Hii Concessional Loan ya miaka 20 ya Rais Samia, mmh!

Acha uongo basi wewe mjamaa...mama ameongelea mkopo wa kujenga reli wa zaidi ya trillion 14 aliosaini leo...kuwa utalipwa ndani ya miaka 20. Hebu niambie leo ameongelea wapi mkopo wa covid wa trillion 1.3?
Reli si ilikuwa ijengwe kwa trilion 7???? Hizo zimeongezekaje??? Maana mi najua sgr trl 7 na stiglas trl 6
 
....Sawa tunalalamika, lakini hoja hupingwa kwa hoja. Je mtoa mada ametupotosha kwa andiko lake? Upi ni usahihi basi?
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] wee lijamaa liongo kweli kweli !! Yaani mazungu haya yanataka waTZ tuelimike na kuwaadabisha mabadhirifu ya CCM na liserikali lao ? Hahahahaaaaa !! Wacha kicheke tuu !!!
Ndivyo ilivyo. Wazungu walishagundua ni ngumu kuitoa CCM madarakani kwa kutumia wapinzani wachache wenye uelewa , wakati Watanzania wengi ni wajinga.

Hii kitu ya vyama vya ukombozi vya Kijamaa Afrika kudumu mpaka leo kikiwemo CCM kwa Tanzania, inawakera sana Wazungu. Wanajiuliza, tatizo ni nini? Wanagundua tatizo ni ukosefu wa elimu hali inayopelekea kushindwa kujitambua, ikizingatia Tanzania ilikuwa ni nchi ya Kijamaa, hivyo juhudi za ziada zinatakiwa kufanyika ili kubadili mindset za Watanzania wengi. Silaha mojawapo ni kufadhili elimu yetu kwa gharama yoyote ile.

Wazungu walishagundua janja ya CCM ya kufuja misaada ya maendeleo, bila kuchukuliwa hatua na wananchi kwa sababu ya ujinga. Ndio maana wapo tayari kutoa hela yoyote katika elimu ili kuleta ukombozi wa kifikra kwa Watananzia.

Rejea enzi za Kikwete, ulikuwa unapewa hela fasta za bure, ukiandika proposal Ulaya ya kuomba hela ili uhamasishe elimu ya uraia.



Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Nani kakuambia mabeberu wanataka mjikomboe? Labda wanataka muweze kuhoji na kuanzisha fujo na baadae vita wauze siraha na sio muendelee
 
..huu mjadala naamini tutafaidika kama Kilatha, Gerald .M Magembe , Chige, watajumuika nasi.
Mada fikirishi, unfortunately sikuwapo around!!

Lakini ngoja nigusie jambo moja kwanza!! Hivi kwanini watu wanaamini na hivi vitozo vyetu ndo basi tena the nation is well-off?! Wala tusiende mbali... Kenya tu hapo kwa majirani!

In 2021 FYI, Kenya Revunue Authority walikusanya almost KES T1.7 Trillion ambayo ni almost TZS 34 Trillion, ambao ni wastani wa TZS 2.8 Trillion kwa mwezi... kiwango ambacho sisi hata kunusa, hatujanusa but still Kenya is a poor country with a lot of challenges!

Lakini nikirudi kwenye mada ya britanicca ambae anahoji kama hao wazungu wanatupenda, kwanini wasituruhusu kumalizia SGR!!

Mkuu Britanicca, kwani Wazungu wametukataza kumalizia SGR yetu?! Au ulimaanisha kutumia hizo TZS 1.3 Trillion kujengea SGR?! Kama ndo ulichomaanisha, HILO HALIWEZEKANI!!

SGR inaweza kusubiri lakini huwezi kusubiri mtoto kwenda shule! Kwahiyo kama COVID-19 imeathiri uchumi wetu, hata mimi ningekusaidia uhakikishe mfumo wa elimu hauathiriki kwa sababu ya COVID-19!

Ningekusaidia uhakikishe mfumo wa afya hauathiriki kutokana na COVID-19!! Kama taifa linaona bora kwake ni SGR na sio shule, basi zile pesa zako mwenyewe ambazo ulitaka kujengea shule zipeleke huko SGR kwa sababu tayari kwenye mashule umeshapata backup! Kama sivyo, nenda kakope kwenye mabenki, au at least kajenge hoja World Bank ukawashawishi ni na namna gani SGR yako itapunguza umaskini nchini kwako!
 
Ndio afya ya taifa, ukiona taifa la watu milioni 60 mawazo yanafanana ujue hilo ni taifa mfu
 
Tanzania tuna laana ya kulalamikia kila jambo utafikiria tumekalia vitu vyenye ncha Kali, ni watu tusio na jema kabisa
Tanzania ni taifa la watu milioni 60, mnataka taifa la watu milioni 60 watu wote wafanane mawazo kama mazombi?! Halafu Watanzania huwa wanalalamika tu sehemu nyingine nyingi huwa wanatoka na kuandamana kabisa.
 
Tanzania ni taifa la watu milioni 60, mnataka taifa la watu milioni 60 watu wote wafanane mawazo kama mazombi?! Halafu Watanzania huwa wanalalamika tu sehemu nyingine nyingi huwa wanatoka na kuandamana kabisa.
Nchi hii hata Yesu akiwa Rais watalalamika tu, kulalamika bila kuchukua hatua ni ujinga huo
 
Ifafanue wewe hiyo pesa ya SGR italipwa vipi unajua miaka 20 ni kipindi kifupi sana. Jiandae kuwa mtumwa acha kuwa bedbugs

Kwahiyo unachotaka ni nini hasa? Kodi haitoshi je reli isijengwe? Wewe hapo ulipo huna mkopo? Kwanini umekopa?
 
Kuwekeza kwenye huduma za jamii, kupitia mikopo, hakuna shaka ni mzigo kwa Taifa. Tuna safari ndefu kupata viongozi wenye maono ya kujitegemea
 
Ukikosoa kwa maslahi ya Taifa unaitwa Sukuma gang.

Haya wezi gan endeleeni kupora.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…