Japo sijaiona hiyo habari ya leo kuhusu kukopa na kujenga shule, ila ningependa nikujibu kwa nini Wazungu ni rahisi kutoa misaada, mikopo ya riba nafuu na mikopo ya bila riba katika elimu yetu.
Hii hali ilikuwepo tangu enzi za Kikwete, Wazungu kufadhili elimu yetu.
Nachowaza, Wazungu wameishagundua, Watanzania wengi ni wajinga kwa sababu ya kukosa elimu. Hali hii imepelekea wananchi kufanyiwa mambo ya hovyo, na hawahoji. Hili linawakera Wazungu sana.
Baada ya Wazungu kugundua, tatizo la Watanzania ni kukosa elimu, basi Wazungu wamekuwa wepesi sana kufadhili elimu yetu. Rejea Equip, World Bank, IMF etc.
Wazungu wanaamini, wakifadhili elimu ya Tanzania, basi Watanzania wengi wataelimika na hivyo kileta mabadiliko chanya katika nyanja za kiuchumi, kijamii na kisiasa.
Viongozi wa Tanzania hasa wa CCM wanalijua hili, ila hawana namna kwa sababu wanabanwa na masharti ya mikopo. Viongozi hasa wa CCM wanajua kwamba, anguko la CCM ni pale ambapo Watanzania wengi watapata elimu na kujitambua.
Mama Samia yupo sawa kabisa kukopa na kuboresha elimu, kwa sababu elimi ndio ufunguo wa maisha, ila wale waroho wa madalaka hawapendi kuona Watanzania wanajitambua.
Kwahiyo, tukope tuboreshe elimu yetu, ili baadae tuwe raia wawe majasiri wa kuwakaba mashati viongozi wabadhilifu.
Binafsi napendekeza, tujikite kukopa na kuboresha elimu kwanza kwa gharama yoyote ile.
Mikopo ya kuboresha uchumi huishia kwenye matumbo ya baadhi ya viongozi, lakini mikopo ya kielimu, matokeo tutayaona tu baada ya miaka kadhaa, pale vijana watakapojitambua na kuanza kuwabana viongozi wao.
Sent from my TECNO F1 using
JamiiForums mobile app