Nakuthibitishia 4g inarudi, na Likuku linarudi kuwa Lukaku,
sababu ni chache sana kama mbili tatu tuu lakini za ukweli,
1. Usajili wa January
2. FA CUP na UEFA Champions league
Naamini January mou atasajili mchezaji mmoja tuu sijui mshambuliaji au kiungo lakini sio beki, hatoacha mchezaji wa maana mwenye namba kwenye kikosi chake, hii itawapa confidence wachezaji kwamba bado wanacheza kwenye malengo ya kocha na confidence ni silaha muhimu sana kushinda kwenye mechi ngumu..
Mkorogo wa FA CUP na Champions league utagharimu timu nyingi kwa sababu ya kucheza mechi mbili kwa wiki, jambo ambalo mou hana wasiwasi nalo sana kulingana na upana wa kikosi chake..
Mimi kama mshabiki wa man sijavunjika moyo kabisa bado naamini tutanyanyua makwapa zaidi ya mara moja mwaka huu