mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,897
- 18,477
Wacha maneno wewe, nchi ilikuwa imefungwa na Magufuli yes kwani kuna ambae hajui? Kila Rais na sera zake na sio dhambi, MAgu sera zake ni kujifungia na kuchukia wenye nacho either wa nje ya nchi au wa ndani, mama Samia sera zake ni kuinua uchumi kupitia uwekezaji kutoka nje ya nchi au ndani mbona simple tu, unalia lia nini sasa?
Ishia hapo hapo kuhusu kusheheni maliasili inayotamaniwa! Hujui kitu bora kaa kimya.
Nchi nyingi sana zina maliasili na zinatuzidi, hatuna kitu kipya duniani wala hatuna cha ziada ila tuna maliasili kama yalivyo mataifa mengine. Jenga hii dhana kichwani kwako uelimike na uache kulaumu watu badala ya kujilaumu mwenyewe kwa kuendekeza siasa badala ya uwajibikaji
Aliyetamka kwamba anaifungua nchi ndio alibanwa na mtangukizi wake mawazo yake ya holela ndio madhara. Alichotamka JPM enzi za uhai wake ni kwamba angefunga makufuli wenye nguvu za kisiasa na kiuchumi waliokuwa wakitumia vibaya kuwadhulumu wananchi wa chini bila kuzingatia sheriaKuna hii dhana ya kumsifia kiongozi fulani eti anaifungua nchi, kitu ambacho hata mwenyewe bila hata yeye mwenyewe anashangaa!!nchi ilifungwaje? nani aliifunga? maana serikali haijabadilika! Ilani ya uchaguzi inayotekelezwa haijabadilika!! Tatizo ni watu kujaribu kujikomba bila aibu!!
Watanzania tufanye kazi! hatuna mjomba kule nje ambako tunatamani kutuma mtu akalie lie hali!! Hakuna wa kutupa vya bure! sana sana mabeberu wanaitamani nchi yetu iliyosheheni maliasili waikombe! Tuwe macho!! Tukatae mikopo yenye masharti ya kutuondolea uhuru wetu juu ya maamuzi muhimu yahusuyo mambo ya kijamii na kiuchumi!! Tuchape kazi, tulipe kodi na Mungu atatusaidia!!