Hii haina tofauti na anaetumia "mkorogo" au "karolaiti"!!

Ni vizuri tukaanza na wewe!
Mie najikubali sana Eiyer, sifugi kucha wala siweki za bandia, sio mpenzi wa kushonea nywele bandia wala siweki dawa...kwa kifupi napenda kuwa natural zaidi....
 
na WANAUME pia wamo, wanajichubua, wanaweka nywele dawa, wanapaka lipstik, wanapaka wanja, wanavaa hereni sasa sijui na wanaumwe hawa wanatafuta nini
 
Pamoja na tatizo la kutokujiamini na kutojikubali kwa watumiaji...Mkorogo unasababisha madhara makubwa kwenye mwili wa mtumiaji kama ambavyo dawa za nywele zilivyo na madhara makubwa kwa watumiaji... Anayebisha ni wazi tu kuwa hajui lolote juu ya mambo hayo.
 
Mada kama hii kuhusu nywele imeanzishwa na Mzee Mwanakijiji kwanini zisiunganishwe?

Maudhui tofauti kabisa!Halafu hii haizungumzii nywele peke yake!
 
Mie najikubali sana Eiyer, sifugi kucha wala siweki za bandia, sio mpenzi wa kushonea nywele bandia wala siweki dawa...kwa kifupi napenda kuwa natural zaidi....

Hongera mama!Endelea hivyo hivyo!
 
hivi unakijua kipilipili kichaa wewe? Ukikichana kinajishika kwenye ncha ukitaka kuchana ukakojoe kabisa unaweza chafua mazingira

Jibubali tu,huwezi kutatua tatizo kwa tatizo!
 
Nywele zinazozungumzwa hapa ni zile original, zile za wafu, au aina zote mbili? nauliza tu.
 
Hii nilishawahi kuisoma kwenye makala moja ambayo ilitolewa kwenye gazeti sikuamini kuwa kuna watu wenye kufikiria so low kiasi hiki, kuna mambo mangapi yenye tija kulinganisha na hili? Wanawake wanaonyanyanswa, umasikini ubovu wa hudumaza jamii n.k. Afu mtu analalamikia nywele?! Eti kujikataa!! Mbona hamsemi uvaaji wa suti? Hatujaiga huu? Ah!
 
MJ1,nafikiri hujafikiri vyema,hebu fikiri tena najua utakuja na kitu chenye tija,siamini kama haujui uzito wa tatizo la kujikataa nani maradhi yenye ukubwa wa kutosha,stating point ni nywele lakini ina upana wake!
 
MJ1,nafikiri hujafikiri vyema,hebu fikiri tena najua utakuja na kitu chenye tija,siamini kama haujui uzito wa tatizo la kujikataa nani maradhi yenye ukubwa wa kutosha,stating point ni nywele lakini ina upana wake!

Naelewa unachofikiria but kwa nini uhisi kuwa na nywele za bandia ni kujikataa? Kwangu mimi haina tofauti na wale wamakonde wanaoweka chale na ndonya! Nao pia wanajikataa kaka au we unaangalia kwa upande mmoja tu? Mf mie MJ1 toka Pongwe Tanga, nikatoka nikenda tia ndonya puani na chale usoni kama wamakonde, ntakuwa najikataa?!

What matters is how U feel deep inside na katu si kwa mwonekano wa nje
 
Wanawake ni watu wa kujikataa sana, kwa mambo mengi, hata ngongingo walizopewa wanabadilisha wanaweka la mchina, nanihinoo b@@&kra wanaweka feki kwa kutumia sabuni za kichina femtight n.k.
 
Kwa kweli kuweka madawa kwene nywele ni kutokujikubali, hata watu waitete hoja hii kwa gharama kama ile iliotumika kwene uchaguzi mdogo wa Igunga ila ukwelei utabaki pale pale ni kujiona dhaifu, ni kujiona kwamba tumepungukiwa ikilinganishwa na wenzetu wazungu au jamii nyingine ya watu weupe wakati sio hivo kabisa. Hili sio kwa akina dada tu siku hizi hata wanaume wanasuka na kuweka madawa kwene nywele. Angalieni wasanii wa muziki wa bongo fleva, angalieni waigizaji wa filamu. kwa kweli ni kero na aibu sana. Huwezi kufananisha kubadilisha nguo na kuweka dawa kwene nyele haikubaliki. madhara yalioko kwene kemikali hizi za kubadilisha nywele kutoka kwene uasilia wake wa kawaida yana madhara makubwa sana si tu kwa mwekaji mwenyewe bali hata kwa kizazi chake.

