Hii dhana ya kuifungua nchi ni kujidhalilisha: Kwani nchi ilikuwa imefungwa? kuna vitu watu wanasema bila kufikiri!

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
13,897
Reaction score
18,477
Kuna hii dhana ya kumsifia kiongozi fulani eti anaifungua nchi, kitu ambacho hata mwenyewe bila hata yeye mwenyewe anashangaa!!nchi ilifungwaje? nani aliifunga? maana serikali haijabadilika! Ilani ya uchaguzi inayotekelezwa haijabadilika!! Tatizo ni watu kujaribu kujikomba bila aibu!!

Watanzania tufanye kazi! hatuna mjomba kule nje ambako tunatamani kutuma mtu akalie lie hali!! Hakuna wa kutupa vya bure! sana sana mabeberu wanaitamani nchi yetu iliyosheheni maliasili waikombe! Tuwe macho!! Tukatae mikopo yenye masharti ya kutuondolea uhuru wetu juu ya maamuzi muhimu yahusuyo mambo ya kijamii na kiuchumi!! Tuchape kazi, tulipe kodi na Mungu atatusaidia!!
 
Wacha maneno wewe, nchi ilikuwa imefungwa na Magufuli yes kwani kuna ambae hajui? Kila Rais na sera zake na sio dhambi, MAgu sera zake ni kujifungia na kuchukia wenye nacho either wa nje ya nchi au wa ndani, mama Samia sera zake ni kuinua uchumi kupitia uwekezaji kutoka nje ya nchi au ndani mbona simple tu, unalia lia nini sasa?

Ishia hapo hapo kuhusu kusheheni maliasili inayotamaniwa! Hujui kitu bora kaa kimya. Nyie mnasumbuliwa na ubinafsi na siasa mbovu achana na maliasili. Unaijua Dubai? Unaijua Singapore? Unaijua Malaysia? Hawa wana maliasili gani hawa, unaonaje uchumi wao sasa hivi? Si tulikuwa nao sawa hawa miaka ya 1970?

Nchi nyingi sana zina maliasili na zinatuzidi, hatuna kitu kipya duniani wala hatuna cha ziada ila tuna maliasili kama yalivyo mataifa mengine. Jenga hii dhana kichwani kwako uelimike na uache kulaumu watu badala ya kujilaumu mwenyewe kwa kuendekeza siasa badala ya uwajibikaji
 
Kazikwe nae chato pumbavuu

Nchi hii tulishindwa hata kuuza mazao nje ya nchi mazao yakawa yanaozea shamba kwa ajili ya kiburi cha mtu mmoja, sasa hivi hela bwereree kwa wakulima

Uwekezaji kutoka nje ukawa umesimama hadi shilingi yetu ikawa inaporomoka, wafanyabishara wa Bureau de Change wakatupiwa lawama na fedha zao kuporwa
Sasa uwekezaji umepanda mara 20 zaidi na shilingi yetu imekuwa stable tena

KAZIKWE NAE CHATO
 
Waliokuwa na funguo wanafahamu jinsi tulovyokuwa tumefungiwa, wewe uliyekuwa umefungiwa ndani, utijuaje kufuli iliyotumika kukufungia?
 
Na kuna nchi nyingi sana hazina rasilimali na zimetuzidi kwa mbali sana kimaendeleo
Wacha maneno wewe, nchi ilikuwa imefungwa na Magufuli yes kwani kuna ambae hajui? Kila Rais na sera zake na sio dhambi, MAgu sera zake ni kujifungia na kuchukia wenye nacho either wa nje ya nchi au wa ndani, mama Samia sera zake ni kuinua uchumi kupitia uwekezaji kutoka nje ya nchi au ndani mbona simple tu, unalia lia nini sasa?

Ishia hapo hapo kuhusu kusheheni maliasili inayotamaniwa! Hujui kitu bora kaa kimya.

Nchi nyingi sana zina maliasili na zinatuzidi, hatuna kitu kipya duniani wala hatuna cha ziada ila tuna maliasili kama yalivyo mataifa mengine. Jenga hii dhana kichwani kwako uelimike na uache kulaumu watu badala ya kujilaumu mwenyewe kwa kuendekeza siasa badala ya uwajibikaji
 
Kuna hii dhana ya kumsifia kiongozi fulani eti anaifungua nchi, kitu ambacho hata mwenyewe bila hata yeye mwenyewe anashangaa!!nchi ilifungwaje? nani aliifunga? maana serikali haijabadilika! Ilani ya uchaguzi inayotekelezwa haijabadilika!! Tatizo ni watu kujaribu kujikomba bila aibu!!

Watanzania tufanye kazi! hatuna mjomba kule nje ambako tunatamani kutuma mtu akalie lie hali!! Hakuna wa kutupa vya bure! sana sana mabeberu wanaitamani nchi yetu iliyosheheni maliasili waikombe! Tuwe macho!! Tukatae mikopo yenye masharti ya kutuondolea uhuru wetu juu ya maamuzi muhimu yahusuyo mambo ya kijamii na kiuchumi!! Tuchape kazi, tulipe kodi na Mungu atatusaidia!!
Aliyetamka kwamba anaifungua nchi ndio alibanwa na mtangukizi wake mawazo yake ya holela ndio madhara. Alichotamka JPM enzi za uhai wake ni kwamba angefunga makufuli wenye nguvu za kisiasa na kiuchumi waliokuwa wakitumia vibaya kuwadhulumu wananchi wa chini bila kuzingatia sheria
 
Hayo yote yalikuwa kimkakati a.k.a magufulidetoxification. Unfortunately form is temporary and classy is permanent!
 
Back
Top Bottom