Hii haina tofauti na anaetumia "mkorogo" au "karolaiti"!!

Mada zake zote hua anafanya hivyo dearest.Mtu akipingana nae basi ataambiwa hajui kitu/hana hoja.

Neway kuhusu huo mfano mimi ndio maana hata sikutaka kuugusia. Inabidi tuache mpaka kutoboa masikio, kujipulizia marashi, kusuka hata twende kilioni ili tusionekane tunajikataa.
 
Na kusema ukweli madhara hayaishii kwa wao tu...yanaweza kwenda hata kwa watu wengine na hasa wapenzi wao pia(waume, watoto nk) kwa njia ya kugusana, harufu/gas nk.
 
Mh hebu mtujuze kwa nmifano sie wengine matomaso! Nywele za bandia mfano zimeleta madhara yepi? Cancer? Mtindio wa ubongo? Kuna kesi vivid ambazo zina direct link na nywele za akina dada? Mwenzenu mie sijui zaidi ya kuona mdada anapendeza kama zina madhara hebu nijuzeni kwa ushahidi maana naamini tutakuwa nayo mingi tu maana wadada sie ndo imekuwa sehemu ya maisha yetu wengine for over 20 years now! Wadada wengi walianza kutengeneza nywele zao tangu wakiwa mashuleni!! Hebu nitoeni hili tongo la macho mwenzenu!
 
Unajua watu wanaona ngozi nyeupe kuwa ndo ya maana sana, huu ni ujinga mkubwa sana. Mtu wa kwanza Adamu hakuwa na rangi yoyote ile kati ya tuzionazo leo, rangi zote za ngozi unazoziona leo ni matokeo ya dhambi. Kwa kifupi ni rangi za laana. Lakini wapumbavu wengi wanaamua kukataa ngozi nyeusi ya laana anajiongezea ngozi nyeupe. Kwa hiyo anakuwa na rangi mbili za ngozi zilizolaaniwa. Yaani ni laana squared. Handsome wa mama nawaonya mnaomfundisha kazi Mungu kana kwamba hakujua alichokuwa anakifanya tubuni maana msipotubu mtachomwa moto hadi mjishangae.
 

Wewe unaonekana una wigi kichwani ndo maana mm uwa na waeshimu wanawake ambao najieshimu lakini kama unavaa mawigi na kubadilisha nywele mm nawaona kama makahaba tu kama wabuguruni kwani wanauza utu wao na mtu ambaye kabadilisha ngozi yake namuona kama kahaba tu
 

Ni mtazamo wako wala sikupingi! So kwako anayevaa wigi ni sawa naanayetumia mkorogo.kuna mwingine anaonaafadhali ya wigi kuliko mkorogo na mwingine anaheshimu wote. So ni suala la mitazamo.mwingine anampa hela kabisa mkewe ili akabadili nywele ili awe kama wengine.

Naheshimu mtazamo wako
 

Kwa hili nitakuunga mkono. Halina kupingwa.
 
Huu umbea wa wanaume kujifanya hatupendi wake zetu wapendeze tunautoa wapi? Wote tunajua minywele yetu waafrika ilivyo mibaya na migumu kuichana kiasi ukiilazimisha inakatika. Sasa mimi sioni similarity ya kutengeneza nywele na kujichubua. Suala ni mahitaji. Nyie mnaojishaua hapa ndio wa kwanza kukurupukia videmu vilivyoweka wave kwenye nywele lkn kwa kuwa hatufahamiani kila mtu anaongea utumbo wake.

Nani kati yenu atapenda kufuatana na mkewe akiwa amesuka mibutu kama sio kuleta ufukunyuku hapa?
Wewe mwenye mada hii anzia kwanza kukataza kutoga masikio na kutahiri wanaume kwani nako ni kubadili maumbile. Na unapozungumzia suala la kujikubali hebu jiulize hili kwanza: TUNAPOTUMIA KIINGEREZA MAOFISINI NA SHULENI, NI KUWA HATUKIKUBALI KISWAHILI AU NI MAHITAJI NDIO YANATUFANYA TUKIELEKEE KIINGEREZA?

Ushauri kwa wadada: Msijichubue na wala msiongeze makalio, lkn wekeni nywele dawa na mtinde nyusi. Pakeni kucha rangi na midomoni wekeni lip shiners za kufa mtu. Kwa kifupi pendezeni muipambe dunia na moyo wa Shizukan ufurahi....msisikilize maneno ya watu ambao wake zao mawigi hayawapendezi. Nywele za kiafrika ngumu bana
 
Kutengeneza nywele na kujichubua havifanani kabisa ...
Nywele ni nywele acha wapendeze mkuu. Kwa wanaume zikiwa ndefu sana ni uchafu kwa wanawake ni fahari kwao.
 
Kubadili nywele au kuvaa wig sio kujikataa jamani, ni kuongeza kujiamini zaidi. Nakumbuka mama yangu miaka ile ya 60 alikuwa akipasha chanuo ktk moto na kuchana nywele zake then akizipaka mafuta ya samli zinakuwa kama za kiarabu. Kutia dawa ni baada ya tekinolojia kukua badala ya kuchana kwa chanuo la moto ndio wanatia dawa. Tukubali au tukatae, bibi na mama zetu walikuwa wakijikoroga kwa mayai na unga wa dengu..na wakitengeneza nywele. Mikorogo na wig ni advanced tec. Nawasilisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…