knows
JF-Expert Member
- Nov 9, 2021
- 1,453
- 2,234
Habar wana jf,
Natumain mko salama wote ni wazima mungu anaendelea kutupigania.
Naomba niende kwenye point staki mambo mengi sababu siko sawa kiukweli napitia wakati mgumu bas tu.
Niko na mwanamke tupo kwenye mahusiano huu mwaka wa 3 sasa japo ups and downs ni nyingi sana ila tunasonga, kunakipindi nilisafiri kikazi kwenda mkoani kwa muda wa kama 2 months umbali ule ulianza kuleta shida maugonvi yakaanza kuwa mengi sana japo tulikuwa tunajaribu sana kuwekana sawa.
To cut a story short baada ya kurud niligundua kuwa kacheat sababu kila alipokua akikaa na mimi akawa kama anakitu anajutia kupitia yale maugonvi yetu na baada ya kumbananisha alilia sana na kukili kuwa nikweli na kusema yale maugonvi yetu alikua yanamvuruga akili so hiyo siku alikunywa sana.
Daah kiukweli niliumia sana wakuu baada kujua na ndio siku nilijua kuwa usaliti unaumiza sana hasa kwa mtu unaempenda sikutaka kuendelea tena kuwa karibu nae nilikaa mbali ila kwake ilikua ngumu sana kukubali wiki nzima yeye ni kulia tu na kujutia usaliti wake hali ilienda wiki nzima.
Kifupi yaliisha nikamsamehe maisha yakaendelea mbaka now sasa shida ni kwamba kinacho nitesa ni ile memory tu kuna kipindi inaibuka tu na kuanza kunitawala kichwani na kuni stress kisha kunisabishia maumivu makali.
Simchukii nampenda kama kawaida ila kuna muda ukipita ile memory inakuja kichwani kwamba Kwaiyo alienda kulala na mwanaume mwingine seriously hii kitu inanipa hard time sana wakuu inanipa maumivu makali sana japo staki kumwambia sababu nikimwambia namjua ataumia sana na kujistress na hatokua na amani kila akiwa na mimi na mimi hicho staki apitie nataka awe happy tu.
Ni kweli anajua nimesamehe na nikweli ila sijasahau najitahid sana mbaka nakua sawa nasahau ila kuna kipindi hali ya kukumbuka inajirudia tena naanza kupitia maumivu makali.
Leo niliamka vizuri na tukawa powa tu nikaenda kazini kipindi nipo kazini ile hali ikanijia aisee maumivu ni makali mbaka narud home nimeingia saa 3 usiku home nikajitahidi sana asijue chochote lakini hata nikimzuga vip huwa anajua kama siko sawa sjui Kwanini nimezuga kuwa niko na furaha kama nilivyo ondoka asubuh lakin nikashangaa ananiambia nahsi kama hauko sawa nini tatizo.
Kiukweli sikuwa sawa kweli moyoni nina maumivu ila nikimwangalia Natamani kumwambia nini napitia lakin najizuia ili nisimfanye aanze kujskia vibaya na kutokua na furaha.
Wakuu naomba msaada kwa ushauri wenu tu bas napitia wakati mgumu mbaka kuna muda nahsi kwenda kwa Therapist au cancellar labda nitapata kitu 😔😔 .
Karibu kwa ushauri wenu Mshana Jr na wengine wote nawategemea
Wale wakunisema Hapana nawaomba sababu kwa hali nilikuwa nayo na ninayopitia ukinisema unazidi kunivurga na kufanya kunipunguzia uwezo wa kufikir jins ya kutatua tatizo.