Hii gari niliyonunua sijapigwa hapa?

Hii gari niliyonunua sijapigwa hapa?

Nje ya mada kidogo... Wakuu mbona uko Beforward Altezza bei zimenyooka hafla? Yaani zinakimbizana na Mark X za 2010+ saiv!!
Hizo Altezza zimeshakula mods kama sijakosea mkuu
 
Mkuu,
Nakuhakikishia hujapigwa. Binafsi ilinitokea Be Forward nilinunua gari tarehe 19 May 2021 nimepokea gari August 21, 2021.
Tatizo corona imeleta shida biashara na usafiri wa meli. Nilipata gari bora kabisa.
Uwe mvumilivu hizo ni kampuni kubwa huwezi kudanganywa.
Yataka moyo kuvumilia mkuu, mdio maana wengine wanaamua kuzama yard za kibongo.

Nimeagiza inaingia trh 5 Jan. 2022 ila naona mbali kinoma[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Mkuu bora wewe umepewa hata tarehe. Mimi nimelipia tarehe 28 mwezi wa 7 na mpaka leo hata booking haijafanyiwa. Yani nmeulizia hiyo kampuni mpaka nimeamua kukausha tu.

Nasikia korona effect inafanya mizigo kuchelewa. Hata wafanyabiashara wengine naona nao wameathirika sana hawa wa nguo, electronics equips n.k ... Siku hizi watu wanaagizia vitu dubai kuliko China/Japani...

Tuvumilie mzee mimi sidhani hata hiyo ndinga nitaigusa maana naweza sepa kabla haijafika...
Mimi nilipigwa.
Jamaa waliniagizia gari nikakaa miezi mitatu imefikq gari sio yenyewe ila zinafanana.

Nikapelekeshana nao wakanirudishia hela.

Jamaa wanajiita MAGARI RAHISI.
 
Huduma za mwanzoni kama approval ya kupokea hela,inspection certificate umepata?. Kama tayari waulize meli gani wanategemea kutumia. Hii itakupa mwanga zaidi na kukuondolea panick. Kwa kifupi taratibu ya makampuni yako sawa. Upande wa booking inategemea vessel availability mara nyingi ni wiki 2 baada ya inspection
COVID-19 imefanya booking ya vehicle kuwa ngumu Sana
 
Back
Top Bottom