Mi nafikiri ni wakati muafaka sasa watu wa jamii ya kiAifrika tujivunie maumbile na vile ambavyo Mungu wetu aliamua kutuumba tuwe hivo. Ukiwa nje ya Tanzania kwa kweli unatamani hata ufiche uso wako kwa maana wenzetu wazungu wanatushangaa eti sisi waafrika tunatamani kujibadilisha na kuchukua sura tofauti. Siku hizi ukiwa huku nje haswa ukiwa Ulaya au Marekani wazungu wanasema ukitaka kumwona muafrika kwa uasilia wake labda uende Afrika kwani wengi walioko huku wanume kwa wanawake wenye asili ya kiafrika wameshindwa kabisa kuhifadhi uasilia wao. Wengi wanweka madawa kwene nywele na kuzifanya ziwe refu kama za wazungu wengine wamejichubua kabisa na rangi zao hazina tofauti na wazungu. Kwa kweli this is a shame to Africans who are not proud of their nature.
 
MJ1,kuweka pini puani na kutoboa masikio na mengine hayawezi kubadili ujinga huu!Kile unachofikiri kinaonekana kupitia matendo yako,kama unajiamini umekamilika unakwenda kuweka nywele za bandia ili iweje?Au unajiona unapendeza na nywele zako za kipilipili unaenda saluni kuseti ili iweje?Ili ufanye haya ni lazima uwe mtupu ndani yako,we unafikiri Michael Jackson angetumia gharama zote hizo kama angekua anajiona ni kamili?Hoja zako hazina mashiko,wala huna point hapa!Usitetee jambo kwa sababu tu unalifanya!Nakushauri utulie coz huwezi kutetea maradhi kama haya ni aibu!
 
Kama unataka watu wenye mawazo tofauti na wewe wasichangie mada yako usiiweke jamvini sehemu ambayo ina watu wenye mawazo ya kila aina.Swala la kumwambia mtu mwingine hoja yake haina mshiko wala point ni indicator tosha kwamba wewe ndie ulieksa point ya kutetea hoja yako hivyo unamwaattack mtu badala ya kumpinga kwa hoja.Alafu eti unasema asitetee kitu kwasababu anafanya, unataka akuunge mkono kana kwamba maneno yako ni sheria? Sio kila mtuni bendera fuata upepo brah, ukiweka mada jamvini kua tayari kukutana na mawazo ambayo yanajitegemea na yanayopingana na wewe. And if you can't deal with that then keep your thoughts/beliefs and claims to yourself.
 
Duh, basi siku ya jf get together part siji maana mtanizodoa sana

1. Nina less wig refu hadi kiunono
2. Nna kope za kubust
3. Nyusi nimepiga tatoo from china
4. Kingo za mdomo zina tatoo from china
5. Nimepiga deki kiaina usoni, afu huwa natupia na poda za mac kufukia mabonde
6. Kifua nakibust kwa bra tu
7. Navaa skin tight za kuongeza makalio, naogopa kupaka dawa
8. Tumbo nalibana na yale mambo yetu, wadada mtakuwa mnayajua.

Am I fake?
 

Hapa tunagombana au vipi maana sikuelewi na wala sikutegemea ungetumia nguvu ya aina hii kutetea hoja yako! Mie sijabadili nywele zangu wala sina nywele ndefu ninachojaribu kusema hapa ni kuwa kila mtu anao uhuru wa kufanya akipendacho mradi hakuzuii kula wala kukunyima usingizi. Ningekuunga mkono kama ungeweza nithibitishia kuwa wote wanaobadili nywele hawajajikubali au wanabadili kwa ajili ya kukubaliwa na watu! Kila mtu anao utashi wake na si lazima akawa hajianimi.

Nijibu kwa hoja na si kuniattack personnally, that is what being a great thinker means!
 
Mkuu hiyo mada ni pana sana.

Vipi wewe nywele zikiwa ndefu huwa unanyoa? Mbona unakosoa kazi ya Mungu? Makucha je?

Nadhani kwa kutengeneza nywele kwa kina dada si sawa na kujichubua, sijui lakini mawazo yangu tu

mawazo yako ni sawa. Kuweka kitu katika hali nzuri ni muhimu bwana. Kama ndio hivyo hata ukishaoga na mafuta pia tusipake.
 

Mamii haina tabu nina uhakika ameghafilika tu hakumaanisha hicho alichokiweka hapo.

Mydia ametoa mfano wa Michael Jackson!!! That is an extreme maana yeye alishaweka wazi kuwa alikuwa anachukia kuwa Mweusi sasa atafananishwa na mdada ambaye ametaka tu kutengeneza nywele ili kutia chachandu unadhifu na urembo wake!!
 
Nywele zinazozungumzwa hapa ni zile original, zile za wafu, au aina zote mbili? nauliza tu.

ni nywele original tunaambiwa wanawake tusizipake dawa wala mafuta na kuzichana pia tusizichane maana huko ni kujikataa. Lol
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…