Hizo ni chapati za maji?
Nakushauri ingia youtube utakutana na mwanamama Aroma kila aina ya pishi utalikuta kwake, ni vema kuangalia na kufanya kuliko kusoma.
Me pia mapishi mengi nimejifunzia youtube.
Turudi kwa topic yetu, chapati za maji, weka yai/mayai, vitunguu maji, karoti na hoho au kimoja wapo katika hivyo ili kuleta ladha na kukata ile harufu ya yai.
Mchanganyiko wako usiwe mzito sana wala mwepesi sana, size ya kati. hapo utatoa kitu mwake mwake, mafuta weka kiasi sio kama unakomoa, unapakaza tu juu ya chapati sio unamwagia.