Hii hapa Television ya kumiliki kulingana na kipato chako

Hii hapa Television ya kumiliki kulingana na kipato chako

Kila mtu anapenda kumiliki kitu kizuri ila baadhi kipato hakiruhusu, hii imepelekea kuwepo kwa bidhaa za kila aina sokoni ili kubeba pesa yoyote mteja aliyonayo. Kwa upande wa TV zipo kampuni nyingi sana na hapa nazigawa kwenye makundi matatu

1. Samsung LG SONY Panasonic
2. TCL Hisense Haier
3. Alitop Aborder Ailyons Solarmax Skyworth Mr.UK Mewe Boss e.t.c

Kutoka kundi namba moja TV ambazo zimezoeleka sana ni LG na Samsung, tofauti ya hawa wawili LG anakupa picha kali (real 4K) wakati Samsung anakupa picha kali pamoja na frame kali kuliko frame ya LG. LG anakupa durability na kioo chake ni kigumu kupasuka kuliko Samsung.

LG wanakupa series 4 ambazo ni (UHD NANOCELL QNED OLED) Samsung wao wana (UHD QLED OLED)

Bei zake zinapanda kulingana na latest series, kumiliki TV za kundi hili lazima uwe una pesa kulingana na series unayotaka pamoja na inches ngapi unahitaji na ndio TV zenye bei kubwa zaidi sokoni.

Namba mbili tukianza na TCL ni TV nzuri ambayo kama unapenda kitu kizuri na umeshindwa kufika bei ya hapo juu, TCL wanakupa picha nzuri pia inadumu ukiweka ndani ni mkataba.

Tukija kwenye hisense wenyewe wana series za bei ndogo na kubwa, hawa jamaa wana TV nzuri kulingana na bei zao ila quality yake haiwafikii hao wazee hapo juu, pia ndio TV ambazo zinauza sana sokoni kwa sasa kutokana na jina lakini pia bei zao zinaendana na watu wa uchumi wa kati, hawa jamaa baadhi ya series zao zinarudi sana kwa fundi ila ukiotea ni mkataba.

Haier wenyewe wamekuja karibuni kwenye soko la Tanzania na wanafanya vizuri, bei zao zipo chini kidogo ya Hisense, ukikosa pesa ya kununua hisense basi kimbilia hapa kabla hujafika namba tatu kwa wachina wenyewe.

Kundi namba tatu nimeweka kampuni za kichina zilizojaa sokoni, hawa wameamua kumuuliza mteja ana bei gani kisha watengeneze bidhaa, kwa hili kundi TV yenye picha nzuri ni Alitop na Skyworth lakini pia bei zao ni nzuri unaweza kumiliki 43" below 450k price; Aborder wanakupa durability nzuri pia.

Uliza swali lolote kwenye coments kulingana na mada, ukitaka kujua bei weka kampuni gani na inches ngapi, lakini pia series kama haufahamu uliza nitajibu.
Ciao
Nimesikia kuwa Hisense huwa zinatoka sana mistari hasa kuanzia inch 43 kwenda juu
 
Rising Android tv nchi 43 naenjoy mno, picha kali na nimekaa nayo muda mrefu tu. Nyie emdeleeni kununua majina ila mchina anakuja na mizigo mikali sana siku hizi.
Mkuu hiyo Risingi ipigishe ON masaa 20+ alaf mchukua LG ama Samsung mpigishe masaa hayo hayo alafu uone nan atakufa mapema

Durability always mchina hana hiyo kanuni
 
Nimesikia kuwa Hisense huwa zinatoka sana mistari hasa kuanzia inch 43 kwenda juu
Inategemea mkuu, watanzania akiharibikiwa kitu nyumbani kwake anafanya generalisation kisha kila mtu anamweleza hivo muda mwingine unakuta yeye ndiye aliyekosea matumizi, Hisense wana hizo case ila kwa latest series zao hiyo case haipo sana
 
Back
Top Bottom