoupush per day naona kabisa mzigo hautakwisha na nitapata hasara.

Kinachoniumiza kichwa, matumaini yangu kama biashara ingekuwa vizuri hiyo hela ndo ingenisaidia kumsafirisha first born wangu shule this weekend. Kilichonisukuma kuandika uzi huu wakuu, ni imani yangu kwamba jukwaa hili lina aina zote za watu so kwa yeyote anayefahamu maybe mtu mwenye uzalishaji mkubwa wa Cane juice au popote kwenye kiwanda cha kutengeneza ethanol/spirit ili niiuze hii tani 7 kwa pamoja angalau niokoe gharama za msingi nilizoingia especially usafiri, labour charges etc.

Kwa yeyote mwenye kujua ufumbuzi wa hili jambo nahitaj msaada wake
Mwasiliano: 0624406434
Natanguliza shukrani!
Hivi malighafi zipo za kutosha afu sukari inauzwa juu! Kumbe serikali yetu haiko makini kila siku inasema itafanya watz tuwe na maisha murua. Hayo maisha murua tutayapataje Kama mtu anafanya kazi soko la mazao yake linakuwa siyo la uhakika? Ni wakati wa kufanya maamuz sahihi

Afu wale watu wanaohangaika na democracy kwanini wasihangaike na mambo Kama haya? Ila samahani kwa kuzungumzia siasa sana

Ushauri: Jaribu kuongea hata na wale vijana wanauza miwa ya kumenya barabarani najua ukichanganya na wauza juice mzigo utapungua

Pole sana kamanda
 
Anzisha kijiwe cha kuuza juice ya miwa. Tafuta location nzuri piga kazi.
Hivi mkuu mko serious? Au me ndo nimechukulia picha kubwa!..ni Kama ulime tikiti eka 5 umshaur auze kwa vipande vya 500!..
Unajua kilimo Cha miwa gharama!.then aishie kuwek mashine akamue juice auze 500!!.aisee
 
Jamani tuelewane hapa! Kilimo Cha miwa sio lelemama Kama zao lolote lile..Bora alomshauri atengeneze sukari ! Atkeast ni level yake .lakini juice ya miwa?? Nitekeleze millions of money nije nifungie juic point?
Pole Sana mkuu
 
Back
Top Bottom